Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  2 Jumada II 1442 Na: 1442/26
M.  Ijumaa, 15 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi wa Kwanza wa Hizb ut Tahrir Nchini Tunisia

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23].

(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia inaomboleza kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla na kwa watu wa Tunisia haswa, mbebaji ulinganizi msafi, mcha Mungu, mmiliki wa tabia ya hali ya juu na fikra angavu, Ustadh Muhammad Al-Fadel Shatara, mzawa wa kijiji cha al-Ataya katika Kisiwa cha Kerkennah, aliyezaliwa mnamo Septemba 12, 1942 kijana cha mwanachuoni na khatibu, Sheikh wa Zaitouni, mtetezi na mwanaharakati Abdel-Fattah Shatara, ambaye roho yake – Mwenyezi Mungu amrehemu - ilifariki asubuhi ya Alhamisi 14 Januari 2021 M, akiwa na umri wa miaka 78, ambao aliutumia kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kwa kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, akijitolea nguvu zake zote na uwezo wake kubeba Da'wah hii kwa watu, akiwa ni mwenye subira, mshauri mzuri, akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuipenda Da'wah hii na wabebaji wake miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir.

Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alijiunga na da'wah hii katika miaka ya sitini ya karne iliyopita wakati wa masomo yake ya juu katika nyanja ya Michezo ya Kimwili na Ufundishaji wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.

Baada ya kurudi kwake Tunisia mnamo 1971, alifanya mazoezi ya ualimu katika Shule ya Uteuzi wa Walimu huko Carthage na kisha katika Kitivo cha Sayansi huko Tunis, kisha akasomea Misingi ya Dini (Usul-ul-Deen) katika Kitivo cha Sharia huko Tunis na kupata Ijaza.

Mwenyezi Mungu (swt) amlipe mema, alikuwa mwenge wa kwanza aliyebeba ulinganizi huu na kueneza fikra angavu nchini Tunisia, kwa hivyo aliweza, Mwenyezi Mungu amrehemu, kuanzisha halqa ya kwanza ya Hizb ut-Tahrir mnamo 1973, na yeye na wale aliokuwa nao wakaanza kuvuna wafuasi wa chama huko mji mkuu Tunis na nyumba ya Tamim, Gabes na Kerkennah, na baada ya hapo kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, ulinganizi huu ukaenea katika wilaya zote za nchi.

Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliubeba ulinganizi wa Khilafah katika mazingira magumu na bahari ya mawimbi makali, na akitangaza haki waziwazi na kuudhiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama wanamageuzi wote ambao wanatafuta kuhukumu kwa sheria ya kweli ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuwaamsha Waislamu. Serikali ya Bourguiba ilimkamata mnamo 1983 na alifungwa gerezani kwa dhulma, chuki na uadui, na baada ya kuachiliwa, alifanya kazi kama mwalimu wa elimu ya Kiislamu katika shule huru huku akibaki chini ya uangalizi wa karibu wa usalama.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aumiminie Ummah wa Kiislamu na sisi rehma zake pana kwa kupoteza huku, na kwamba amuingize katika Pepo Yake ya Firdaus ya juu kabisa pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, wema, na hao ndio marafiki wazuri, na kwamba amlipe yeye kwa ajili yetu na kwa niaba ya Waislamu malipo bora kabisa.

Hakika jicho linamwaga machozi, na hakika moyo unanyenyekea, na hatusemi ila yale tu yanayomridhisha Mola wetu, hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarudi, إنا لله وإنا إليه راجعون

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu