Jumatatu, 21 Dhu al-Qi'dah 1446 | 2025/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  15 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: BN/S 1446 / 35
M.  Jumanne, 13 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mamlaka ya Palestina ilimuua Rami Zahran, Kisha Mzee Mmoja, Ikikamilisha Uhalifu wake Dhidi ya Watu wa Palestina

(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumanne,13/5/2025, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Palestina vilimuua kijana Rami Zahran kutoka kambi ya wakimbizi ya Al-Far'a huko Tubas. Kisha wakafuatilisha hili kwa kumuua mzee mmoja (Abu Khalil al-Saba'neh) kutoka mji wa Jenin. Huu ni mwendelezo wa jinai zake dhidi ya watu wa Palestina, zikiwemo za mauaji, uchomaji moto, ukamataji, uvamizi wa misikiti, na unyang'anyaji mali ya Wapalestina kinyume cha sheria, kula mali zao kwa njia ya dhambi na fujo.

Mamlaka ya Palestina (PA) imekwenda mbali katika uhusiano wake na umbile la Kiyahudi, ikitabanni uongo wake na kuhalalisha mauaji yake na mzingiro wa watu wa Gaza. Hata inashiriki jinai zake dhidi ya watu wa Palestina na inashindana nalo katika uadui wake dhidi yetu. Haishangazi basi kwamba mwongo muovu Anwar Rajab anajitokeza na kudai kwamba walimuua Rami Zahran kwa kujilinda na kwamba yeye ni ishara ya machafuko ya usalama.

Wakati wote huu Mayahudi wanakanyaga hadhi yao na kuyavamia makao yao makuu, kana kwamba wamezoea udhalilifu na wameuchukulia kama rafiki, na wamezoea utumwa kwa adui, hivyo wamewatoa watu wa Palestina kama kafara kwa ajili ya Mayahudi.

Wakati wote huu Utawala wa Palestina unatumai, licha ya kudhalilishwa kwake, kwamba Mayahudi wataacha baadhi ya Ukingo wa Magharibi kwa ajili yake, ambako wanapora mali za watu, na kwamba wataipa mamlaka fulani huko Gaza ili iweze kuwakandamiza watu wa Gaza kama inavyofanya katika Ukingo wa Magharibi.

Mamlaka ya Palestina imekuwa kama Mayahudi katika uadui wake dhidi ya watu wa Palestina. Imekuwa adui wa watu wa Palestina, na kwa kufanya hivyo, imevuka dori ya washiriki. Ni wale tu ambao Mwenyezi Mungu amezizima nyoyo zao ndio wataendelea kufuatilia jinai zake. Iwapo kuna yeyote aliyesalia miongoni mwa vyombo vyake mwenye uzito wa chembe ya wema moyoni mwake, basi na afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kumfikia adhabu itokayo kwake na kufagiliwa mbali.

Tunarudia tena katika hotuba yetu kwa Ummah: Mzigo wa watu wa Palestina uko kwenye shingo za Umma wa bilioni mbili, umewaacha watu wa Palestina kuwa mawindo ya Mayahudi na kisha kwa Mamlaka ya Palestina, ambayo inashindana na Mayahudi katika uadui wake kwa watu wa Palestina. Umma umewaacha watu wa Palestina kama mawindo pale ulipochelewesha ukombozi wa ardhi ya Isra’ na Mi’raj na kutii amri za watawala ambao uovu wao ni sawa na wa PA. Ummah umewaacha watu wa Palestina kama mawindo pale ulipokubali kwamba watawala hao wabaki wamekaa kwenye shingo zake na kuyazuia majeshi yake kuelekea Palestina. Ummah umewaacha watu wa Palestina kama mawindo pale ulipokubali Trump apokewe katika ardhi ya Misikiti Miwili Mitukufu kama mshindi, hali yeye ndiye aliyeruhusu damu yetu kumwagwa na Mayahudi kwa maneno na silaha zake. Ummah umewaacha watu wa Palestina wakati majeshi hayakutoka kwenye kambi zao ili kuitikia wito wa Mola wao.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيّاً وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيراً]

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako [An-Nisa: 75]

Ama Mamlaka ya Palestina imepoteza uhusiano wa kusikia na umepofuka, imekuwa kama wale walioelezwa na Mwenyezi Mungu (swt):

[صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ]

Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. [Al-Baqarah:18]. Lakini haijui kwamba mwisho wa mabwana wake unakuja bila shaka, na siku Umma utakapoliponda ponda umbile hilo, hautakuwa na huruma juu ya wale waliokuwa mkono, mguu, na kiatu chake.

[فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّى حِينٍ * وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ * أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ * فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنْذَرِينَ]

Na waache kwa muda * Na tazama, na wao wataona * Je! Wanaihimiza adhabu yetu? * Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa!” [As-Saffat: 174-7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu