Afisi ya Habari
Malaysia
H. 10 Rajab 1446 | Na: HTM 1446 / 16 |
M. Ijumaa, 10 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Unafiki wa Kisiasa katika Demokrasia Kamwe Hautaisha Mpaka Tuubadilishe kwa Siasa za Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 06/01/2025, rufaa ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Najib Tun Razak kuhusu kuwepo kwa amri ya nyongeza ya Mfalme, inayomruhusu kutumikia kifungo chake kilichosalia chini ya kifungo cha nyumbani, imekubaliwa na mahakama kwa wingi wa 2-1. Majaji wa Mahakama ya Rufaa kisha wakaamuru kesi hiyo irudishwe katika Mahakama Kuu ili ombi la Najib la uhakiki wa mahakama lisikizwe na jaji mpya. Amri hii ya nyongeza, ambayo ni sehemu ya mchakato wa msamaha wa kifalme, imekuwa jambo la kawaida, ambalo halijawahi kutokea katika asili yake. Sambamba na hilo, kulikuwa na jambo jengine - mkusanyiko mkubwa wa kuonyesha mshikamano uliokusanyika nje ya mahakama, ulioandaliwa na vyama ambavyo hapo awali vilikuwa wapinzani wa kisiasa wa Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Kufuatia uamuzi wa mahakama uliothibitisha kuwepo kwa amri ya nyongeza, suala la “derhaka” (kutotii) kwa Mfalme lilitumiwa sana na wapinzani, wakielekeza kwa serikali kuficha agizo hilo tangu kutolewa kwake Januari 29, 2024. Hata hivyo, tuhma hii inaonekana kurudi nyuma kwa vile upinzani wenyewe ulikuwa na rekodi ya “kutotii”. Suala la amri ya nyongeza limefunika suala halisi katika kesi hii. Upinzani na wafuasi wao wanaonekana kupuuza kwa makusudi ukweli kwamba, chini ya mfumo wa kidemokrasia wanaoutetea, Najib amepatikana na hatia si katika moja tu, bali katika ngazi tatu za mahakama, na alikuwa amepitia kesi ya kina na majaji wakuu zaidi wa taifa na kutetewa na timu mashuhuri ya mawakili. Licha ya hayo yote, Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Malaysia anasherehekewa kama shujaa mkubwa asiye na hatia na upinzani na wafuasi wake.
Enyi Waislamu! Katika Uislamu, mtu akipatikana na hatia na Kadhi (hakimu) na kuhukumiwa, hakuna hakimu mwengine mwenye mamlaka ya kusikiliza tena, kubadilisha, au kubatilisha hukumu hiyo. Kwa maana nyengine, uamuzi wa hakimu ni wenye kupaswa utekelezwaji wake na lazima utekelezwe. Bila kujali mkosaji ni nani, awe miongoni mwa watu wa kawaida au kiongozi, maskini au tajiri, mwenye ushawishi au asiye na ushawishi, mara tu wanapopatikana na hatia, hukumu lazima itekelezwe. Hata Khalifa au mkuu wa nchi hawezi kutoa msamaha kwa mkosaji. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitukumbusha kwa nguvu sana hili: :«إِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الضَّعِيفُ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا» “Watu waliokuwa kabla yenu waliangamia kwa sababu anapoiba mtu mtukufu miongoni mwao, walimwacha, lakini kama mtu dhaifu miongoni mwao akiiba, walimtimizia adhabu ya kisheria. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau kama Fatimah, binti ya Muhammad, angeiba, ningeliukata mkono wake” [Bukhari].
Hadithi hii kwa uwazi na kwa kukatikiwa inathibitisha kwamba hakuna undumakuwili katika Uislamu na hakuna msamaha unaoweza kutolewa na yeyote, kwa wale wanaokiuka Hudud za Mwenyezi Mungu (swt). Hii ndiyo hukumu ya Kiislamu katika mambo kama hayo ambayo ni lazima izingatiwe na kutekelezwa. Kama hadith hii ingefuatwa, suala la msamaha au amri ya nyongeza kama “njia ya kutokea” kwa wakosaji wa hali ya juu, ambayo kwa sasa inajadiliwa, haingetokea.
Kipengee chengine ambacho ni muhimu vile vile ni nafasi ya mtu ambaye aliwahi kuwa madarakani lakini hakutekeleza Hudud wa Mwenyezi Mungu (swt), au baya zaidi, ambaye wakati fulani alitangaza wazi kukataa kwake kutekelezwa kwa Hudud za Mwenyezi Mungu (swt) - kosa kama hilo la uasi ni kosa kubwa sana! Watawala wa namna hii wasiheshimiwe bali wakataliwe. Mtawala yeyote aliyepewa mamlaka na Mwenyezi Mungu, lakini akapuuza kusimamisha Hudud Zake, hakika huyo ni anasaliti amana ya Mwenyezi Mungu. Yeye (swt) asema (swt):
[وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُهِينٌ]
“Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.” [An-Nisa' (4): 14].
Kukuiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa kufeli kushikamana na sheria zake kunawakilisha uasi wa hali ya juu kwa Mwenyezi Mungu (swt), hasa kwa wale walio na mamlaka, au wameshika madaraka hayo. Kwa Waislamu, hili liwe kipaumbele cha kwanza katika masuala ya kisiasa – jukumu la kuwahisabu watawala wanaoonyesha kumuasi Mwenyezi Mungu (swt). Mtazamo huu unajumuisha kiini cha kweli cha ushiriki wa kisiasa katika Uislamu. Kwa hakika, siasa ndani ya Uislamu inazunguka katika usimamizi wa mambo ya umma. Watawala wanatakiwa kutawala kwa mujibu wa Uislamu, huku wananchi wakiwa na wajibu wa kuwahisabu watawala, pia kwa mujibu wa Uislamu.
Inaumiza moyo kuona kila aina ya siasa chafu ambazo zimeegemezwa kwenye maslahi yanayotawala Malaysia na ulimwengu wa Kiislamu leo. Wanasiasa wengi wanaonekana kuongozwa na tamaa isiyokoma ya madaraka, mara nyingi wakitumia njia yoyote muhimu ili kufikia malengo yao, bila kujali Halal au Haram, na kutoonyesha aibu kwa unafiki wao. Demokrasia imewafanya waamini kwamba miungano ya kisiasa na visasi lazima vizingatie maslahi. Kwao, hakuna dhana ya “marafiki wa kudumu” au “maadui wa kudumu”, bali “maslahi ya kudumu.” Pekee.
Enyi Waislamu! Kwa muda mrefu sana, tumeshuhudia unafiki wa kisiasa uliomo katika mfumo wa demokrasia, mfumo ambao unaendelea kutuangusha na utaendelea kufanya hivyo isipokuwa tukichukua hatua za dhati kuelekea mabadiliko ya maana. Mandhari ya kisiasa nchini Malaysia na katika ulimwengu mzima wa Kiislamu bado inazongwa na kutomtii Mwenyezi Mungu (swt), ufisadi na hadaa, huku wanasiasa wakiendelea kushikamana na demokrasia—mfumo uliokita mizizi katika itikadi za Magharibi ambazo zinapingana kabisa na mafundisho ya Uislamu. Ni muhimu kwamba tusimame kutafuta mfumo wa kisiasa wenye kuleta mabadiliko, unaoongozwa na viongozi wanyoofu ambao wanashikamana tu kanuni za Uislamu pekee. Tunakuombeni mushirikiane na Hizb ut Tahrir katika kufuata njia ya haki, kwa kufuata mtindo wa kisiasa wa kipenzi chetu Mtume (saw). Kwa pamoja, hebu na tuukatae mfumo mbovu wa Kijahiliyyah (demokrasia) na tujitahidi kusimamisha mfumo wa Uislamu (Khilafah), ambao peke yake unaweza kuleta uadilifu, ustawi, na radhi za Mwenyezi Mungu (swt).
Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Malaysia |
Address & Website Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor Tel: 03-8920 1614 www.mykhilafah.com |
Fax: 03-8920 1614 E-Mail: htm@mykhilafah.com |