Jumatano, 09 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  28 Rabi' II 1447 Na: 03 / 1447 H
M.  Jumamosi, 20 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Makubaliano ya Aibu ya Kuhalalisha Usalama na Mayahudi na Miradi ya Ugawaji ni Hatari Kubwa Inayolenga Kuvunja Utashi wa Kiota na Ushindi Uliopata

(Imetafsiriwa)

Katika taarifa ambazo, kusema kwa uchache, ni hatari, zilizotolewa na mkuu wa awamu ya mpito, Ahmed al-Sharaa, vipengee vya hali ya sasa ya Syria vilifichuliwa. Alionyesha kwamba “Syria inajua jinsi ya kupigana, lakini haitaki tena vita,” na kwamba “haina chaguo ila kufikia makubaliano ya usalama na Israel,” wakati “kujitolea kwa Israel kwa makubaliano haya ni suala tofauti.” Pia alieleza kuwa matukio ya Sweida yalikuwa tu “mtego uliotayarishwa makhsusi kuzuia makubaliano ya awali juu ya utaratibu wa usalama,” na kwamba “baadhi ya mirengo ndani ya SDF na PKK ilivuruga makubaliano ya Machi na kupunguza kasi ya mchakato huo.” Amesisitiza kuwa “hali ya kaskazini mashariki mwa Syria inatishia usalama wa kitaifa wa Uturuki pamoja na Iraq,” na akadokeza kuwa “ikiwa uwiano hautafikiwa ifikapo Disemba, Uturuki inaweza kuchukua hatua za kijeshi.” Katika kujibu matakwa ya SDF ya ugatuaji wa madaraka, al-Sharaa ilisema kwamba “Syria inategemea 90% kwenye mfumo wa ugatuzi kwa mujibu wa Sheria Na. 107,” lakini kwamba “Mujtamaa wa Syria haujajiandaa kujadili ufederali,” akiyachukulia matakwa haya “kuficha kujitenga kusikokubalika.”

Sambamba na kauli hizi, utekelezaji wake wa kivitendo ulifanyika kupitia mkutano wa tatu kati ya Waziri wa Mambo ya Nje Asaad al-Shaibani na Waziri wa Masuala ya Kimkakati wa umbile la Kiyahudi Ron Dermer jijini London, mbele ya Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Syria Thomas Barrack, msanifu wa makubaliano ya aibu ya kuhalalisha mahusiano kati ya Damascus na umbile la Kiyahudi. Vyombo vya habari viliripoti kwamba wakati wa mkutano huo, al-Sheibani, Dermer, na Barrack walijadili rasimu ya mkataba mpya wa usalama uliowasilishwa na ‘Israel’.

Kauli zote hizi zinadhihirisha kiwango cha hatari ya njama iliyopangwa dhidi ya ash-Sham na watu wake. Msisitizo wa kupendekeza makubaliano ya usalama na umbile la Kiyahudi ni usaliti wa wazi wa damu ya mashahidi na jaribio lililoundwa na Marekani la kujisalimisha, linalokusudiwa kupita chini ya pazia la “usalama na utulivu.” Hata hivyo, ukweli ni kwamba lengo sio utulivu, bali ni kutiishwa kwa nchi na kiota chake na kuunganishwa kwake ndani ya mfumo wa majimbo kwa mujibu wa dira ya Marekani, ambayo hutumikia tu maslahi ya Amerika na umbile la Kiyahudi kwa gharama ya utashi wa watu wetu nchini Syria na watu wa eneo zima.

Madai kwamba matukio ya Sweida hayakuwa tukio la kupita, bali ni mtego uliotungwa kwa uangalifu, yananuiwa kukwamisha njia yoyote huru na kumakinisha mlingano unaotakiwa na walaji njama: Syria ima itii makubaliano ya kudhalilisha au itumbukie kwenye machafuko.

Kwa upande wa wanamgambo wa SDF, waliovalia guo la ugatuaji, hawawakilishi chochote zaidi ya mradi wa kujitenga unaoungwa mkono na nchi za kigeni, unaotumikia ajenda ya msambaratiko na mgawanyiko. Kisingizio cha Sheria ya 107 ni kifuniko tu cha kupigia debe umajimbo au kitu kilicho karibu nayo chini ya kisingizio cha uongo, kinachokusudiwa kutengeneza mazingira yafaayo kwa ajili ya kuvuruga umoja wa nchi baadaye.

Dori ya Uturuki katika mchezo huu hatari haiwezi kupuuzwa. Tishio la uingiliaji kijeshi kaskazini mashariki mwa Syria, na kuakhirishwa kwake kwa kubadilishana na mikataba ya kisiasa yenye shaka, si chochote zaidi ya karata ya ulaghai inayotumiwa na Ankara kulinda maslahi yake, hata itakuwa kwa gharama ya Syria. Nchi sio mashirika ya kutoa misaada; maslahi yao ndio yanayokuja kwanza.

Enyi Watu wa ash-Sham, kiota cha mapinduzi: Semeni kwa sauti kubwa: Jaribio lolote la kuweka makubaliano ya kusalimu amri na adui yetu wa milele, au kuendeleza miradi ya migawanyiko chini ya kivuli cha ugatuaji au ufederali, halitapita na halitakubaliwa. Hatukutoa maelfu ya mashahidi ili ardhi yetu iuzwe kwenye soko la uaini, wala watu hawakuasi ili jiografia yao igawanywe na utashi wao kukanyagwa. Kuweni kama mulivyokuwa kwenye mapinduzi yenu, imara kuliko njama zote.

Enyi Watu wa Mapinduzi, nyinyi mlioandikiwa hatima ya kushindwa baada ya ushindi mlioupata, kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, semeni kwa sauti kubwa: Yeyote anayeshirikiana na au kufanya biashara katika damu yetu atakutana na hatima mbaya kama walivyokuwa waliowatangulia. Tangazeni kwa sauti kubwa: Hatutapiga magoti, hatutalegeza msimamo, hatutatiishwa na mikataba ya aibu, na mradi wa ugawanyaji hautafaulu, bila kujali ni kwa kiasi gani dola za kimataifa na kikanda na zana zao zinakula njama ili kuulazimisha.

Enyi Watu wa Mapinduzi, wale waliojitolea mhanga, na wale wanaostahiki damu: Vita hivi leo si vita vya mipaka au mamlaka, bali ni vita vya uwepo na utambulisho vinavyobainishwa na Aqida (itikadi yetu). Ni jambo lisiloepukika kwa umbile la Kiyahudi na pamoja na wale wanaoliunga mkono umbile la Kiyahudi. Yeyote asiyetambua ukweli huu ni bwege. Yeyote anayetawanya kipande kidogo cha kile kilichokombolewa kutoka kwenye uchafu wa Assad kupitia damu ya mashahidi na mapambano ya waumini anatawanya mustakabali wa taifa zima na kulipeleka katika hali ya udhalilifu, utegemezi na unyonge. Hebu natusimame kwa pamoja tushinde mipango ya njama kabla hatujapoteza mafanikio yote ya ushindi ambao Mwenyezi Mungu ametukirimu nao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu