Afisi ya Habari
Wilayah Syria
H. 22 Muharram 1447 | Na: 02 / 1447 H |
M. Alhamisi, 17 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Matukio ya Umwagaji damu huko Sweida Yafichua Hatari za Makundi Yenye Uhusiano wa Kigeni Uhalalishaji Mahusiano ni Jinai Inayohujumu Miaka 14 ya Muhanga wa Mapinduzi
(Imetafsiriwa)
Kufuatia siku kadhaa za mapigano makali yaliyogharimu maisha ya mamia ya ndugu zetu waliokufa shahidi, Wizara ya Ulinzi ghafla na kwa mshtuko ilitangaza Jumatano kuwa ni siku ya kuanza kujiondoa kwa jeshi la Syria katika mji wa Sweida. Haya yanajiri baada ya wito wa Marekani wa kuondoa vikosi vya serikali katika jimbo hilo na msururu wa mashambulizi makali ya anga yaliyofanywa na umbile la Kiyahudi mjini Damascus siku ya Jumatano, Julai 16, 2025, yakilenga jengo la Jeshi, Wizara ya Ulinzi na maeneo jirani ya Kasri la Rais. Mashambulizi ya awali yalikuwa yamepiga maeneo mengi viungani mwa Damascus, Daraa na Sweida, yakilenga maeneo ya kijeshi na misafara ya jeshi la Syria na vikosi jumla vya usalama vilivyokuwa vikielekea Sweida, na kusababisha idadi kubwa ya mashahidi na majeruhi.
Mapinduzi sasa yanakabiliwa na misukosuko mikubwa na changamoto zilizopo. Baada ya kumshinda mhalifu mkimbizi Bashar, lazima tusimame kidogo kwa ajili ya kujitafakari kwa dhati na kufanya tathmini ya kijasiri ya njia ya sasa, kwani makosa ya mara kwa mara yamedhoofisha hadhi ya mapinduzi na kuvuruga faida kubwa zilizopatikana kwa damu ya mujahidina. Huu ni wito wa kusahihisha mwenendo wa mapinduzi na kuregea katika sheria ya Mwenyezi Mungu.
Ni lazima tuwe na yakini kwamba kujisalimisha kwa maagizo ya kimataifa na kuamini ahadi za Marekani kutatupeleka tu kwenye hasara kamili hapa duniani na kesho Akhera. Wametuacha tukiwa hatarini kwa umbile la Kiyahudi, ambalo limeua mamia ya ndugu zetu mujahidina huku sisi tukishikilia kile kinachoitwa "haki ya kujibu," na kuyaacha makabila ya Kibedui huko Sweida wakiwa wamenyang'anywa silaha na kukabiliwa na kulipizwa kisasi bila ulinzi.
Uamuzi wa msamaha wa jumla: "Nenda, kwa kuwa uko huru!" uliashiria mgeuko hatari. Ulifanywa bila ya kushauriana na watu wa mapinduzi au kutafuta maoni ya mujahidina walioikomboa ardhi na kujitolea muhanga mkubwa zaidi. Hili lilikosa fursa muhimu ya kusuluhisha mambo kwa uamuzi na kufungua mlango wa machafuko. Ukawa ndio mwanzo wa msururu wa maafikiano, makubwa zaidi ambayo yalikuwa ni kumkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutoitekeleza Shariah yake kwa kisingizio cha kuiogopa Marekani na Magharibi ijapokuwa dola hizo zimekuwa ni maadui wakuu wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na mapinduzi ya ash-Sham tangu kuasisiwa kwake.
Kuwazuia mujahidina kulinda pwani wakati wa matukio ya zamani ilikuwa usaliti mkubwa, ikiruhusu wengine kupanua na kujipa ujasiri dhidi ya mujahideen.
Mtazamo wa upole wa kushughulikia suala la Druze ulifichua uzembe hatari wa utawala mpya. Mwakilishi wao alifukuzwa, ulinzi wa kimataifa uliombwa, na hata kulikuwa na mawasiliano na umbile la Kiyahudi – kitendo cha wazi na kisichoweza kukataliwa cha usaliti. Majibu kwa hili yalikuwa hafifu, kiasi cha kujisalimisha kwa wahusika wenye hatia ya uhaini mkubwa kwa kuwasiliana na kufanya uratibu pamoja na umbile la Kiyahudi.
Kupotea kwa utashi huru wa kisiasa pamoja na maamuzi yanayohusiana na maagizo, mipango, na maslahi ya Marekani na harakati za kupata kibali na ulinzi wao kumeufanya utawala mpya kushindwa kufanya maamuzi madhubuti kuhusu masuala ambayo yanaathiri sana ubwana na uhuru wa kitaifa. Hili lilidhihirika wakati wa mapigano ya ukanda wa pwani na ikawa wazi kwa faili la Druze, ikiwaanika mujahidina na kuifanya mihanga yao kuwa bure kabla ya malengo yao kufikiwa.
Itikadi yetu inafafanua uhusiano na umbile la Kiyahudi wanyakuzi wa matukufu yetu na wahusika wa uhalifu wa kutisha dhidi ya watu wetu mjini Gaza na kote Palestina kama moja ya vita na migogoro iliyopo. Vita kati ya wana wenye ikhlasi wa Umma na Mayahudi ni jambo lisiloepukika. Ni lazima pasiwe na uhalalishaji mahusiano au aina yoyote ya mkataba unaokubali hata shubiri moja ya ardhi ya Waislamu chini ya ubwana wao.
Vita na umbile la Kiyahudi ni jambo lisiloepukika, na ucheleweshaji wowote hupelekea upotezaji zaidi wa maisha na rasilimali. Kwa hivyo, lazima tujiandae kwa kila kitu tulicho nacho.
Hatua ya kwanza kuelekea ushindi ni kujitolea kikweli kutabikisha Shariah ya Mwenyezi Mungu bila kuchelewa au kukwepa kutafuta radhi na msaada Wake, sio wa Marekani au wengineo. Bila hili, kamwe hatutasimama imara, wala nchi haitafurahia usalama au ubwana. Ni lazima tutegemee msingi wa kimapinduzi na wanawe wenye ikhlasi, kwani wao ndio nusra ya kweli baada ya Mwenyezi Mungu wakati wa mgogoro na shida.
[وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]
“Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq :3]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Syria |
Address & Website Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria www.tahrir-syria.info |
E-Mail: media@tahrir-syria.info |