Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 29 Safar 1446 | Na: HTY- 1446 / 05 |
M. Jumanne, 03 Septemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utunzaji nchini Yemen ni Dhaifu kuliko Nyumba ya Buibui!
(Imetafsiriwa)
Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa mnamo Jumamosi tarehe 31/8/2024 katika wilaya ya Bani Musa Al-Jarf huko Wusab As Safil Wilaya ya Dhamar, yalisababisha vifo vya watu 27, kujeruhiwa kwa watu 8, na kupoteza watu 2. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mafuriko hayo pia yamesababisha kubomolewa kwa nyumba 15, uharibifu wa nyumba 8 katika wilaya ya Wadi Al-Akhshab, na kusombwa kwa magari 4, pikipiki 2 na duka moja. Hapo awali Umoja wa Mataifa ulisema mafuriko yaliyokumba jimbo la Al-Mahwit mnamo Jumanne iliyopita tarehe 27/8/2024 yalisababisha vifo na hasara ya zaidi ya watu 41 na kuathiri takriban familia elfu moja. Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu limedokeza kuwa maafa hayo yametokana na mvua kubwa iliyonyesha na mlipuko wa mabwawa matatu katika wilaya ya Malhan.
Mvua zilizonyesha katika maeneo mbalimbali nchini tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti iliyopita zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 120, na kuathiri takriban watu robo milioni, hasa wanaoishi katika kambi za wakimbizi, mabonde na tambarare, na kusababisha uharibifu wa nyumba, mali, mashamba na barabara katika majimbo kadhaa ya Yemen. Maafa haya yanaongeza mateso kwa watu wa Yemen wanaoteseka sana. Mateso yataendelea maadamu Waislamu wanaishi bila ya dola inayotekeleza Shariah ya Mola wao na mambo yao yamechukuliwa na watawala wahalifu ambao ni vibaraka wa Magharibi. Hatujaona chochote kutoka kwao isipokuwa umwagaji damu, uporaji wa fedha, migogoro ya viti, na kuiuza nchi na watu wake kwa maslahi ya makafiri wakoloni wa Magharibi!
Watu wa Yemen wamefuata maombi ya watu wa wilaya ya Hamdan katika wilaya ya Malhan katika mkoa wa Al Mahwit kwa mamlaka rasmi ili kuwasaidia, lakini maombi haya yalikabiliwa na uzembe na kutojali mateso ya watu. Siku mbili baada ya maafa hayo, mkuu wa Shirika la Habari la Saba jijini Sana'a alisema kuwa upatikanaji wa eneo hilo bado ni mgumu kutokana na kufungwa kwa barabara! Kauli hii inaonesha ni kwa kiasi gani uzembe umefikia katika masuala ya maisha na mali za watu, ukiachia jukumu la uokoaji, makaazi na huduma ya kwanza kwa jamii! Je, ni busara kwamba uwezo wa nchi nzima umeshindwa kutafuta njia ya kuwasaidia waathirika?!
Vyanzo vya kodi ambavyo mamlaka ya Sana'a inakusanya havihesabiki, kwani hakuna tena wakala wowote wa huduma za serikali, bali zote zimekuwa za kuzalisha mapato! Yale yanayoitwa maeneo halali pia yanafurahia rasilimali na utajiri, na ni viongozi na watu mashuhuri pekee wanaofaidika nayo. Kauli mbiu mashuhuri ya watawala hao pamoja na watangulizi wao ni kwamba utawala ni faida (nguvu na mali), na kula pesa za watu kwa dhulma kupitia kodi na ushuru ulioharamishwa na kuunyima Umma rasilimali zake ili kujaza matumbo na mishipa yao na kufurahia pesa za Ummah, bila kujali mateso na masaibu ya watu! Popote unapoenda, hatapata huduma hata katika mambo rahisi! Watawala hawa wanapuuza kuwa uchungaji mambo ni jukumu lao, kwani ni wajibu wao kutunza mabwawa, kuweka lami na kutengeneza barabara, kuwaondoa wakaazi kutoka katika njia za mafuriko na kuwapeleka katika maeneo salama, kutoa miundombinu, huduma za afya na huduma...
Mtawala katika Uislamu lazima awe mchungaji na mtumishi wa Ummah. Kutoka kwa Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kutoka kwa Mtume (saw) amesema: «فَالْأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ» “Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya anachochunga.” (Imepokewa na Al-Bukhari).
Sisi tunao mfano mzuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kigezo cha hali ya juu; Imepokewa kutoka kwa Bukhari kutoka kwa Anas ambaye amesema: Mtume (saw) alikuwa mbora wa watu, mkarimu kuliko watu wote, na shujaa wa watu. Watu wa Madina waliogopa usiku mmoja, basi watu wakatoka kuelekea kwenye sauti, na Mtume (saw) akawakuta akiwatangulia watu kwenye sauti hiyo, na alikuwa akisema: «لَنْ تُرَاعُوا لَنْ تُرَاعُوا» “Msiwe na msiwe na wasiwasi.” Alikuwa amepanda farasi wa Abu Talha bila tandiko na upanga ulining'inizwa shingoni mwake. Akasema, “Nimemkuta (farasi) kama mto mkubwa” au alikuwa mto mkubwa (akimaanisha kasi yake).
Enyi Waislamu: Suluhisho pekee la kuwaokoa wanadamu kutokana na maovu ya wajeuri na madhalimu ni kuregea kwa Uislamu tu kama mfumo uliotekelezwa; ni mfumo wa kiwahyi unaoshughulikia mahitaji yote ya wanadamu na unaoangalia mambo ya wanadamu kwa jumla na haswa Waislamu, na ndio pekee unaofikia utunzaji wa kweli.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |