Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  24 Dhu al-Hijjah 1444 Na: HTS 1444 / 45
M.  Jumapili, 16 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yalazimisha Majadiliano kwa Pande Zinazozozana nchini Sudan baada ya Mchanganyiko wake wenye Sumu Kukomaa
(Imetafsiriwa)

Baada ya miezi mitatu ya mauaji, uharibifu, ufurushaji, uporaji wa mali ya umma na ya kibinafsi, na uharibifu wa miundombinu, Marekani imerejea kuzungumza kuhusu majadiliano kati ya pande zinazozozana nchini Sudan. Washirika wake katika eneo hili waliunga mkono sauti yake, na mazungumzo juu ya uzito wa hali ya Sudan yakaanza, kana kwamba vita vimeanza jana tu! Inaonekana kana kwamba mchanganyiko wa sumu wa Marekani umekomaa, kwa hivyo Marekani inashinikiza pande zinazopigana kujadiliana ili kusitishwa. Huyu hapa balozi wake jijini Khartoum akisema kupitia Al- Jazeera Live, "Wito uliotolewa na baadhi ya makundi ya kijeshi wa kukataa usuluhishi wowote wa mzozo uliojadiliwa ni kutowajibika."

Kauli hii ya balozi wa Marekani jijini Khartoum inathibitisha yale tuliyohitimisha tangu kuzuka kwa vita hivi visivyo na maana, kwamba ni matakwa ya Marekani yaliyokusudia kuhujumu muundo wa makubaliano ambao unapeana mamlaka halisi, pindi unapotekelezwa, kwa watu wa Uingereza (raia).

Mpango huo mchafu wa Marekani ulifanikiwa kuwakusanya watu karibu na jeshi baada ya vitendo vya kutisha vilivyofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka dhidi yao. Kwa hivyo, Marekani ilihakikisha uungwaji mkono wa hatua zozote za baadaye zinazoimarisha msimamo wa jeshi. Mazungumzo kuhusu serikali ya kiraia ni udanganyifu tu machoni pa watu wa Sudan wanaoomboleza. Haitakuwa bora kuliko serikali ya Hamdok; itakuwa ni serikali ya mfano ambayo misheni yake pekee ni utekelezaji.

Hivyo basi, tunaona mbio hizi za vibaraka wa Marekani katika eneo hili, kuanzia na Mkutano wa IGAD nchini Ethiopia, ukifuatiwa na mkutano wa kilele wa nchi jirani za Sudan, zikiongozwa na Misri mnamo Alhamisi, 13/7/2023. Mikutano yote miwili ililenga kusitisha mapigano na majadiliano. Pande zinazozozana zilielezea kukaribisha kwao usitishaji huo wa mapigano, na majadiliano ya kivitendo yakaanza kwa kuondoka kwa ujumbe wa jeshi na ujumbe wa Vikosi vya Msaada wa Haraka mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Inasikitisha sana kwamba nchi yetu imekuwa uwanja wa kutekeleza njama za makafiri wa kikoloni kwa gharama ya damu na heshima yetu, na kwamba hii inafanywa na mikono ya baadhi ya watu wetu ambao wameuza Dini yao kwa faida za kidunia za wengine.

Enyi Watu wa Sudan, fanyeni kazi pamoja na wale wanaojitahidi kuregesha maisha yenu kwa Uislamu, jambo ambalo linapatikana kwa kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Inang'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka kwa nchi yetu, inatafuta kulipiza kisasi kutoka kwa vibaraka wake, inalinda matukufu, na kueneza kheri kwa wanadamu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu