Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  9 Rajab 1445 Na: 1445 / 29
M.  Jumapili, 21 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Badala ya Kunyesheza Makombora jijini Tel Aviv kwa ajili ya Ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Majeshi ya Waislamu Yanarushiana Makombora katika Maeneo Yao Wenyewe katika kwa Sababu ya Upotofu fikra ya Dola ya Kitaifa

(Imetafsiriwa)

Baada ya mashambulizi ya droni na makombora ya Iran katika wilaya ya Panjgur ya Pakistan, Pakistan pia ilifanya mashambulizi katika eneo la Sistan nchini Iran. Mashambulizi ya kujibizana yanathibitisha kwamba upotofu wa fikra ya dola ya kitaifa ndiyo sababu halisi ya mgawanyiko, na kusababisha udhaifu wa nguvu za Waislamu. Kwa hivyo, Iran iliipiga Syria, Iraq na Pakistan baada ya kuuawa shahidi Waislamu katika mji wa Kirman wa Iran, na kisha Pakistan ikaipiga Iran. Hata hivyo, mauaji ya kishahidi ya Waislamu 24,000 huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan haitoshi kuwakusanya wanajeshi waumini wa Iran na Pakistan ili kukomboa Ardhi Iliyobarikiwa na Msikiti wa Al-Aqsa. Hakika ni upotofu kuyapa thamani zaidi maeneo ya dola ya kitaifa, kwa misingi ya utaifa, kuliko matukufu ya Uislamu, kwa msingi wa amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw).

Masaa machache baada ya kuuawa kwa watoto wa Sabz Koh, na Panjgur, katika jimbo la Balochistan, Pakistan ilimfukuza balozi wa Iran. Majeshi ya Pakistan yaliwekwa katika hali ya tahadhari na kuhamasishwa kwa ajili ya operesheni ya "Marg Bar Sarmachar" (Kifo kwa Waasi). Hapo awali, mnamo Februari 2019, kwa kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Dola ya Kibaniani huko Balakot, majeshi ya Pakistan yalikusanywa ndani ya masaa machache, na kujibu kwa jibu la nguvu, lenye kuvunja taya. Hata hivyo, Mayahudi wa Kizayuni wameiangamiza Gaza, huku wakifanya uhalifu ambao hata wanyama porini wangeweza kuukwepa. Hata hivyo, siku 100 zimepita na uongozi wa kijeshi haujajibu kilio cha Waislamu wa Gaza, kwa operesheni ya "Kifo kwa Uvamizi wa Kizayuni". Hakuna afueni kwa Waislamu bila ya kuzika uovu huu wa dola ya kitaifa. Fikra ya dola ya kitaifa itazikwa tu kupitia kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.

Mashambulizi hayo yamethibitisha kwamba maombi kuhusu kudhoofisha uchumi, “matatizo tata ya usalama wa ndani na ya kisiasa” ya Pakistan na hofu ya vikwazo vya kimataifa ni visingizio tu vya kusikitisha. Kuchafuliwa kwa sanamu la dola ya kitaifa hakukubaliki, isipokuwa wakati bwana Marekani anapokiuka mistari mekundu ya dola ya kitaifa. Washington yenyewe ni kibla cha usalama cha uongozi wetu wa kisiasa na kijeshi. Walakini, nje ya unajisi wa sanamu hili, hakuna risasi inayofyatuliwa, wala uhusiano wa kidiplomasia unaokatwa kwa kumfukuza balozi. Hakuna kinachofanyika endapo Kitabu kilichoteremshwa cha Mola Mlezi wa Ulimwengu, Quran Tukufu, kitachomwa moto, au kuwepo jaribio la kuvunja utakatifu wa Mtume wetu kipenzi cha Mwenyezi Mungu (saw), au ikiwa Waislamu watauawa shahidi katika mji baada ya mji, kwa miezi, au hata miaka.

Vile vile, mashambulizi hayo ya makombora pia yamethibitisha kwamba nguvu zetu za kijeshi, uwezo wetu wa kijeshi na utayari wa vikosi vyetu uko imara. Umma wa Kiislamu una uwezo kamili wa kukabiliana na adui yeyote halisi, awe ni umbile la Mayahudi, Dola ya Kibaniani au Marekani. Tatizo letu halisi ni nusra kamili ya uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Waislamu ambao umepanuka hadi kwenye mfumo fisadi na wa kidhalimu wa kilimwengu wa Kimagharibi. Uongozi wa Waislamu uko tayari tu kuchukua hatua ambazo mfumo wa kilimwengu unaoongozwa na Marekani unaruhusu. Kwa hivyo, bila ya kupindua uongozi huu, kamwe hatuwezi kulinda matukufu ya Uislamu na Waislamu, na kamwe hatuwezi kupata uhuru wa kweli.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Sifa yenu imechafuliwa machoni pa Waislamu. Kulia kama wanawake majumbani mwao kwa matukio ya uchungu ya Gaza, kumedhoofisha msimamo wenu machoni pa adui zenu. Umma wa Kiislamu, wakiwemo Waislamu wa Pakistan, wana kila haki ya kukuulizeni, “uko wapi ushujaa wenu, heshima na roho ya Kiislamu?” Mwenyezi Mungu (swt) wala waumini hawakubali udhuru wenu kwamba “hatukupokea amri.” Msiruhusu utiifu wenu kwa vibaraka wasaliti wa Marekani ukuongozeni kwenye kuteketezwa katika moto wa Jahannam pamoja nao. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ]

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.” [Surah Al-Fath 48:29]. Hata hivyo, uongozi wa Waislamu kwa makafiri ni laini kama hariri, lakini huzungumza na Waislamu kwa lugha ya moto na baruti. Uislamu unawajibisha kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kimabavu, kwa hivyo waondoeni wasaliti wanaosimama katika njia yenu.

Uislamu unawajibisha kuwaondoa watawala ambao ni watumwa wa maadui. Unawajibisha kusimamisha uongozi wa Kiislamu wa ikhlasi unaotutawala kwa yale yote aliyoteremsha Allah (swt). Kwa hivyo, toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir, chini ya Amiri wake, mwanachuoni mkubwa na mtawala, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Hapo pekee ndipo mutakapokuwa na uongozi unaokuhamasisheni kwa ajili ya ushindi au shahada, mpaka mufungue milango ya Msikiti wa Al-Aqsa uliokombolewa kwa mikono yenu wenyewe, huku mukipaza Takbira kwa sauti kubwa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [Surah Ar-Rum 30:4].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu