Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Jumada II 1442 Na: 1442 / 44
M.  Jumatatu, 25 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sera ya Kujizuia na Hakikisho la Kutokuwa na Vita Juu ya Kashmir Iliyokaliwa Imeishajiisha Tu Dola ya Kibaniani Kuyaelekeza Majeshi Mpakani na China

(Imetafsiriwa)

Kukaririwa kwa amani na India na watawala wa Pakistan sasa kumefichuka kikamilifu kama utiifu wa hila kwa Amerika, kwa gharama ya maslahi muhimu ya kitaifa. Dola ya Kibaniani inataka kuhamisha askari shambulizi kutoka mpakani mwa Pakistan, hadi mpakani mwa China, hivi karibuni. Kwa hivyo, tunauliza, ni juu ya maagizo ya nani ambapo serikali ya Modi imehakikishiwa mpaka tulivu na Pakistan, ili jeshi oga la India liweze kupata ujasiri wa kupeleka tena vikosi ziada ili kukabiliana na China? Baada ya kuitelekeza Kashmir Iliyokaliwa kwenda India kwa maagizo ya Amerika, watawala wa Pakistan sasa wanatimiza agizo la Amerika la kuzuia majeshi yetu matukufu kutokana na kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa, licha ya kuwa na uwezo kamili wa kufanya hivyo. Kwa hivyo, wasaliti katika uongozi wa Pakistan wanaisaidia Amerika katika kuendeleza mpango wake wa India kukabiliana na China na Waislamu wa eneo hilo, bila changamoto yoyote kutoka Pakistan.

Tangu 5 Agosti 2019, watawala wa Pakistan wamewanyima wanajeshi wenye ari wa Pakistan heshima ya kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa, licha ya uchokozi wa kuendelea wa India katika Mpaka wa Udhibiti na Mpaka wa Kufanya kazi. Kwa kuongezea, watawala wa Pakistan wainyonga Jihad huko Kashmir chini ya pazia ya kutimiza matakwa ya FATF, na vilevile wakitaja hofu ya vita vya nyuklia na umasikini. Kinachozidisha usaliti ni kwamba hili linafanyika katika wakati ambapo ni dhahiri India ni dhaifu mbele ya China, ambapo uchumi wake umechanika pamoja na suala la virusi vya Korona kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, huku jeshi lake linatetemeshwa na Waislamu wenye ujasiri wa Kashmir Iliyokaliwa. Mtawala ambaye ni mkweli kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) peke yake bila shaka angewakusanya wanajeshi wanaotafuta shahada na ushindi, wakitumia kikamilifu hali nzuri ambazo wameruzukiwa na Mwenyezi Mungu (swt). Lakini, badala yake, wasaliti katika uongozi wa Pakistan wametabanni msimamo dhaifu kama huu, ambapo Dola dhalimu ya Kibaniani ina ujasiri, hata katika hali yake dhaifu, kupeleka tena vikosi kukabiliana na China.

Enyi Simba wa Majeshi ya Jeshi la Pakistan! Kila siku inayopita inaweka wazi kuwa nguvu ya kistratejia ya Pakistan inatumiwa na Amerika kutokana na vibaraka wanaounga mkono Amerika waliowekwa ndani ya uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan. Wakiwa wamejitolea kikamilifu kwa minyororo ya wakoloni na minyororo ya sheria za kimataifa, mifumo ya kimataifa na mashirika ya kimataifa, wasaliti hawa wanakataa kuutekeleza Uislamu kindani na sera ya kigeni ya Uislamu ya Dawah na Jihad, nje. Wamesimama mabegani mwenu, huku wakisisitiza utiifu wenu, wasaliti hawa ni walinzi wa maslahi ya Amerika na India katika eneo letu. Je! Wakati haujawadia sasa wa kuwakamata wasaliti hawa kwa shingo zao za uongo? Ni nani kati yenu atafufua urithi mtukufu wa baba zetu wa Kiislamu? Nyinyi ni wana wa wale waliowashinda Wamongolia, Watartari na majeshi ya msalaba. Nyinyi ni wana wa wale waliotawala Bara Hindi, kwa yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliyateremsha, kwa karne nyingi. Toeni Nussrah yenu sasa kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ili Khaleefah muongofu awaongoze katika vita na maadui wa Ummah, kuwalazimisha kurudi nyuma, kushindwa na kudhalilishwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [Surah At-Tauba 9:14].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu