Jumatano, 08 Jumada al-awwal 1447 | 2025/10/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  3 Jumada I 1447 Na: 11 / 1447
M.  Jumamosi, 25 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Asim Munir jijini Cairo ni Hatua ya Kutekeleza Ruwaza ya Trump kwa Mashariki ya Kati

(Imetafsiriwa)

Katika utekelezaji wa ruwaza ya Trump kwa Mashariki ya Kati, ambayo inatazamia kupandishwa cheo kwa umbile la Kiyahudi ndani ya ulimwengu wa Kiislamu baada ya usawazishwaji mahusiano, na kujumuishwa kwa serikali zote zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu ndani ya kile kinachoitwa ruwaza ya Mikataba ya Abraham, uhusiano wa hivi karibuni kati ya vibaraka wa Amerika katika ulimwengu wa Kiislamu umefanyika, kwa lengo la kutimiza ndoto za Trump katika eneo hilo. Katika muktadha huu, Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, ambaye Trump alimtaja kama “dikteta anayempenda,” alimpokea Field Marshal Asim Munir, ambaye Trump alimtaja kama “field marshal anayempenda” na ambaye utawala wake ulimteua Trump, muuwaji wa Gaza, kwa Tuzo la Amani la Nobel, katika Jumba la Al-Ittihadiya huko Mashariki mwa Cairo. Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Misri. Pande hizo mbili zilidai kujadili ushirikiano wa pamoja na uimarishaji wa usalama wa kikanda, huku balozi wa Pakistan jijini Cairo pia akiwepo.

Asim Munir pia alikutana na Luteni Jenerali Abdel Meguid Saqr, Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Jeshi na Waziri wa Ulinzi na Uzalishaji wa Kijeshi. Majadiliano yalilenga kuimarisha uhusiano wa kijeshi kati ya vikosi vya jeshi vya Misri na Pakistan, yakisisitiza “ruwaza ya pamoja” ya miundo inayounga mkono amani na usalama wa kimataifa, ingawa imeundwa kulingana na mahitaji ya Mayahudi na Amerika. Jenerali Sisi alielezea shukrani zake kwa kile alichokisifu kama “maendeleo makubwa katika uhusiano wa Misri na Pakistan,” akisisitiza kujitolea kwa utawala wake kuendelea kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ili kutumikia “maslahi ya pamoja,” ikimaanisha maslahi ya mabwana zao katika Ikulu ya White House.

“Maslahi ya pamoja” yaliyojadiliwa yalihusiana na kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kati ya pande hizo mbili, sio kuikomboa Palestina, kusafisha Al-Masjid Al-Aqsa kutokana na uchafu wa Mayahudi, au kulipiza kisasi makumi ya maelfu ya mashahidi waliouawa katika mauaji ya halaiki yaliyoongozwa na Trump mikononi mwa Mayahudi waovu. Hakika, Palestina wala Al-Masjid Al-Aqsa hazikutajwa hata kidogo katika mkutano huo! Ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa unawezaje kujadiliwa, huku Jenerali Sisi akitenda kama mpatanishi kati ya upinzani na Mayahudi, akifungua milango ya hoteli na maeneo ya mapumziko ya Misri kwa wajumbe na marais wanaokubaliana kuhusu kuua na kupokonya silaha upinzani, na kutuma vikosi vya kimataifa kuchukua nafasi ya vikosi vya uvamizi, ili kukamilisha kile mashini ya mauaji ya Kiyahudi ilichoanza, kwa silaha zisizo na kikomo za Marekani na usaidizi wa kisiasa na kiuchumi?! Je, Jeshi la Pakistan limechukua hatua katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwaokoa watu wetu waliokandamizwa mjini Gaza kwamba sasa lichukue hatua kuwasaidia au kuwanusuru watu wa Ardhi Iliyobarikiwa?!

Mazungumzo yao ya kubadilishana utaalamu wa kijeshi si kwa madhumuni ya kuweka Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuikomboa Palestina, bali ni kutimiza ruwaza ya Trump kwa Gaza, akiibadilisha kuwa kimbilio la ufisadi kwake na washirika wake miongoni mwa watawala wa Waarabu na Waislamu. Kwa hivyo, hawakusahau kusisitiza umuhimu wa kuepuka kuongezeka kwa uhasama dhidi ya dola ya Kiyahudi, ambayo waliielezea kwa msemo “kukabiliana na ugaidi na itikadi kali.”

Enyi Wenye Ikhlasi Ndani ya Jeshi la Pakistan na Jeshi la Misri Al-Kinanah! Jueni kwamba mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Palestina yanaendelea kutokana na kutochukua hatua kwenu, na kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ni Shahidi wa majeshi yenye nguvu zaidi yaWaislamu yanayosimama bila kuchukua hatua huku waja Wake wakiuawa, kuchinjwa, kuteswa, kushambuliwa, kudhalilishwa, kufa njaa, na kuhamishwa. Kwa hivyo, tunakuulizeni: Je, ni watoto wangapi zaidi mtawaacha wafe kwa njaa au kulengwa shabaha? Je, ni wanaume wangapi mtawaacha wateswe na kudhalilishwa?

Je, ni wanawake wangapi zaidi mtaviacha vikosi vya Mayahudi viwashambulie? Hivyo jihadharini, enyi askari wa Ummah wa Kiislamu! Mataifa mengi yaliyotangulia yamepotea mikononi mwa viongozi wao wa kidhalimu. Msiwatii wale wanaomuasi Mwenyezi Mungu (swt). Imepokewa katika Musnad Ahmad na Ibn Majah kwa silsila sahihi ya upokezaji kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَنْ أَمَرَكُمْ مِنْهُمْ بِمَعْصِيَةِ اللَّهِ فَلَا تُطِيعُوهُ» “Mwenye kukuamrisheni kumuasi Mwenyezi Mungu miongoni mwao basi musimtii.” Abu Bakr al-Siddiq (ra) pia alitahadharisha dhidi ya kuwafuata watawala waasi, akasema, أطيعوني ما أطعت الله ورسوله، فإن عصيت الله ورسوله فلا طاعة لي عليكم “Ninitiini mimi maadamu namtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake pindi nikimuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake basi musinitii.”

Hii ni licha ya ukweli kwamba Abu Bakr (ra) alikuwa mmoja wa Maswahaba bora (ra)! Kwa hivyo munawezaje kuridhika munapowatii watawala madhalimu wanaotumikia Magharibi, wanaokaidi amri za Mwenyezi Mungu (swt), na hawawezi kamwe kufikia safu za Maswahaba watukufu (ra)? Yatosha udanganyifu, uongo, njama, na usaliti kutoka kwa watawala wa sasa wa Waislamu! Wao ni mzigo kwa Ummah, na lazima muwawajibishe sasa. Ipeni nusrah yenu (msaada wa kijeshi) Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itahamasisha nguvu za kijeshi za Ummah na rasilimali za kiuchumi, kulitokomeza umbile la Kiyahudi, na kumakinisha utawala wa Khilafah katika kanda hii, na kuifanya iwe dola inayoongoza duniani.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Aali Imran:160].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu