Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  6 Jumada II 1442 Na: 1442/27
M.  Jumanne, 19 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Imetosha Kucheza na Hatma ya Nchi Hii
(Imetafsiriwa)

Licha ya miaka kumi tangu mapinduzi yalipoanza dhidi ya mfumo ambao ukoloni ulipanda nchini Tunisia, uhalisia haujabadilika na serikali haijaanguka, ingawa baadhi ya nyuso zimeondolewa, na nyuso ambazo zina uhalifu na ubaya mchache kuletwa! Sababu ya hili ni utambuzi mbaya wa sehemu ya maradhi na maumivu ya janga. Tatizo kuu liko katika ushawishi wa kigeni na mfumo wake wa hadhara ya kirasilimali ambayo kwayo inadhibiti nchi, kuunda vibaraka na mafisadi na kusimamia mambo yao, kuwadhihaki kwa vyombo fisadi vya habari, kuwalinda kwa sheria na maagizo, na kuwaweka katika mandhari ya kisiasa kwa kughushi mapenzi ya wapiga kura na kushinikiza taasisi zake za kifedha, mfumo uliounganishwa kamilifu kwa ufisadi, kufisidi na uporaji, ambao kwao Magharibi na mabalozi wake wanadhibiti masharti na ala zake. Na wakati wowote watu wanapofanikiwa kumuondoa kabaraka, Magharibi inambadilisha na mtu mbaya zaidi kuliko yeye, na ni makosa kushughulisha na mkia wa nyoka na kukiacha kichwa kirushe sumu yake ndani ya mwili wa Ummah.

Leo hii maandamano hufanya upya na kuleta upya kwayo mzunguko na upotoshaji tabaka la kisiasa (watawala na upinzani) wanaopigana kati yao wenyewe ili kujionyesha kama mtumishi bora wa Magharibi na maslahi yake ya kikoloni.Wengine wao wanaunga mkono maandamano hayo, hata kwa nyuma ya pazia ili kulazimisha hali ya kikatiba inayomwezesha kuruka katika mamlaka ya uamuzi wa kuwa mlinzi wa mfumo wa Kimagharibi na mwajiriwa Mkuu miongoni mwa duru za wakoloni, na baadhi yao huyasifu maandamano na waandamanaji kama magenge yaliyovalia barakoa na kushikamana na mfumo fisadi ambao dhidi yake watu waliasi na kusababisha kuiweka rehani nchi kwa mlima wa madeni ya kigeni na mizigo mizito ambayo yalipooza uwezo wake wa mwamko na maendeleo sahihi ya kiuchumi, na kurithisha watu wake umaskini, kutengwa, gharama kubwa ya maisha, ukosefu wa ajira, kuzuia matarajio, na ukosefu wa usawa wa kieneo mbali na kuzorota kwa huduma za afya na elimu.

Na kati ya hii na ile, watu hubaki wamepotea, wakitaka kubadilisha hali hiyo, na hawajui jinsi ya kufanikisha hili?!

Sababu kuu iliyosababisha uzalishaji wa mfumo ule ule ambao watu waliasi mnamo 17Disemba 2010 M, na kuiwezesha Magharibi kudhibiti zaidi nchi; Kupanga, kutunga sheria na utekelezaji ni ukosefu wa wanamapinduzi wa mradi mbadala wa kihadhara kwa mfumo wa Kimagharibi, pamoja na ukosefu wao wa uongozi wa dhati na fahamu wa kisiasa, ambayo ilisababisha uchovu wa waandamanaji na mahitaji kwa matakwa ambayo yaliwazubaisha kwa dalili za tatizo bila ya kiini chake, na pia kuutenga Uislamu kutoka kwa utawala na sheria ili watu wapoteze matumaini ya mabadiliko.

Leo, mabadiliko makubwa yamekuwa jambo linalojiweka wenyewe kwa watu wetu nchini Tunisia, na hakuna njia mbadala au chaguo jengine isipokuwa kazi nzito ya kubadilisha uhalisia kwa msingi wa Uislamu. Kwa hivyo, inapasa juhudi zetu kuungana nyuma ya uongozi wenye ikhlasi kwa Mola wake unaoshikamana na Sheria Yake, wenye kutambua kiini cha kadhia, unaomtambua adui na hila zake, ili kukata mikono yake yenye kuhujumu nchi yetu na hatima yetu, na kauli mbiu yetu iwe "watu wanataka kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu."

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu