Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  3 Ramadan 1443 Na: 1443 / 50
M.  Jumatatu, 04 Aprili 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ondoeni Demokrasia na Msimamishe Khilafah kwa ajili ya Mabadiliko ya Kweli, kwa Kutabikisha Yale Yote Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt)

 (Imetafsiriwa)

Shina la matatizo yetu sio ni nani anayetutawala, bali ni kipi anachotutawala nacho. Maadamu Pakistan inatawaliwa na sheria zilizotungwa na mwanadamu chini ya Demokrasia, badala ya Shariah iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) chini ya Khilafah, kamwe hatutaona mabadiliko ya kweli. Hatutaona mabadiliko ya kweli ikiwa Imran Khan, Nawaz Sharif au Zardari watafanikiwa katika uchaguzi. Zaidi ya hayo, jenerali Bajwa au Jenerali Faiz Hameed au jenerali mwingine atafaulu kuwa mkuu wa jeshi baada ya Novemba 2022, hakutakuwa na mabadiliko ya kweli.

Katika Demokrasia, watawala na mabunge hutunga sheria kulingana na matakwa na matamanio yao yanayotusababishia mateso, ambapo katika Uislamu sheria ya nchi inatokana na nususi za kiwahyi zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) ameonya,

 [وَأَنْ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Mai’dah 5:49]. Demokrasia inawaruhusu wenye nguvu kutunga sheria zinazoafikiana na maslahi yao, huku katika Uislamu sheria lazima ziwe madhubuti kwa mujibu wa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume.

Kuionda Demokrasia na kusimamisha Khilafah pekee ndiko kunakoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika uchumi wetu. Demokrasia inahakikisha kwamba viwango vya riba vinapandishwa kwa wale wanaofanya biashara katika deni la taifa la Pakistan. Demokrasia huongeza ushuru ili kumudu malipo ya riba ili kupata faida kwa wale wanaofanya biashara ya deni. Demokrasia hubinafsisha rasilimali za nishati na madini, hivyo kuwanyima wananchi kwa ajili ya kuyapa faida makampuni ya kigeni na ya ndani.

Ni Khilafah ndiyo itakayoiokoa Pakistan kutokana na mtego wa deni kwa kuharamisha riba, kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ameamuru hilo katika Quran Tukufu. Ni Khilafah ndiyo itakayowatoza tu wenye uwezo wa kifedha pekee, kutoa misaada kwa masikini na wenye deni, wanaostahiki Zaka. Khilafah ndiyo itakayohakikisha kwamba nishati na madini ni mali za umma, ambao mali yake nyingi inatakiwa kutumika kwa mahitaji ya watu, kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliliweka hilo katika Sunnah zake.

Kuiondoa Demokrasia na kusimamisha Khilafah pekee ndiko kunakoweza kuhakikisha usalama wetu. Demokrasia imewaruhusu watawala kuharamisha Jihad dhidi ya wale wanaokalia kimabavu Ardhi za Kiislamu, wakitangaza Jihad kuwa ni hiyana na ugaidi. Demokrasia inazuia uhamasishaji wa vikosi vyetu vya kijeshi, kuwashajiisha adui zetu kutushambulia. Demokrasia inakataza kuondolewa kwa mipaka ya kitaifa inayogawanya Ardhi za Waislamu, kutugawanya na kutudhoofisha mbele ya maadui zetu.

Kusimamishwa tena kwa Khilafah kutatutia nguvu na kuwalazimisha maadui zetu kurudi nyuma. Khilafah itakomesha muungano na maadui zetu, ikiwemo Marekani, kukata uhusiano wa kidiplomasia, kijeshi na kiuchumi. Khilafah itafanya kazi ya kuziunganisha Ardhi za Kiislamu kama dola moja, yenye nguvu na rasilimali tele. Khilafah itatimiza faradhi ya Jihad kuikomboa Ardhi ya Kiislamu inayokaliwa kwa mabavu. Khilafah itatimiza faradhi ya kubeba Dawah kwa wanadamu wote, na kuondoa vikwazo kupitia Jihad, ili Uislamu utawale juu ya dunia nzima kwa mara nyingine tena.

Kwa hivyo, Enyi Waislamu wa Pakistan, msipoteze tena nguvu zenu katika kuitekeleza demokrasia. Fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, kutimiza faradhi ya kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu