Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 28 Shawwal 1446 | Na: H.T.L 1446 / 15 |
M. Jumamosi, 26 Aprili 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kisimamo cha Kulaani cha Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon jijini Beirut
“Kutoka Beirut hadi Gaza, Kuweni Answari wa Mwenyezi Mungu, Enyi Majeshi ya Ummah”
(Imetafsiriwa)
Mamia ya Mashababu (wanachama) na wafuasi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon walishiriki katika kisimamo cha kulaani kilichoitishwa na Hizb, baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 25/4/2025, jijini Beirut, mbele ya Msikiti wa Mohammad Al-Amin. Kisimamo hicho kilikuwa na kichwa “Kutoka Beirut hadi Gaza, Kuweni Answari wa Mwenyezi Mungu, Enyi Majeshi ya Umma,” ambapo mabango yalinyanyuliwa yakitaka kuhamasishwa kwa majeshi, kupinduliwa kwa viti vya utawala vya madhalimu, na kunusuriwa kwa Gaza kupitia jihad na silaha.
Washiriki pia waliimba kauli mbiu za kuinusuru Gaza, zikiwemo: “Hatutaki kushutumu na kulaani, tunataka Khaybar nyengine,” “Enyi majeshi ya Waislamu, simameni muinusuru Dini hii,” na “Umma unataka tangazo la jihad”...
Zaidi ya hayo, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Ustadh Ahmad Al-Abdullah, alitoa hotuba ya kusisimua ambapo aliyataka majeshi ya Waislamu kufuata mfano wa vizazi vya mwanzo vilivyoinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu. Alisisitiza kuwa, Gaza na Palestina yote ni kadhia za Kiislamu, na suluhisho lake liko katika kuyakusanya majeshi na kushiriki katika jihad dhidi ya Mayahudi.
Vile vile alisisitiza kwamba hilo linaweza kupatikana tu kwa kuwapindua madhalimu, kuziunganisha ardhi za Waislamu, kusimamisha Khilafah, na kuyakusanya majeshi. Fauka ya hayo, aliregelea kauli ya Netanyahu kuhusu Mayahudi kutoruhusu kusimamishwa Khilafah katika mwambao wa Bahari ya Mediterania, na kubainisha kwamba kuisimamisha ni faradhi juu ya Waislamu na ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hakuna atakayeweza kuzuia kusimamishwa kwake.
Wakati wa kisimamo hicho, matoleo yaligawanywa yakiangazia faradhi ya kuinusuru Gaza.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/lebanon/4647.html#sigProIdfec88e1a5e
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |