Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  28 Ramadan 1445 Na: 1445 / 42
M.  Jumapili, 07 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu wa Pakistan na Jeshi Lao! Hakikisheni Waislamu wa Gaza Wanasherehekea Idd kama Tunavyosherehekea Sisi kwa Kutuma Askari Wenu Utashi na Uwezo

(Imetafsiriwa)


Hata kama Waislamu wa Pakistan wanajiandaa kwa ajili ya furaha ya Idd, akili zao zinazunguka mara kwa mara kwa ajili ya masaibu ya Waislamu wa Gaza. Ama watawala wa Pakistan, walijaribu kupunguza hasira iliyoenea kwa kukataa kwao kwa kuendelea kutuma jeshi la Pakistan kuinusuru Gaza. Kwa hivyo, mnamo 4 Aprili 2024, siku tatu kamili baada ya mauaji ya kutisha ya Hospitali ya Al-Shifa kufichuliwa wazi machoni mwa ulimwengu, Waziri Mkuu alikutana na Balozi wa Palestina. Walakini, hakukutana naye kutangaza habari njema ya kutuma makombora, vifaru na ndege za wapiganaji kulishinda umbile la Kiyahudi. Badala yake, kile alichotangaza kiliongeza chumvi kwenye majeraha ya Waislamu wa Gaza, huku wakikandamizwa na kusagwa na mabuldoza ya jeshi, wakizingirwa na kufa njaa. Mrengo wa vyombo vya habari vya serikali ulisema kwamba Waziri Mkuu, “alimhakikishia Balozi wa Palestina kwamba Pakistan itaendelea kutoa sauti yake katika kila mkutano wa kimataifa kwa mshikamano na watu wa Palestina. Pakistan hadi sasa, imetuma vipeto saba vya bidhaa za misaada kwa watu wa Gaza. vipeto vingine vimepangwa mara tu baada ya Idd.” Kwa hivyo, watawala wa Pakistan wanaendelea katika dhambi lao la mapuuza.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Udhaifu mkuu wa Ummah ni kutokuwepo kwa uongozi wa kisiasa kwa msingi wa Uislamu, kwani sio upungufu katika kitu chengine chochote. Mwenyezi Mungu (swt) ameupa Ummah wa Kiislamu zaidi ya askari wa kijeshi milioni tatu, ambao hubeba hamu ya kufa shahidi na ushindi. Mwenyezi Mungu (swt) amewapa Waislamu sehemu kubwa ya rasilimali asili ya ulimwengu. Kinachoharibu baraka hizi zote ni watawala ambao wako katika udhalilishaji, udanganyifu dhidi ya Waislamu na vibaraka kwa maadui zetu. Kutokuwepo kwa Khilafah, tangu 1924, karne kamili iliyopita, ndio udhaifu mkuu wa Ummah wa Kiislamu. Pasi kwayo ni kama watoto yatima bila mlezi wa kinga, aliyechinjwa na maadui zetu kwa mtazamo kamili wa ulimwengu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ فَإِنْ أَمَرَ بِتَقْوَى اللَّهِ وَعَدَلَ فَإِنَّ لَهُ بِذَلِكَ أَجْرًا وَإِنْ قالَ بغَيرِه فَإِن عَلَيْهِ مِنْهُ» “Hakika ima ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye. Ikiwa ataamrisha kumcha Mwenyezi Mungu, na akafanya uadilifu, kutakuwa na thawabu kwake. Ikiwa ataamua vyenginevyo, atahesabiwa dhidi yake.” [Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim]

Enyi Waislamu wa vikosi vya jeshi la Pakistan!

Kuweni upande wa Ummah dhidi ya watawala wasaliti ili kulinda Dini yenu na Akhera yenu. Dori yenu sio kulinda mipaka ya kitaifa, kwa msingi wa utaifa. Jukumu lenu ni kuwalinda Waislamu na kuinua neno la Mwenyezi Mungu (swt) kuwa juu zaidi ulimwenguni. Kutoka kwa Ali bin Abi Talib, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja naye, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  (saw), amesema: «الْمُسْلِمُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ وَيَسْعَى بِذِمَّتِهِمْ أَدْنَاهُمْ وَيَرُدُّ عَلَيْهِمْ أَقْصَاهُمْ وَهُمْ يَدٌ عَلَى مَنْ سِوَاهُمْ» “Maisha ya Waislamu wote ni sawa. Wa chini wao zaidi wanaweza kuhakikisha ulinzi wao. Wa mbali wao zaidi wanaweza kuwazuia wengine kuvunja ulinzi waliopeana. Ni kundi moja dhidi ya wengine wote.” Kwa hivyo musiseme, 'Kwa nini tunapaswa kuingia vitani kwa watu wa Gaza?' Au, 'hatuwezi kuhimili matokeo ya vita! Jukumu lenu ni moja na damu yenu ni moja dhidi ya wale wanakalia hata shubiri moja ya ardhi ya Waislamu, popote pale. Hii ndio Dini ya Muhammad al-Mustafa (saw). Hii ndio Dini ambayo majeshi ya Salahudin na Muhammad bin Qassim waliandamana, juu ya masafa makubwa kutafuta shahada na ushindi.

Enyi Waislamu wa vikosi vya jeshi la Pakistan! Mwenyezi Mungu (swt) amekuandalieni jukwaa la nyinyi kusonga. Watawala wa Waislamu wote wameshafichuka katika kesi ya Gaza. Kwa hivyo, Waislamu hawatatoa machozi mkiwaondoa mamlakani. Ummah wa Kiislamu kutoka Tunisia hadi Pakistan sasa hujaza mabarabara, wakitaka uhamasishaji wa majeshi. Kwa hivyo, Waislamu watasherehekea kote ulimwenguni, pindi mtakapohamasika chini ya Khalifa Rashid. Malizeni utawala wa ukandamizaji na mutoe nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida. Bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) haitacheleweshwa, Mwenyezi Mungu akipenda, kwa kutimiza yale Ahmad aliyoyaripoti kutoka kwa hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye alisema, «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Mtegemeeni Mwenyezi Mungu (swt) na mutimize wajibu wenu, kwa baraka ya Mwenyezi Mungu (swt), ndugu wapendwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu