Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: HTS 1444 / 44
M.  Alhamisi, 15 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Al-Junaynah Yaungua
Mamia Wauawa na Maelfu Kujeruhiwa, huku Gavana wa Jimbo na Serikali Hawachukui Hatua Yoyote!
(Imetafsiriwa)

Serikali ya jimbo la Darfur inasema kuwa idadi ya waliopoteza maisha katika Al-Junaynah, jimbo la Darfur Magharibi, imezidi elfu moja (Al-Hadath, 14/6/2023). Muungano wa Madaktari wa Sudan unaonya kuwa hali ya Al-Junaynah imekuwa mbaya, mbaya zaidi kuwahi kutokea. Mkuu wa misheni ya UNITAMS aliandika tweet kwenye tovuti ya misheni hiyo, akisema, “…huko El Geneina (Darfur Magharibi)…kuna mtindo unaoibuka wa mashambulizi makali dhidi ya raia kulingana na utambulisho wa makabila yao, yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Kiarabu na baadhi ya watu wenye silaha waliovalia sare za Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF). Ripoti hizi zinatia wasiwasi sana na, zikithibitishwa, zinaweza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu.”

Gavana wa Darfur Magharibi, Khamees Abakar, saa chache kabla ya kuuawa kwake, alisema katika mahojiano na Idhaa ya Al-Hadath mnamo siku ya Jumatano, Juni 14, 2023, kwamba mji wa Al-Junaynah ulikumbwa na uvunjaji kamili sheria wa Vikosi vya Msaada wa Dharura na wanamgambo wenye silaha wanaowaunga mkono. Alikanusha kubainisha hali ya Al-Junaynah kama mzozo wa kikabila kati ya Massalit na makabila ya Waarabu. Alieleza masikitiko yake kwa kutoingiliwa kati na vikosi vya jeshi kulinda watu, kwani walibaki kwenye kituo chao cha 15 cha Kitengo cha Wanajeshi wa Ardhini. Alitaja kuwa watu walilazimika kujihami kwa silaha ili kujilinda wao na familia zao.

Huu ndio uhalisia katika mji wa Al-Junaynah, mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi, na ndio uhalisia wa kusikitisha kwa kila maana ya neno hili. Inathibitisha uzembe wa serikali katika kutekeleza wajibu wake kwa raia wake kwa kuwapatia ulinzi na usalama. Kwa hakika serikali inashiriki katika haya yanayotokea, kama inavyothibitishwa na kauli ya marehemu gavana kwa Idhaa ya Al-Hadath kwamba jeshi halikuingilia kati kuwalinda watu, na kuwaacha kwenye huruma ya wanamgambo. Wala hawla wala quwata illa billah.

Serikali yoyote ambayo itashindwa kutoa usalama kwa raia wake haistahili kubaki madarakani. Wajibu wa kimsingi wa serikali yoyote duniani ni kuhakikisha kuhifadhi maisha ya watu, kulinda utu wao dhidi ya ukiukwaji, na kulinda mali yao dhidi ya kunyonywa. Katika Uislamu, mtawala ni ngao inayoulinda Ummah kutokana na madhara yoyote. Amesema Mtume Muhammad (saw): «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (mtawala) ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.” Tangu kuanguka kwa Dola ya Khilafah na kuibuka kwa tawala za kidhalimu katika ardhi za Kiislamu, damu za Waislamu zimekuwa duni, utu wao unakiukwa, na mali zao zinafujwa na maadui. Huu ndio uhalisia wa kusikitisha ambapo maisha ya Waislamu hayathaminiwi, na haki zao zinapuuzwa.

Hali yetu haitarekebishwa, na Waislamu nchini Sudan au katika nchi nyingine yoyote ya Kiislamu hawatapata usalama, amani, ustawi na utulivu isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hii ni ahadi itokayo kwa Mwenyezi Mungu na bishara njema kutoka kwa Mtume wake «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “...kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu