Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  8 Muharram 1444 Na: 02 / 1444 H
M.  Jumamosi, 06 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkutano wa Kilele kati ya Erdogan na Putin ni Muendelezo wa Vita dhidi ya Watu wa Ash-Sham na Mapinduzi yao
(Imetafsiriwa)

Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho, Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, walithibitisha mnamo Ijumaa, 5/8/2022, kuamsha mchakato wa kisiasa na mapambano dhidi ya mashirika yote ya kigaidi nchini Syria. Taarifa hiyo ya mwisho ya mkutano huo ilieleza kuwa wakati wa mazungumzo yao kuhusu faili ya Syria, marais hao wawili walionyesha umuhimu mkubwa kuamsha mchakato wa kisiasa. Umuhimu wa kuhifadhi umoja wa kisiasa wa Syria na hadhi ya eneo ilisisitizwa, kulingana na taarifa hiyo.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Mfuatiliaji wa mengi ya matokeo ya mikutano kati ya utawala wa Urusi na utawala wa Uturuki anafahamu vyema kwamba lengo la mikutano yao linazunguka pambizoni mwa makubaliano ya kuhifadhi umoja wa maeneo ya Syria, na kupambana na mashirika yote ya kigaidi. Vitendo vingi vinaangukia chini ya vifungu hivi ambavyo hatimaye vinapelekea kuyabatilisha mapinduzi ya Ash-Sham, upotevu wa muhanga wake mkubwa, na kuregesha uhalali kwa dhalimu wa Ash-Sham; na udhibiti wake juu ya maeneo yote, na labda kufungua mwanya kwenye njia za mawasiliano, ambazo zinaendeshwa na viongozi, wa vikundi vinavyo nasibishwa (na pande za nje), ni ushahidi bora zaidi wa hili. Kifungu cha kupambana na kile kinachoitwa ugaidi, na kupambana na mashirika yote yanayoitwa ya kigaidi, kinakwenda sambamba na kifungu cha kuhifadhi umoja wa ardhi ya Syria. Inajulikana kuwa mtazamo wa mashirika yenye silaha na vikundi vya kijeshi kutoka kwa utawala wa Kirusi na utawala wa Kituruki, hutofautiana kiumbo na kukubaliana katika maudhui, na pande zote zinacheza dori sawa katika kudhibiti maamuzi ya mashirika haya.

Bila shaka, hatima ya mashirika na vikundi hivi inajulikana baada ya kucheza dori yao na kufikia malengo yanayotarajiwa yaliyowekwa na nchi changamfu katika faili ya Syria, ambazo zinataka kufikia masilahi yao kwa gharama ya masilahi ya watu wa Ash-Sham, na kutafuta kuihifadhi serikali ya vibaraka na ya kihalifu jijini Damascus; kupitia utekelezaji lile linaloitwa "suluhisho la kisiasa la Amerika" lenye sumu.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, nyumba ya Uislamu:

Kukabidhi uamuzi wa mapinduzi yenu yenye baraka kwa wale waliofanya njama dhidi yake na kufanya biashara na mihanga ya watu wake, na kimya chenu juu ya njama za maadui zenu na wale wanaodai kwa uwongo kwamba wao ni "marafiki" zenu, na kutojali kwenu na kunyamaza kwenu kuhusu yale yanayopangwa na kutabikishwa juu ya ardhi hii, bila shaka ni kujiua kisiasa, na kutumbukia shimoni, na kujitupa kwenye maangamizi, hasa huku mkiona kwa macho yenu jinsi mambo yanavyozidi kuwa mabaya zaidi, na kutoka kwenye ugumu hadi ugumu, na siku itafika ambapo mutajikuta muko baina ya meno ya dhalimu wa Ash-Sham na uhalifu wake, endapo mutasalia kimya. Kwa hivyo, tambueni tatizo, okoeni mapinduzi yenu, na mujiokoe nafsi zenu, watoto wenu na mali zenu. Kabla hamjachelewa.

Sisi ni ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir, muonyaji. Mushapitia ukweli wa kauli zetu na nasaha zetu kwenu, na hatutaki sifa kwa hilo, huu ni wajibu juu yetu, na tutakutana na Mwenyezi Mungu kwa hilo Siku ya Kiyama.

Kwa hiyo, kimbilieni kusahihisha mwenendo wa mapinduzi yenu, kupitia kuyakata mafungamano yote na nchi zile zinazoitwa zenye kuunga mkono, kwani hizo sio misaada, bali ni serikali za utendakazi zinazotaka kukuangamizeni.

Hebu na tuutabanni mradi wa wazi wa kisiasa unaochipuza kutokana na itikadi yetu ya Kiislamu, ili kudhamini kupata radhi na ushindi wa Mola wetu (swt) Mlezi kwetu. Kwani Mwenyezi Mungu (swt) hatayanusuru mapinduzi ambayo mradi wake wa kisekula unaitenganisha Dini yake na maisha, na unatekeleza mifumo ya ukafiri.

Ni jukumu letu kutabanni mradi wazi na madhubuti wa kisiasa, na sio tu kauli mbiu za kijumla, na inatupasa kufuata uongozi wa kisiasa unaofahamu, mwaminifu na wa dhati, ili kukwepa kile tulichomo ndani yake kutokana na tabia za kiholela zinazotokana na hamasa, na kutembea njia zilizo pinda.

Uongozi wa kisiasa ni kama kichwa cha mwili, na bila yake, hatutadhamini usalama wa njia yake wala uthabiti wa njia hiyo. Hii ndiyo njia pekee tunayoiona yenye wokovu. Basi, tafuteni wokovu na mujihadhari, Mwenyezi Mung (swt) asema:

[اسْتَعِينُوا بِاللَّهِ وَاصْبِرُوا إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ]

“Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu.” [Al-A’raf: 128].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu