Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 22 Jumada II 1446 | Na: 1446 / 23 |
M. Jumanne, 24 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Amerika ni Adui Yenu Dhahiri. Majaribio ya Kuidekeza ni Batili. Ni kwa Kusimamisha Khilafah Rashida Pekee, ndio Mnaweza Kuzima Faida ya Kimkakati ya Amerika na Kuipa Jibu Lililofaa!
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 21 Disemba, 2024, Afisi ya Mambo ya Nje ya Pakistan “ilipinga vikali ukosoaji wa Marekani wa mpango wa makombora wa masafa marefu wa Pakistan, na kuuita usio na mantiki na usio na muktadha wa kihistoria kwani iliapa kuendelea kukuza uwezo wake wa makombora sambamba na kiwango cha chini uzuiaji wake wa kuaminika wa kimkakati, ikisisitiza hitaji lao la kukabiliana na vitisho vinavyoibuka kutoka India. (Chanzo: Dawn). Mnamo tarehe 18 Disemba, Marekani iliweka vikwazo kwa mashirika manne ya Pakistan, ikiwemo kampuni ya kutengeneza makombora inayomilikiwa na serikali ya Pakistan. Hii ni mara ya nne tangu Oktoba ambapo Marekani imeweka vikwazo kwa vyombo vinavyohusishwa na mpango wa makombora wa Pakistan. Vikwazo hivi ni licha ya ukweli kwamba, kwa mujibu wa msemaji wa Afisi ya Mambo ya Nje, “Tangu mwaka 2012 wakati maafisa wa Marekani walipoanza kuzungumzia suala hilo, serikali tofauti za Pakistan, uongozi na maafisa, wamejitahidi mara kwa mara kushughulikia vyema na kuondoa wasiwasi wa Marekani usio na mashiko.” Hii ni licha ya ukweli kwamba Marekani yenyewe inashiriki kikamilifu katika kuipatia Dola ya Kibaniani silaha za kila aina, ili liweze kuwa polisi wa eneo, na kupamba moto dhidi ya nchi nyingine za Waislamu!
Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan hauna mkanganyiko kwamba juhudi hizi za Amerika ni kurudisha nyuma mipango ya nyuklia na makombora ya Pakistan. Hata hivyo, uongozi wa kibaraka bado unajishughulisha mara kwa mara na majaribio tasa ya kuidekeza Washington. Je, Amerika haikuondoa makombora ya Scud ya Iraq na silaha za kemikali kabla ya kuiangamiza kabisa Iraq? Je, Amerika haikuruhusu umbile la Kiyahudi kulenga silaha za kemikali za Syria, ndege za kivita na maghala ya makombora, zisije zikaangukia mikononi mwa wanamapinduzi wanyoofu? Je, Marekani haijafanya ‘mipango ya dharura’ kwa silaha za nyuklia za Pakistan na silaha nyingine za kimkakati? Wakati Marekani inatumia mbinu mbalimbali za kijeshi, kidiplomasia, kiuchumi na kiuthaqafa ili kumaliza nguvu za Waislamu moja baada ya nyingine, basi kwa nini uongozi wa Pakistan unadumisha ushirikiano wa kimkakati na adui Amerika!
Kupitia mfumo wake wa kilimwengu, Amerika inawapa watawala vibaraka kisingizio cha “kulazimishwa kuifuata” Amerika. Hii ni ili waweze kurefusha muda wa nguvu zao, licha ya kutekeleza mipango ya kimkakati yenye madhara. Uhalisia wa “mchezo wa undumakuwili” wa uongozi wetu ni kwamba “mchezo huu wa undumakuwili” unachezwa dhidi ya maafisa wa wenye ikhlasi wa kijeshi na watunga sera wa Pakistan. Watawala wanatumia nguvu zetu za kijeshi dhidi ya maslahi yetu wenyewe. Watawala walivunja mikono yetu nchini Afghanistan chini ya amri ya Amerika. Sasa wanatimiza agizo la Amerika la kuiweka serikali ya Taliban katika udhibiti. Baada ya kuiweka Kashmir mikononi mwa Modi, watawala walimpa zawadi ya kusitisha mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti kwa sababu ya maagizo ya Amerika. Hakika, maagizo ya Marekani yanawadhuru Waislamu kote ulimwenguni. Kwa kisingizio kile kile cha “kubanwa na mfumo wa kilimwengu,” Erdogan awali alitazama mauaji ya makumi ya maelfu ya Waislamu mjini Gaza. Sasa, baada ya Bashar, Erdogan anajenga usanifu wa mtego mpya wa Marekani nchini Syria. Licha ya kumiliki teknolojia za hali ya juu zaidi duniani na majeshi yenye nguvu, chini ya mfumo wa sasa wa kilimwengu, viongozi vibaraka wa Waislamu wanayatumia kama vikosi vya mamluki kwa Marekani. Je, hili haliko bayana kwamba Waislamu sasa hawana budi ila kusimamisha Khilafah Rashida.
Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume itageuza mfumo wa kivita kwa kuondoa manufaa ya kimkakati ambayo Marekani inafurahia chini ya mfumo wa sasa wa kilimwengu wa Marekani. Khilafah Rashida itawapindua watawala vibaraka wa Waislamu, ambao viti vyao vya enzi tayari vinatikisika chini ya ghadhabu ya Ummah, kwa muda mfupi iwezekanavyo. Khilafah Rashidah itaziunganisha ardhi za Waislamu kuwa dola moja yenye nguvu, ambayo makafiri wataogopa hata kuota kupigana nayo. Mfumo mpya wa dunia wa Khilafah utaikataa dolari ya Marekani kama sarafu ya kawaida ya kimataifa na kukomesha ubabe wa dolari inayodhoofika, na kusababisha Marekani kukumbwa na mfumko mbaya zaidi wa bei na mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi kuwahi kutokea. Mfumo mpya wa ulimwengu wa Khilafah utamaliza utawala wa Marekani juu ya njia za baharini za dunia na kulidhalilisha jeshi la wanamaji la Marekani.
Kusimamishwa kwa Khilafah kutakuwa ni tangazo la mwisho wa umbile la Kiyahudi, ambalo halijawahi kupigana na jeshi la dola chini ya uongozi wa kweli. Vikosi vya kijeshi vya Waislamu, vilivyoungana chini ya Khalifa vitaweza kuliangamiza umbile hili, wakati Mayahudi hawa watakapokuwa na hofu ya mawe na miti. Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani tayari anatangaza uwezekano wa makombora ya Pakistan kufika Amerika. Huu ndio uwezo wenu halisi Enyi watu wenye nguvu, ambao uongozi wenu kibaraka unaukana kwenu. Kwa hivyo enyi watu wenye nguvu! Je, ni kitu gani kinakuzuieni kutoka kwenye njia hii ya heshima, ilhali Hizb ut Tahrir inakuiteni kwenye faradhi kubwa ya Sharia? Chaguo la Khilafah si mpango badali. Ndiyo njia pekee ya Shariah ya utekelezaji wa amri za Mola Mlezi wa Ulimwengu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surah As-Saff: 9]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |