Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 23 Rajab 1445 | Na: 1445 / 19 |
M. Jumapili, 04 Februari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Tangazo la Misaada ya Kigeni kama Silaha Dhidi ya Sanaa
Je, Serikali ya Wokovu Imegeukia Misaada ya Kigeni kwa Sababu ya Uhaba wa Machaguo au Hakuna Chaguo Jengine?!
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Kila Siku la Al-Thawra, lililotolewa mjini Sanaa mnamo Ijumaa, Februari 2, 2024, lilizingatia majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Hussein Al-Azzi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kupitia tweet yake kwenye jukwaa la X. Alisema: “Waingereza kudokeza kutumia misaada kama silaha dhidi ya watu wa Yemen ni aibu,” Naibu Waziri aliongeza katika tweet yake kwamba “dokezo hili halitawazuia watu wa Yemen kuendelea na uungaji mkono wao wa haki wa msaada wa kibinadamu kwa raia mjini Gaza.”
Haya yanajiri kufuatia wito wa Umoja wa Mataifa mnamo Alhamisi, Februari 1, 2024, kutoa dolari bilioni 2.7 kufadhili operesheni za kibinadamu nchini Yemen katika mwaka wa 2024.
Yaliyoelezwa kwenye tweet ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wokovu, Hussein Al-Azzi, yanaashiria kung'ang'ania kwa serikali yake kubaki na misaada kutoka nje ya nchi zinazoipiga vita, badala ya kuikataa moja kwa moja, jambo ambalo linastahili! Hasa tangu nchi hizo zianze kutumia misaada kama silaha kufikia malengo ya kisiasa!
Huku Washington ikiweka kando uwekaji vikwazo kwa Sanaa kwa sababu vitaathiri watu, Uingereza inashikilia wazi silaha ya misaada kushawishi maamuzi ya kisiasa ya serikali ya Sanaa!
Misaada ni silaha hatari iliyofichwa mikononi mwa wanaoitoa; wanaitumia kwa urahisi wao. Ina vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na chakula, matibabu, elimu, kijamii, kimazingira, na malengo mengine fiche yaliyofichwa chini ya kibandiko cha "msaada"! Baadhi ya misaada hii inakuja na masharti kutoka kwa nchi wafadhili, yaliyoundwa kimsingi katika nchi inayotoa, na wafanyikazi wake wanaenea katika miji na vijiji vya Yemen kwa njia zisizoweza kufikirika! Kama kawaida, sehemu yake inaishia kwenye mifuko ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na baadhi ya mawaziri na watu binafsi wenye ushawishi ambao, kwa maumbile ya "misaada," wanaitarajia ndani ya maeneo yao ya utaalam. Tumeonya mara kwa mara juu ya hatari ya misaada ambayo serikali inayotawala nchini Yemen imeizoea kwa miongo kadhaa. Msingi wa kibinadamu wa tweet ya Al-Azzi unaonyesha kwamba haitokani na Aqeeda ya Kiislamu. Kwa nini?!
Na swali kubwa hapa ni: Kwa nini Mahouthi wanasisitiza kuendelea kwake?! Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wokovu aliwasilisha barua rasmi mnamo Januari 21, 2024, kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Mpango wa Chakula Duniani, Cindy McCain, mjane wa marehemu mgombea urais wa Republican John McCain. Kabla ya hapo, kulikuwa na wito wa Mohammed Ali al-Houthi mnamo Novemba 26, 2023, kudumisha Mpango wa Chakula wa Ulimwenguni wa Marekani.
Kutokuwepo kwa programu za Serikali ya Wokovu kwa miaka mingi kunaakisi tegemeo lake kwa wengine, yeyote awaye. Mpango dhaifu wa Ruwaza ya Kitaifa, ambao umekuwa nusu ya maisha ya Serikali ya Wokovu, na ruwaza yake kuu ya kiuchumi inayodaiwa kuwa imeundwa ili kuwapunguzia wananchi mizigo ya kiuchumi, ngano kisaki inayoingizwa nchini kutoka nje na kulimwa huko Saada, Al-Jawf, Al- Hudaydah, na kwengineko, na bidhaa zilizosusiwa zinazofurika sokoni, mpango huu unagongana na kanuni za Kiislamu na haujatoa chochote kinachoonekana katika uhalisia!
Hivi ni nini kinachoitofautisha Serikali ya Wokovu na watangulizi wake, ukiachalia kauli mbiu?! Kauli mbiu ya mabadiliko inatangazwa, lakini haipo kivitendo. Serikali ya Wokovu haijawaokoa watu katika maeneo yake inayoyadhibiti; badala yake, imewaangamiza na kuwasagasaga, sawa na serikali ya Baraza la Rais kusini na mashariki mwa Yemen! Matendo yao yana madhara. Mabadiliko ya kweli yanaweza tu kuja kwa kusimamishwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi, kuwalingania watu wa Yemen kuwa sehemu yake.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |