Alhamisi, 12 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  24 Safar 1446 Na: 1446/02
M.  Alhamisi, 29 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Wananchi na Jeshi la Kifahari la Tunisia Wanakubali Mapokezi ya Waziri wa Ulinzi wa wale Wanaoua Ndugu zao mjini Gaza?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, Agosti 28, 2024, Jenerali Michael Langley, Kamanda wa Kamandi ya Amerika ya Afrika (AFRICOM), alisema wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Tunisia Khaled El-Suhaili kwamba Tunisia iko mstari wa mbele katika nchi za Kiafrika zenye ushirikiano wa kihistoria na wa kipekee. Marekani, ikielezea utayari wake wa kuendeleza na kupanua mahusiano haya. Ziara hii inajiri siku tatu baada ya kuapishwa kwa wajumbe wa serikali. Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia tunakumbusha mambo yafuatayo:

1. Marekani ni nchi adui kwa Uislamu na Waislamu. Uhalifu wake wa kikatili nchini Iraq na Afghanistan unajulikana kwa wote, na uungaji mkono wake kwa umbile la Kiyahudi kwa silaha zinazoangamiza watu wetu huko Gaza, Jenin, na Palestina yote ni dhahiri na usiofichika. Je, watu wa Tunisia na maafisa wake watiifu wanakubali mapokezi ya wauaji hawa na wahalifu wa kivita katika nchi yetu, Tunisia?!

2. Mkutano kati ya Jenerali wa Marekani na Waziri wa Ulinzi Khaled El-Suhaili umekuja siku tatu baada ya Rais Kais Saied kuwashambulia wale aliowataja kuwa wanafungamana na dola za kigeni. Je, mapokezi ya Kamanda wa AFRICOM yanaendana na maneno ya Rais na msisitizo wake wa Tunisia kuwa dola huru katika maamuzi yake?! Je, Rais Kais Saied hatambui kuwa AFRICOM awali iliundwa kupambana na Uislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kuitawala Afrika?

3. Msaada wenye sumu wa kijeshi wa Marekani kwa jeshi la Tunisia si chochote ila ni rushwa na sumu iliyofinikwa kwa mafuta ili kuifunga imara Tunisia kupitia makubaliano ya usalama na kijeshi ambayo yameifanya Tunisia kuwa kambi ya hali juu ya majeshi ya Marekani barani Afrika.

4. Mkutano wa Kamanda wa AFRICOM na Khalifa Haftar nchini Libya baada ya ziara yake nchini Tunisia, na mkutano wake wa awali na Rais wa Algeria Tebboune, unathibitisha nia ya Amerika katika kanda nzima ya Afrika Kaskazini kutokana na umuhimu wake wa kimkakati kwa Ulaya, Afrika, na Mashariki ya Kati. Kwa hivyo, juhudi za Marekani za kuondoa ushawishi wa dola za kikoloni za zamani hazitakoma hadi pale Marekani itakapopata udhibiti wa kanda hii, ikiwemo Tunisia, ikisaidiwa na uoga na usaliti wa watawala.

Enyi Watu wa Tunisia, Ardhi ya Mujahidina Mashujaa:

Kamanda wa AFRICOM aliyeruhusiwa kuingia nchini mwetu na watawala wa Tunisia ni muuaji mhalifu, na nchi yake, Amerika, iko katika hali ya vita kivitendo dhidi ya watu wetu huko Gaza, Jenin, na Palestina yote. Hali hiyo hiyo inatekelezeka kwa Ufaransa, Uingereza, na Ulaya. Udhalilishaji huu tuliowekewa na watawala wetu utaisha tu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kuweni miongoni mwa wanaoifanyia kazi, na mutapata malipo ya dunia na Akhera.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surat Al-Ma’ida:51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu