Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Ramadan 1445 Na: 1445 / 41
M.  Jumapili, 31 Machi 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni juu ya Majeshi ya Waislamu Kuwang'oa Watawala,

Kusimamisha tena Khilafah Rashida na Kwenda Kuinusuru Gaza

(Imetafsiriwa)

Ni juu ya majeshi ya Waislamu kukusanyika kwenda kuinusuru Gaza, ili wawe sako kwa bako na Umma wa Kiislamu katika kuinusuru Gaza. Mtume kipenzi wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ كَرَجُلٍ وَاحِدٍ إِنْ اشْتَكَى عَيْنُهُ اشْتَكَى كُلُّهُ» “Waislamu ni kama mtu mmoja, jicho lake likiwa na maumivu, mwili wote unapata maumivu.”

[Waislamu]. Hakika Waislamu wamejitahidi kwa kadri wawezavyo kwa njia yoyote inayopatikana kwao, licha ya kukumbana na matatizo mengi wenyewe. Waislamu wamesusia vikali makampuni ambayo yanahusika na umbile la Kiyahudi, na kuwasababishia hasara ya mabilioni ya dolari. Vijana wake wamekataa fursa ya kazi zinazolipwa vizuri na kampuni kama hizo, licha ya ukosefu mkubwa wa ajira. Waislamu wamefanya kazi kwa bidii katika kuhamasisha, kuhusu mateso ya Waislamu wa Gaza, katika kukabiliana na vikwazo vya mitandao ya kijamii. Waislamu wamekusanya kiasi kikubwa cha fedha kuwasaidia Waislamu wa Gaza, kwa njia yoyote wanayoweza, licha ya umaskini mbaya unaowakabili. Katika Ulimwengu mzima wa Kiislamu, Waislamu wanaandamana dhidi ya watawala wa Waislamu, wakipinga dhulma zao, vitisho, majambazi na mabomu ya machozi. Basi je, si juu ya majeshi ya Waislamu kuwa upande wa Waislamu katika kuinusuru Gaza?

Ni juu ya majeshi ya Waislamu kuwang'oa watawala wahalifu wa Waislamu, ambao wameegemea upande umbile la Kiyahudi. Watawala wa Waislamu wamepuuza kwa jinai wajibu wao wa kuinusuru Gaza, ingawa kwa pamoja wanaongoza zaidi ya wanajeshi milioni tatu wa Kiislamu. Baya zaidi, watawala hawaachi juhudi yoyote katika kulipa uhai wa umbile la Kiyahudi, iwe wako karibu na Gaza, au mbali. Ama watawala wa Kiarabu, wanawapa Mayahudi mafuta kwa ajili ya vifaru na ndege zake za kivita, huku wakiwarushia mabomu ya machozi Waislamu wanaopinga khiyana zao. Ama mtawala wa Waturuki, anaendelea kufanya biashara na adui wa Kizayuni, akituma meli na vifaa muhimu. Ama watawala wa Pakistan, wanazuia jeshi la Waislamu lenye nguvu zaidi ulimwenguni kutokomeza umbile la Kiyahudi, huku wakipigia debe "suluhisho la dola mbili" la Marekani, ambalo linasalimisha sehemu kubwa ya Palestina kwa ukaliaji kimabavu wa Mayahudi. Mnamo tarehe 23 Novemba 2023, kulingana na mrengo wa vyombo vya habari vya jeshi, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari PR-196/2023-ISPR, uongozi wa kijeshi, "ulisisitiza msimamo wa Pakistan wa kuunga mkono suluhisho la dola mbili." Basi je, sio juu ya majeshi ya Waislamu kuwang'oa watawala hawa walio katika kilele cha uhalifu wao?

Ni juu ya majeshi ya Waislamu kusimamisha tena Khilafah, ambayo ni ngao ya Waislamu huko Gaza na nje ya Gaza. Mtume wetu kipenzi cha Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao". Waislamu wanapigana kwa nyuma yake na wanajihami kwaye.” [Bukhari]. Ilikuwa ni Khilafah Rashida ya Umar al-Farooq (ra) ndiyo iliyoifungua Palestina kwa Uislamu. Ilikuwa ni Khilafah iliyomtuma Salahudin kuikomboa Palestina kutokana na uvamizi. Ilikuwa ni Khilafah ya Abdul-Hamiid II iliyokataa majaribio ya Wazayuni mnamo tarehe 18 Mei 1901 kununua ardhi nchini Palestina, huku akisema, “Siwezi kutoa hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina, kwa kuwa si mali yangu, bali ni mali ya Umma wa Kiislamu. Watu wangu walipigania nchi hii na kuinywesha kwa damu yao.” Sasa, Ummah hauna ngao ya Khilafah. Badala yake, una watawala ambao ni ngao kwa maadui wa Waislamu, na panga dhidi ya Waislamu. Basi je, si juu ya majeshi ya Waislamu, kutoa Nusrah yao (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida?

Enyi Waislamu wa Pakistan! Ramadhan hii, lazima tuyatake majeshi yetu yasimamishe tena Khilafah na kusonga kuelekea Gaza. Ni lazima tumkumbushe kila afisa wa jeshi kwamba tunajua thawabu kubwa inayomngoja mpiganaji anayetoa nusra yake ya kimada kwa ajili ya kusimamisha tena utawala wa Uislamu. Lazima tuwakumbushe kuhusu Sa’ad ibn Muadh (ra), ambaye alitoa Nusrah yake kwa Mtume (saw) ili kupata utawala wa Uislamu katika al-Madinah al-Munawwarah. Ni lazima tuwakumbushe kuhusu Janazah ya Sa’ad. Mtume (saw) alieleza wepesi wa mwili wa Sa’ad kwenye Janaza yake.

«ما يمنعه أن يخفَّ وقد هبط من الملائكة كذا وكذا لم يهبطوا قط قبل يومه قد حملوا معكم»

“Hakuna kilichoufanya mwili wake kuwa mwepesi, isipokuwa waliteremka miongoni mwa malaika idadi kadha na kadha idadi ambayo kamwe haijawahi kuteremka, waliokuwa wamembeba pamoja nanyi.” [Imesimuliwa katika Tabaqat, na ibn Sa’ad]. Ni lazima tuwakumbushe bishara njema ambazo Mtume (saw) alimpa mamake Sa’ad aliyekuwa na huzuni,

«ليرقأ (لينقطع) دمعك، ويذهب حزنك، فإن ابنك أول من ضحك الله له واهتز له العرش»

“Machozi yako yatakwisha, na huzuni yako itaondoka. Ukijua kwamba hakika mtoto wako ndiye wa kwanza Mwenyezi Mungu kutabasamu kwa ajili yake na Kiti cha Enzi (‘Arsh) kutikisika kwa ajili yake.” [Imesimuliwa katika at-Tabarani]

Enyi Waislamu katika Jeshi! Je, kuna utumishi mkubwa zaidi wa kijeshi kuliko ule wa Saad ibn Muadh (ra)? Alitoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha hukmu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Alikuwa mshindi juu ya maadui. Malaika waliteremshwa kuubeba mwili wake kwenye Janazah yake. Mwenyezi Mungu (swt) alitabasamu na Arshi yake ikatikisika baada ya kuipokea roho yake. Yakumbatieni maneno ya Sa'ad bin Mu'adh (ra) katika Vita vya Badr, pale alipomwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa maneno ya wazi na ya uthabiti, , "فوالذي بعثك، لو استعرضت بنا هذا البحر فخضته لخضناه معك، وما تخلَّف منا رجل واحد، وما نكره أن تلقى بنا عدونا غداً. إنا لصبر في الحرب، صدق في اللقاء. لعل الله يريك منا ما تَقَرُّ به عينك، فسر بنا على بركة الله" "Naapa kwa yule Aliyekutuma, ikiwa utatwambia sisi kuvuka bahari hii na wewe kutumbukia ndani yake, tutatumbukia ndani yake pamoja nawe. Hakuna mwanaume ambaye angebaki nyuma. Hatupendi wazo la kukutana na adui yetu kesho. Tuna uzoefu wa vita, tunaweza kupigana. Huenda Mwenyezi Mungu akakuonyesha kitu kitakachokufurahisha, basi tuchukue pamoja na baraka za Mwenyezi Mungu.” Ifufueni ari ya Badr ndani ya nafsi zenu na muhamasike.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu