Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 10 Jumada I 1446 | Na: HTY- 1446 / 07 |
M. Jumanne, 12 Novemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ala za Kindani kama Kikaragosi cha Makafiri wa Magharibi katika Kutekeleza Sera Zake, na Hakuna Suluhisho kwa Watu wa Yemen isipokuwa kwa Kutekeleza Shariah ya Mwenyezi Mungu
(Imetafsiriwa)
Zaidi ya miezi mitatu iliyopita, Muungano wa Kikabila wa Hadhramaut na Kongamano Jumuishi la Hadhramaut, lililoongozwa na Amr bin Habrish Al-Alyi (ambaye ameshikilia nafasi ya Naibu Gavana wa Kwanza wa Jimbo la Hadhramaut kwa miaka tisa), alitangaza kikao kwenye Meza ya Hadhramaut ili kurudisha haki zilizoporwa za Hadhramaut. Walisimamisha usafirishaji ng’ambo wa dizeli kutoka kwa kampuni ya PetroMasila, ambayo ilisababisha kampuni hiyo kusimamisha uzalishaji wake. Malori yanayoondoka kwenye kampuni, ambayo hutoa soko la ndani na vifaa kama vile vituo vya umeme mjini Mukalla na miji mengine, yalizuiwa kupita.
Kikao hicho kinaambatana na habari za makubaliano kati ya serikali ya Baraza la Rais na Mahouthi kuanza tena mauzo ya mafuta kutoka Hadhramaut baada ya kusimama kwa muda mrefu kufuatia mashambulizi ya Houthi kwenye bandari za mafuta chini ya udhibiti wa Baraza la Rais. Mkutano huo ulifanyika wakati Rais wa Baraza la Uongozi wa Rais wa Yemen alipozuru Hadhramaut mnamo Julai 27, 2024, bila kuhutubia kikao hicho. Katika kujibu, Kongamano Jumuishi la Hadhramaut lilieleza msimamo wake kuhusu hali mbaya ya maisha na huduma jimboni Hadhramaut, na kusisitiza kwamba jimbo hilo halijapata uangalizi unaostahili kutoka kwa mamlaka zinazohusika licha ya hadhi yake. Badala yake, limekabiliwa na kutelekezwa kwa makusudi na kutengwa licha ya muhanga na msimamo wake. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kongamano Jumuishi la Hadhramaut lilibainisha kuwa ziara ya Rashad Al-Alimi huko Hadhramaut haikukubalika na hata kukataliwa hadi matakwa yatimizwe na Hadhramaut ipate haki zake kamili.
Mpaka sasa, kikao kingali kinaendelea, bila kufikia malengo yaliyokusudiwa; matakwa ya waandamanaji hayajatekelezwa, wala mafuta hayajauzwa nje ya nchi kulingana na makubaliano yaliyodaiwa na Mahouthi. Katika kipindi hiki, Gavana wa Hadhramaut, Mabkhout bin Madi, alitembelea kikao hicho na kueleza kuunga mkono matakwa hayo bila kuchukua hatua yoyote madhubuti ya ima kukomesha au kufikia malengo yake. Hili limesababisha mgogoro mkubwa wa mafuta katika jimbo hilo, na kuongezeka kwa kukatika kwa umeme kutokana na ukosefu wa vifaa vya dizeli kutoka PetroMasila kwa ajili ya vituo vya umeme. Mfumo wa umeme mjini Aden pia umeathiriwa na kukatwa kwa vifaa kutoka kwa PetroMasila.
Yeyote anayetazama hali hii anaweza kuona kwa uwazi jinsi mashirika ya ndani yanavyoendeshwa ili kufikia mafanikio ya kisiasa huku kukiwa na mzozo unaoendelea Yemen. Wakati Saudi Arabia ilipoishinikiza serikali kufikia makubaliano na Mahouthi na kuanza tena mauzo ya mafuta, UAE ilishajiisha Muungano wa Hadhramaut kusonga na kuzuia makubaliano haya. Katika mkutadha huu, Saudi Arabia pia ilihuisha Baraza la Kitaifa la Hadhramaut, ikifanya mkutano nalo nchini Saudi Arabia mnamo Oktoba 8, 2024, na kutangaza marekebisho ya kiutawala ya baraza hilo. Hii inaonyesha jinsi vyombo mbalimbali vya ndani vinavyofanya kazi chini ya muonekano wa lengo moja - kutumikia Hadhramaut - lakini ukweli ni kwamba utiifu wao wa kisiasa unatofautiana. Kwa hiyo, misimamo yao inatofautiana, na wakati mwingine kusababisha mizozo ya umwagaji damu ambayo inatumikia maslahi ya dola za kikoloni, ambazo huingilia kati kupitia mawakala wao wa kikanda bila shida yoyote.
Watu wetu wa Hadhramaut na Yemen yote lazima watambue kwamba uongozi wa kisiasa nchini Yemen, kaskazini na kusini, haujali matatizo na mahitaji yao. Kinyume chake, unazidisha tu mateso yao, iwe kupitia kuzorota kwa uchumi au kukosekana kwa huduma muhimu kama vile umeme, maji, na mahitaji mengine kwa maisha yenye staha. Ni lazima tuondoe uaminifu wetu kutoka kwa wao wote, kwani pindi wanapotenda, huitumikia Magharibi kafiri, na wanaponyamaza, wanapora mali ya nchi na watu wake bila ya uwajibikaji au uangalizi!
Tunakukumbusheni maneno ya Mwenyezi Mungu:
[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً]
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki,” [Ta-Ha:124]. Leo, tumeipa mgongo Dini ya Mwenyezi Mungu na hukmu zake katika siasa, uchumi na nyanja zote za maisha. Upuuzaji huu, unaoakisiwa kwa kukosekana kwa utawala wa Kiislamu, ndio chanzo kikuu cha matatizo yetu, ugumu wa maisha yetu, na utawala wa wale wasiotujali. Kwa hivyo, tunakuombeni mushirikiane nasi kuwaondoa watawala hawa vibaraka na kumpa bay'ah kiongozi ambaye atatutawala kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake chini ya dola inayotekeleza Uislamu: Khilafah kwa njia ya Utume.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |