Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Sha'aban 1443 Na: 1443 / 48
M.  Jumatano, 23 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Khilafah Pekee Ndiyo Itatuondoa kutoka kwa Mfumo wa Kikoloni wa Kiulimwenguni Inaohakikisha kuwa Hifadhi ya Pakistan yenye Thamani ya Reko Diq Inakabidhiwa Wakoloni wa Magharibi.

 (Imetafsiriwa)

Upanga wa mfumo wa kimataifa umewekwa kwenye shingo ya Pakistan ili kuinyima umiliki wake kamili wa hifadhi kubwa ya dhahabu na shaba huko Reko Diq, ukikabidhi haki nyingi za umiliki kwa Kampuni ya kisasa ya India Mashariki. Kampuni ya Barrick Gold imemaliza mzozo wa muda mrefu na Pakistan na sasa itaanza kuendeleza mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya uchimbaji madini ya dhahabu na shaba duniani, chini ya makubaliano yaliyotiwa saini mnamo tarehe 20 Machi 2022. Ili kupurukusha kile ambacho Pakistan imepoteza, serikali inaelekeza kuondolewa kwa adhabu ya dolari bilioni 11 iliyoamriwa na mahakama ya usuluhishi ya Benki ya Dunia, Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni wa dolari bilioni 10 huko Balochistan na kwamba sasa asilimia 50 itamilikiwa na Barrick Gold, chini kutoka asilimia 75 chini ya makubaliano ya awali, kwa ushirikiano na Antofagasta ya Chile.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Tunauliza kwa nini ni lazima tutoe mabilioni ya dolari za akiba ya Reko Diq kwa Kampuni ya kisasa ya India Mashariki, wakati tunaweza kuchimba madini hayo na kujitajirisha wenyewe? Kuna maana gani ya ‘makubaliano’ yaliyofanywa kwa upanga wa mfumo wa wakoloni shingoni mwetu? Kwa nini mtu akabidhi asilimia 50 ya mali yake kwa maslahi ya mkoloni kafiri? Ni kipi kinachotuzuia kuiendeleza neema hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ili tupate faida yake kamili, asilimia 100? Baada ya yote haya, kwa nini Pakistan haiwezi kusimamia mradi huu wa kila mwaka na kuufadhili yenyewe? Je, ufadhili huu ni zaidi ya trilioni tatu zinazofanywa kama malipo ya riba kila mwaka? Je, teknolojia ni ya juu zaidi kuliko urutubishaji wa uranium ambayo tuliijua kutengeneza silaha za nyuklia? Zaidi ya yote, tunawezaje kukaidi hukmu ya Kiislamu kwamba rasilimali za madini na nishati ni mali ya umma, ambayo manufaa yake kamili ni kwa watu wote na hivyo umiliki wake hauwezi kutolewa kwa mtu binafsi au kampuni yoyote, yote kwa jumla au sehemu yake?

Uamuzi kuhusu mali yetu ya umma unafanywa na mamlaka na mahakama za makafiri, iwe ni Benki ya Dunia au mashirika ndani ya Uingereza na Marekani. Hii ni huku ikiwa imeharamishwa waziwazi katika Shariah kwa Waislamu kuwasilisha mambo yao kwa uamuzi mbele ya mamlaka ya kitaghut ya kikafiri. Iwe ni Mkataba wa Maji wa Indus au kadhia ya Reko Diq, maamuzi ya taasisi hizi za kikoloni daima ni dhidi ya Waislamu. Vyombo hivi ni sura na madalali tu wa dola za kikoloni na kampuni zao za kimataifa. Pia ni udanganyifu ulio wazi kwamba Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni unaweza kuleta mabadiliko ya ustawi wa kiuchumi. Kabla ya Reko Diq, umma uliuziwa ndoto kama hizo kuhusu mradi wa China Metallurgiska Group Corporation wa mradi wa mgodi wa Saindak Copper-Gold, Chaghi. Hata hivyo, yote yaliyotokea ni kwamba wakoloni wa Kichina walinufaika, huku Waislamu wa Balochistan wakiendelea kuzama ndani ya umaskini wa kutisha. Hali ni hiyo hiyo kwa hifadhi ya mafuta nchini Nigeria, ambayo ni mojawapo ya nchi kumi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani. Kwa sababu ya uporaji wa makampuni ya kimataifa ya Magharibi, asilimia 40 ya wakaazi wa Nigeria wanaishi katika umaskini wa kutisha. Kuisalimisha Reko Diq kunaweka wazi kwamba watawala wa Pakistan wanafanywa watumwa wa mfumo wa kiulimwengu wa Amerika, huku wakitutarajia sisi kusherehekea utumwa huo. Njia pekee ya kusonga mbele kwetu ni kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itahakikisha matumizi ya rasilimali zenye thamani za Ummah kwa manufaa ya Waislamu na Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu