Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  1 Rabi' I 1442 Na: BN/S 1442 / 02
M.  Jumatatu, 16 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Kurugenzi ya Wakfu huko Hebron (Al-Khalil) Kusini Imekuwa Chombo cha Usalama Kinachompiga Vita Mwenyezi Mungu na Mtume Wake?!

(Imetafsiriwa)

Jana, Jumapili adhuhuri, Vikosi vya Usalama vya Uzuizi viliwakamata mashababu watano wa Hizb ut-Tahrir kutoka mji wa Dura, kusini mwa Hebron, miongoni mwao ni mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Dkt Musab Abu Arqoub, baada ya swala ya adhuhuri mbele ya Msikiti Mkuu wa Dura. Kwa unyama na jeuri zote, vikosi hivi viliwashambulia mashababu hao katika makao makuu ya Usalama wa Uzuizi, kabla ya wengine kukabidhiwa polisi, na wengine kwa huduma ya ujasusi.

Siku chache zilizopita, vyombo vya usalama vilikusanyika pambizoni mwa Msikiti Mkuu wa Dura, vikiandamana na Nasser Abdul Aziz Dudain, mkuu wa wakfu kusini mwa Hebron, ambaye alitamka maneno mabaya ambayo hayakufaa kwa Muislamu, vipi basi hili linafanywa na mtu ambaye ni msimamizi wa misikiti! Na hakika picha ambayo mkurugenzi wa wakfu na vyombo vya usalama waliidhihirisha ni ya kina cha chuki yao na uadui wao kwa wabebaji ulinganizi na harakati zao endelevu za uharibifu wa nyumba za Mwenyezi Mungu na kuzuia neno la haki kupaazwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu,

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ مَنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَنْ يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَى فِي خَرَابِهَا أُولَئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَنْ يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿

"Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa." [Baqara: 114]

Na hapa tunamuuliza mkuu wa Usalama wa Uzuizi huko Dura, Murad Talib al-Shalaldeh, je wewe ndiye uliyetoa amri ya kuuzingira msikiti na kuwakamata na kuwashambulia mashababu wa Hizb ut-Tahrir, au kuna mtu aliyekuamuru ufanye hivyo? Tunaweza kuuliza juu ya dori ya naibu gavana, Khaled Abdel Aziz Dudain, kaka wa mkurugenzi wa Wakfu za Kusini. Je! Yeye na kaka yake wanaupiga vita Uislamu kila mmoja kwa cheo chake na kwa uratibu kamili? Tunaweza kuuliza dori ya gavana katika yote yaliyotokea, na dori ya Muhammad Shtayyeh, Waziri Mkuu wa Mamlaka na Waziri wa Wakfu ni ipi?! Tunawauliza hawa wote ni kwa maslahi ya nani mnafanya kazi, kutaharaki na kukamata? Misikiti hii ilijengwa kutokana na pesa za Waislamu ili jina la Mwenyezi Mungu litajwe ndani yake, Uislamu utukuzwe ndani yake na haki itangazwe ndani yake, wala haikujengwa kwa ajili ya wanafiki au mamluki ambao hukimbilia kuwafanya vipenzi maadui wa Uislamu!

Kwa kumalizia, tunaiambia mamlaka na vyombo vyake: Nyinyi ni wingu linalopita la majira ya joto linalopita juu ya watu wa Palestina, ama Uislamu na wabebaji ulinganizi wake watabakia kama mti mzuri, ambao shina lake liko imara, na tawi lake liko angani, na kwa yakini mtalipa thamani ya uhalifu wenu, fedheha hapa duniani na adhabu kali kesho Akhera.  

وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ﴿

Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. [Ash-Shu'ara: 227]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Ardhi Iliyobarikiwa Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu