Jumatano, 15 Shawwal 1445 | 2024/04/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  1 Sha'aban 1445 Na: 1445 / 21
M.  Jumapili, 11 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Mwaka Mwingine wa Hijria Unaotuleta Karibu na Kusimamishwa Khilafah
(Imetafsiriwa)

Ifikapo tarehe 28 ya mwezi wa Rajab al-Fard, 1445 H, tutakuwa tumefika mwaka wa 103 wa kuanguka kwa Khilafah ya Uthmaniya... na utapita mwaka mwingine wa Hijria, unaotuleta karibu na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Baada ya kutokuwepo ambapo sisi Waislamu tulifiwa, mama yetu alikuwa Khilafah na baba yetu alikuwa Khalifa wa Waislamu. Mamlaka ya Waislamu yalitoweka duniani na pamoja nayo utawala wa Uislamu haukuwepo, hivyo hali yetu ikawa mbaya. Mataifa yametushambulia kutoka pande zote, yanavamia nchi kavu, baharini na angani, yanapigana vita dhidi ya Dini yetu, yanatuua, yanamwaga damu yetu, yanatuhamisha makao yetu katika ardhi yetu, yanazikalia kimabavu na kuzichana ardhi zetu, na yana ulafi kwa mali zetu... Majeraha yetu yanavuja damu nyakati hizi katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na haswa mjini Gaza, majeraha na maumivu kuanzia Sudan hadi Yemen... yakiongezewa na majeraha yaliyopita!

Ni mwaka mwingine wa Hijri ambapo ulimwengu unatumbukia katika shimo kubwa, huku ukiingia kwenye vita vipya, migogoro ya kisiasa kutokana na mzozo mkali kati ya nchi za kibepari, migogoro ya kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa madeni ya hazina za umma za nchi kwa kushindwa uwezo wao wa kulipa, na migogoro ya kijamii kutokana na kuibuka kwa mahusiano yasiyo ya kawaida yasiyo sahihi kati ya wanaume na wanawake. Yote haya ni kwa sababu ya mtazamo wa kimakosa wa ulimwengu, mwanadamu na maisha, ambapo umepelekea kutenganishwa kwa dini na maisha.

Uislamu pekee ndio wenye uwezo wa kuokoa ulimwengu kwa kuifanya haki itawale, na kufikia mizani ya uadilifu ambayo haikuwepo kwa kutokuwepo hukmu ya Uislamu, ambayo hailegezi msimamo kwa mtu yeyote aliye katika utawala ... na ambayo kwayo wapinzani wanakuwa sawa mbele ya mahakama, na yenye kulinda fedha, maisha, na haki za watu kutokana na uovu wa madhalimu na ufisadi wa mafisadi, hata wawe nani. Tuna mafunzo mengi kutoka kwa: “Ulihukumu, ukawa salama, ukala, ewe Umar,” na kutoka kwa: “Tangu lini umewafanya watu kuwa watumwa wakati mama zao waliwazaa wakiwa huru?”, na kutoka kwa: “Wa Mu’tasimah.”

Ulimwengu leo unaharibiwa na mioto ya mifumo uliyotungwa na wanadamu. Walifanya makosa katika mtazamao wao kuhusu ulimwengu na maisha, kwa hiyo hawakujua ukweli na uadilifu. Shetani aliwapendezeshea matendo yao na wakadhania kuwa wameongoka!

[الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعاً]

“Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri.” [Al-Kahf: 104]

Enyi watu wenye nguvu na ulinzi nchini Yemen wenye imani na hekima! Enyi wajukuu wa Saad bin Muadh, Usayd bin Hudayr, Saad bin Ubadah, Al-Qaqa bin Amr, na Al-Habbab bin Al-Mundhir, Mwenyezi Mungu awe radhi nao: Sisi, kama Waislamu tunaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah tunawageukia watu wenye nguvu kutoka kwa watu mashuhuri wa Yemen na maafisa na askari wa jeshi letu, ili kuunusuru Uislamu na kuipa nguvu Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake kuchukua madaraka. Tunawakumbusha maafisa na askari wa jeshi nchini Yemen, ambao wamekuwa wakielekezana silaha zao vifuani mwao na kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa. Tunawakumbusha kwamba silaha zilizo mikononi mwao lazima, kwa udharura, zinyanyuliwe ili kuunusuru Uislamu na vita viwe dhidi ya maadui zao. Tunawakumbusha,

[فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ]

“Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.” [Adh-Dhariyat: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu