Jumamosi, 18 Rajab 1446 | 2025/01/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  29 Jumada I 1446 Na: 1446 / 18
M.  Jumapili, 01 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ghasia za Hivi Karibuni za Kisiasa ni Mapambano ya Madaraka Kati ya Makundi ya Kisiasa yanayoshindana juu ya Kiti Utawala cha Udhalilifu, Khiyana na Ubaraka kwa Amerika

(Imetafsiriwa)

Maandamano ya hivi majuzi yaliyoitwa “Wito wa Mwisho”, yalianza mnamo tarehe 24 Novemba 2024 na kuhitimishwa katika uwanja wa D-Chowk jijini Islamabad mnamo Novemba 27. Mbali na kufungwa kwa barabara, shule na mitandao ya intaneti, karibu makumi ya watu, vikiwemo vyombo vya utekelezaji sheria na raia, waliuawa na makumi kadhaa kujeruhiwa. Hata hivyo, vyovyote itakavyokuwa kwa matokeo ya ghasia hizo kali, masaibu ya watu wa Pakistan yatabaki yale yale. Machafuko haya ya kisiasa ni mapambano ya madaraka kati ya vikundi tofauti  vibaraka wa Amerika. Mabadiliko ya kweli kwa watu yatakuja pale tu majeshi yatakapotoa Nusrah yao kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida.

Makundi mbalimbali ya kisiasa katika mfumo wa sasa yana msimamo sawia katika masuala yote makuu. Masuala makubwa yanaelekezwa na uongozi wa kijeshi ambao ni kibaraka wa Amerika. Hii ni pamoja na kulizika suala la Kashmir kwa kuomba maazimio ya Umoja wa Mataifa yatekelezwe, kujisalimisha kwa usawazishaji mahusiano na India kwa kuongeza ushirikiano ambao haujatangazwa na India, kukataa kupeleka vikosi vya jeshi kuinusuru Gaza, kuitia shinikizo serikali ya Taliban nchini Afghanistan kupitia mapigano ya mpakani, uharibifu wa uchumi kwa kutekeleza masharti ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, kukandamiza Da’wah ya Uislamu ili kuhakikisha utawala wa maadili ya kiliberali ya Magharibi katika mfumo wa kijamii na mfumo wa mahakama wa Kiingereza, muungano na adui mkubwa wa Waislamu, Marekani, na kupuuza mateso ya kikatili ya Waislamu wa Xinjiang (Turkestan Mashariki) kwa badali ya mikopo ya China.

Ruwaza, ajenda na manifesto ni sawa kwa vibaraka wote wa Amerika, isipokuwa tofauti chache za juu juu. Kwa hivyo machafuko ya kisiasa si chochote bali ni mapambano ya madaraka. Je, masaibu yetu hayatokani na ajenda na ruwaza zisizo sahihi? Kwa hiyo, ni wazi kwamba machafuko haya ya kisiasa hayataleta tofauti yoyote kwa wananchi, mbali na kukandamizwa katika vita vya vipote hivyo vya kisiasa! Maandamano haya yamethibitisha kuwa mabadiliko ya kina hayawezi kuletwa kwa msaada wa umma. Mabadiliko yanahitaji msaada kutoka kwa jeshi pia. Pia imethibitisha kuwa wananchi wanapinga mfumo wa sasa na wanataka mabadiliko. Sababu muhimu zaidi ya mabadiliko ya kina inabakia. Ni kuwashawishi maafisa wenye ikhlasi katika jeshi la Pakistan kutoa Nusrah yao kwa ajili ya kusimamishwa kwa Khilafah Rashida.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Mwenyezi Mungu (swt) amekupeni uwezo mkubwa wa kijeshi wa Umma wa Kiislamu, kwa hiyo musisaliti amana yenu.  Hali itakuwaje, wakati mutasonga kuondoa uongozi kibaraka, kumaliza machafuko ya kisiasa na uwakala kwa Amerika. Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah itasitisha makubaliano yote na wakoloni, na kukomesha utawala na ushawishi wao juu ya ardhi zetu. Khilafah itafunga kambi zao, balozi zao na kung'oa mipango yao yote ya kikoloni. Khilafah itakuhamasisheni kwa ajili ya ukombozi wa Gaza na Kashmir. Khilafah itaunganisha Waislamu shupavu na walio tayari wa Asia ya Kati, Ghuba na nchi nyingine za Kiislamu pamoja na Khilafah, na kumaliza udhalilifu mikononi mwa watawala wasaliti wa Waislamu. Shikamaneni na Uislamu, muimarishe azma yenu, musimwogope yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt), fanyeni Tawwakul kwa Mwenyezi Mungu (swt) na songeni kwa ajili ya Radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Surah Al-Ra'd 13:11].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu