Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 27 Rajab 1446 | Na: BN/S 1446 / 24 |
M. Jumatatu, 27 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nani Anasherehekea Maadhimisho ya Isra na Mi’raj?
(Imetafsiriwa)
Waislamu wanaadhimisha kumbukumbu ya Isra na Mi’raj, kwa kusoma Ayah (aya):
[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ]
“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Surat Al-Isra:1]. Ayah hii na muujiza huu ulianzisha Msikiti wa Al-Aqsa kama sehemu kuu ya Aqidah (itikadi) ya Waislamu.
Umma wa Kiislamu unaadhimisha kumbukumbu hii wakati Msikiti wa Al-Aqsa ukiendelea kuwa mateka mwenye huzuni, amefungwa chini ya mshiko wa viumbe viovu zaidi, inayonajisiwa asubuhi na jioni. Watu wake wamezuiliwa kurukuu na kusujudu ndani ya kuta zake.
Ummah unaadhimisha tukio hili huku viunga vya Al-Aqsa vikitiwa doa kwa damu ya Al-Shuhadaa Al-Mujahedeen (wapiganaji waliouawa shahidi), watoto, wanawake, na wazee. Nyumba zake zimefunikwa na weusi wa uharibifu, kuhama, njaa, na hofu.
Ummah unaadhimisha kumbukumbu hii huku watu wa Gaza wakihesabu zaidi ya mashahidi 60,000 na mamia ya maelfu ya waliojeruhiwa, huku makumi ya maelfu ya nyumba zikiharibiwa, wahanga wa uoga wa Mayahudi.
Ummah unaadhimisha huku wakaazi wa Kambi ya Wakimbizi ya Jenin wakihamishwa kutoka kambi yao, wakiregelea kuhamishwa kwa mababu zao mnamo 1948. Uhamisho huu unaakisi hali mbaya ya watu wa Gaza chini ya mashambulizi ya mabomu, uharibifu, na mauaji, yanayojumuisha maafa ya watu wa Palestina ambao wametelekezwa kwa Mayahudi kwa karibu miaka themanini.
Ummah unaadhimisha kumbukumbu hii huku Trump akitishia kuwafukuza wakaazi waliosalia wa Ukingo wa Magharibi na Gaza hadi Jordan na Misri, na jibu linabaki kuwa ni kulaani na kupinga pendekezo la “nchi mbadala”, badala ya kuchukua hatua kwa ajili ya ukombozi!
Tawala za ulimwengu wa Kiislamu zinatoa wito wa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka huu, licha ya kuwa wametambua uwepo wa umbile linaloinajisi ardhi iliyobarikiwa ya Isra na Mi’raj. Wamesimama kando, wakishuhudia mito ya damu ya Wapalestina ikitiririka, mabomu yaliyosababisha nyumba kuwa vifusi, na uharibifu ulioharibu vitongoji, mazao, na vizazi. Wametazama huku hofu ikiwashika wazee na vijana, huku njaa isiyo kifani ikiwasibu, na huku baridi ikigandisha miguu na nyoyo za watu. Watawala hawa wamejishutumu wenyewe kuwa ni washirika katika mauaji kupitia msaada wao kwa madhalimu, usaliti wao, na kuwazuia wenye uwezo kuwasaidia ndugu zao na kuukomboa utakatifu wa Mtume (saw) kutokana na unajisi ya wale ambao ghadhabu imewashukia juu yao!
Msikiti wa Al-Aqsa, viunga vyake, na watu wake hawataki tu maadhimisho ambayo yanawasha cheche ya jihad katika moyo wa mtu, bali wale wanaoinuka kwenye ukombozi wake. Hawataki mafuta ya kuwasha taa zake wakati imegubikwa na giza la utumwa na nyua zake zimegubikwa na maneno ya kufr (ukafiri).
Msikiti wa Al-Aqsa, viunga vyake, na watu wake hawasubiri duara za ukumbusho kutoka kwa Waislamu.
Wanasubiri vitengo, vikosi, na majeshi ambayo yanamdhukuru Mwenyezi Mungu huku wakiingia humo kama wakombozi, wakiitakasa kama vile Swalah al-Din alivyofanya katika siku mithili ya hizo.
Msikiti wa Al-Aqsa, viunga vyake, na watu wake hawaokolewi kwa machozi, mashairi, ukumbusho, vyakula, au vinywaji. Wanaokolewa tu na wale wanaosoma,
[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى[ “SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja” [Surat Al-Isra:1] ambao wanafuata mfano wa yule aliyechukuliwa na Mwenyezi Mungu katika safari ya usiku huo, na wanaiga wale waliopokea funguo za Ardhi ya Isra, na vile vile wale walioukomboa Msikiti wa Al-Aqsa. Wale tu wanaoita, kutenda, na kusonga kwa ajili ya ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ndio wenye haki ya kusherehekea maadhimisho haya.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa– Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: 0598819100 www.pal-tahrir.info |
E-Mail: info@pal-tahrir.info |