Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  4 Muharram 1444 Na: 01 / 1444 H
M.  Jumanne, 02 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utawala wa Kihalifu wa Damascus Unaendelea Kuharibu Matukufu ya Waislamu huku Ukimwaga Damu zao
(Imetafsiriwa)

Wanaharakati wa Syria walisambaza kwenye mitandao ya kijamii na vituo vya habari picha zinazoonyesha watu wakifanya matambiko ya kidini ya kiajabu katika Msikiti wa Umayyad jijini Damascus, kama sehemu ya ukiukaji wa utawala wa kihalifu wa Syria dhidi ya watu wa Ash-Sham na matukufu ya kidini yao.

Picha hizo zinaonyesha mtu mmoja aliyevalia nguo za rangi ya machungwa akifanya tambiko la ajabu la kutafakari mithili yoga, pamoja na mwanamke mmoja ambaye ni mfuasi wa mtu huyo pia akiwa amevalia vazi la rangi ya machungwa akiwa amezungukwa na kundi la wanawake wanaoonekana kucheza mbele ya watu hao.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Hapana shaka kwamba matukufu ya Waislamu katika ardhi ya Ash-Sham yamekiukwa, na matukufu yao yanaporwa, hasa chini ya utawala wa baba na mwana, madhalimu wa Ash-Sham. Katika miaka ya nyuma ya mapinduzi, misikiti mingi ilivunjwa, ikiwemo ile ya zama za Umayyad, na misikiti mingi iligeuzwa kwa madhumuni mengine. Wanaharakati wamesambaza (video ya) shambulizi kwenye Msikiti wa Abu Bakr As-Siddiq katika mji wa Aleppo. Pia, zaidi ya Waislamu milioni 1.5 waliuawa, maelfu ya wanawake wa Kiislamu waliojisitiri wakiwa ndani ya vituo vya uzuizini na wengine kubakwa, bila ya kusahau mamia ya maelfu ya wafungwa magerezani, mamilioni ya watu waliokimbia makaazi yao, miji na vijiji iliyoharibiwa, na majumba na mali zilizoporwa.

Yanayotokea katika nchi za Waislamu kwa jumla, na hasa katika ardhi ya Ash-Sham, ya uhalifu na uvamizi dhidi ya matukufu, yanasababishwa na watawala wa maangamizi na kutokuwepo mlinzi kwa Waislamu na imamu, ngao ambaye watu hupigana nyuma yake na hulindwa na yeye, anaye hukusanya majeshi kwa ajili ya mwanamke mmoja, kuhami heshima ya Waislamu na kuhifadhi matukufu yao.

Magharibi Kafiri, wapambe wake, na mawakala wake hawakuthubutu kukiuka matukufu ya Waislamu au kumdhihaki Mtume wao Mtukufu au kuvunja heshima zao, isipokuwa baada ya kuivunja dola yao, wakaitenga Dini yao katika dola na jamii, na wakapandikiza watawala vibaraka juu yao wanaofanya kila aina ya uonevu, ukatili na uhalifu; ili kuhifadhi mifumo ya kikafiri na kuzuia kurudi kwa Uislamu kwenye utawala, na kufikia maslahi ya mabwana zao na kuzikoloni kwao nchi za Waislamu.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, makaazi ya Uislamu: Maisha chini ya mifumo hii ya kiutendaji iliyotungwa na mwanadamu ni maisha ya udhalilifu, utumwa na unyonge, na bila shaka ni maisha ya dhiki ambayo Mola wetu Mlezi (swt) ametueleza juu yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى)

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 124].

Ukimya wenu kuhusu vitendo vya madhalimu na wahalifu hautabadilisha chochote. Bali madhalimu watazidisha dhulma na ukandamizaji, na mutazidisha udhalilifu juu ya udhalilifu, na fedheha juu ya fedheha. Madhalimu wataendelea kurithi udhalimu wao; kila dhalimu anapoangamia, dhalimu mwengine humrithi, na watoto wetu watarithi maisha ya udhalilifu na fedheha kizazi baada ya kizazi.

Ili kupata mabadiliko lazima kuwe na muhanga na uthabiti ikiwa munataka maisha ya heshima na adhama chini ya kivuli cha Uislamu kwenu na watoto wenu baada yenu. Mulianzisha mapinduzi yenye baraka dhidi ya dhalimu wa madhalimu wenye nguvu zaidi wanaojulikana katika historia, na mulijitolea muhanga mkubwa sana; mulikitikisa kiti chake cha enzi na kukaribia kuvunja nguzo zake. Hatuna wa kutunusuru baada ya Mwenyezi Mungu (swt), ila kushikamana na misimamo ya mapinduzi yetu, na kufanya kazi ya kurekebisha njia yake, baada ya walaji njama na wale wafanyao biashara (kwayo) kuyavuruga. Na hili litawezekana tu kupitia kutabanni mradi wa wazi wa kisiasa unaotokana na imani ya Waislamu, na kufuata uongozi wa kisiasa unaofahamu na mkweli utakao yaongoza mapinduzi ya Ash-Sham kwa utambuzi wa kufikia vipimo na malengo yake, ambayo kilele chake ni kupinduliwa kwa utawala wa kihalifu na kusimamisha utawala wa Uislamu juu ya magofu yake, ili tupate utukufu wa dunia hii na Akhera, na kwamba jina lenu liandikwe katika mbingu ya juu zaidi, na mutakumbukwa milele katika historia. Kwa hivyo, tafuteni wokovu wenu na mujenge jengo la utukufu wenu kwa mikono yenu wenyewe, na musisubiri suluhisho kutoka kwa maadui zenu au kutoka kwa walaji njama wadanganyifu wanaoitwa "marafiki", wao ndio adui, kwa hivyo jihadharini nao, na mtegemeeni Mwenyezi Mungu Peke Yake, na shikamaneni na Kamba Yake yenye nguvu, kwani ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu Al-Aziz (Mwenye nguvu) Al-Hakim (Mwenye hekima).

(وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ)

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]

 Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu