Jumanne, 04 Safar 1447 | 2025/07/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  26 Muharram 1447 Na: HTY- 1447 / 02
M.  Jumatatu, 21 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mafanikio ya Kiuchumi ya Mahouthi Baada ya Miaka 11:
Kutengeneza Sarafu Mbili za Riyal 50 na 100!!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatatu, tarehe 14/07/2025, Waziri wa Habari wa Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko, Hashem Sharaf al-Din, alitoa taarifa kwa Shirika la Saba, ambapo alisema: “Kila sarafu ya kitaifa inayotolewa kwa wananchi ni daraja la kuelekea katika maamuzi huru, na kila ushindi wa kiuchumi unaopatikana ni ngome isiyotikisika mbele ya dhoruba na kila mafanikio ya kifedha ni ngao ya kinga katika vita vya hadhi, na upanga unaozikata njama za maadui wa Yemen, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwanza, kisha kwa azma ya watu wasiojua lisilowezekana.”

Taarifa hii imekuja kufuatia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Benki Kuu ya Mahouthi jijini Sana’a mnamo Jumamosi, 12/07/2025, ambapo ilitangaza utengezaji wa sarafu ya Riyal 50 kuchukua nafasi ya sarafu ya karatasi iliyoharibika ya kiwango hicho hicho, itakayosambazwa kuanzia siku inayofuata, Jumapili, 13/07/2025. Hii inafuatia utengezaji wa sarafu ya Riyal 100 mnamo Machi 2024, na siku moja kabla ya kutolewa kwa sarafu ya karatasi ya Riyal 200.

Ni haki kwa mtu kuuliza: Je, Mahouthi wametimiza yale waliyowaahidi watu wa Yemen katika mapinduzi yao ya tarehe 21 Septemba 2014? Na je, kitendo chao hiki ni suluhisho msingi kwa mujibu wa mtazamo wa Kiislamu juu ya miamala ya kifedha na sarafu isiyo na thamani ya dhati (fiat), au kuhamia kwenye kiwango cha dhahabu na fedha? Au ni suluhisho tu la viraka ndani ya mfumo wa Benki ya Dunia na mfumo wa uchumi wa kibepari, na sio nje yake?

Kwa kuzingatia hali ya sasa ya mambo, inatosha kuwa jibu: Mizigo ya kiuchumi imeongezeka, pamoja na bei za bidhaa zinazotokana na mafuta ya petroli na gesi, mara nyingi zaidi. Ukusanyaji wenu wa fedha umeongezeka zaidi ya ulivyokuwa kabla ya Septemba 2014. Kadhalika, bei ya nyuzi za umeme imeongezeka, pamoja na kusimamishwa kwa mishahara ya sekta ya umma. Ukusanyaji wenu wa pesa umeongezeka zaidi ya ulivyokuwa.

Na baada ya yote haya, munasherehekea na kupiga tarumbeta na kusifia uhalisia wa ufisadi kama mafanikio ambayo hayajawahi kutokea, kwa kubadilisha sarafu mbili za chuma na noti ya karatasi ya tatu mahali pa sarafu za karatasi zilizoharibiwa! Na munazitaja kuwa ni daraja, ngome, ngao, na upanga—kama alivyosema Waziri Sharaf al-Din—katika muktadha wa mfumo wa uchumi wa kibepari unaooza, unaoyumba duniani! Bila kujua tofauti kati yake na mfumo wa uchumi wa Kiislamu.

Je, Waziri Sharaf al-Din anazungumza kuhusu ubwana, ushindi wa kiuchumi, ujuzi na utoshelevu upi, wakati Idara ya Hazina ya Marekani ilikuwepo kwenye makubaliano ya Sana’a na Aden kuhusu uhamisho wa benki hadi Aden mwezi uliopita? Na wakati IMF, Benki ya Dunia, na ala zao kama vile Mpango wa Chakula Duniani bado zinafanya kazi Sana’a? Je, uthabiti wa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni jijini Sana’a dhidi ya Riyal ni vya asili au ni bandia? Imedhihirika kwa watu wa Yemen kwamba hamuna dira ya wazi ya kiuchumi, wala mpango wa kiuchumi uliotayarishwa kabla—nyinyi pamoja na wale walioongeza usambazaji wa fedha katika Benki Kuu ya Aden bila ya hofu au uchaMungu—na kusababisha upotevu wa mali za watu. Nyinyi na Baraza la Al-Alimi mnashindana katika ufisadi.

Ewe Waziri Sharaf al-Din:

Tunataka sarafu ya dhahabu—“dinari yenye uzito wa gramu 4.25 za dhahabu ya karati 24”—katika miamala ya kifedha, sio saini ya dhahabu kama ulivyotaja katika taarifa yako kwa Shirika la Saba, ambalo linasifia uhalisia wa ufisadi kuwa ni mafanikio yasiyo na kifani, bila kujua tofauti kati ya mifumo miwili ya kiuchumi, ni baina ya mbinguni na ardhi!

Suluhisho kuu la tatizo la sarafu ni kuregea katika kiwango cha dhahabu, iwe kupitia biashara ya moja kwa moja ya dhahabu au kupitia noti wakala zinazoweza kubadilishwa bila kizuizi au masharti. Wanauchumi wengi wamegundua hili. Lau si upinzani kutoka kwa nchi husika, hasa Marekani—kuogopa kupoteza udhibiti wake wa kisiasa na kiuchumi—ulimwengu ungerudi kwao, kwa sababu mfumo huu unahifadhi utulivu na kusababisha ustawi katika shughuli ya kiuchumi bila nchi moja kuitawala nchi nyingine. Ndani yake, sarafu hufungwa kwa kiwango ambacho kinaheshimiwa na kuthaminiwa kiulimwengu. Pia, chini yake, dola haziwezi kuongeza usambazaji wa pesa kiholela, kwa sababu zimefungwa kwa hifadhi ya dhahabu. Hii ni kinyume cha sarafu za fiat (zisizo na thamani ya dhati).

Mtazamo wa Kiislamu unaweka wazi kwamba hakuna kitu kilicho halali kuwa kama fedha isipokuwa dhahabu na fedha, kwa kuzingatia dalili za Kiislamu, miongoni mwazo ni idhini ya Mtume (saw) ya kutumia dhahabu na fedha kama sarafu katika dola ya Kiislamu. Uislamu umehusisha hukmu za kisheria na dhahabu na fedha: umeharamisha kuzifanyia ukiritimba, ukawajibisha zaka kutoka kwazo ukizingatia kuwa ni sarafu na bei za bidhaa na ujira wa kazi: (Kwa kila dinari 20, nusu dinari; na kwa kila dirham 200, dirham tano.) Uislamu umeweka fedha za umwagaji damu kwa dhahabu na fedha, na pia nisab kwa wizi pindi masharti yanapotimia: “Mkono wa mwizi usikatwe isipokuwa kwa (thamani ya mali ilioibwa) ya robo dinari au zaidi.” Kwa hivyo, dola inayotaka kurudi kwenye kiwango cha dhahabu lazima ifuate sera ya kujitosheleza: kupunguza uagizaji na kubadilishana bidhaa kutoka nje na za ndani. Ni lazima pia iuze bidhaa zake kwa badali ya zile inazohitaji au kwa dhahabu na fedha au kwa sarafu inazohitaji ili kuagiza mahitaji kutoka nje. Mfumo huu lazima utekelezwe kikamilifu na sio kivipande, pamoja na hukmu nyenginezo za kisheria za Kiislamu katika utawala, mahakama, elimu, nk., chini ya dola ya Khilafah.

Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Yemen tunawajibika kuwabainishia watu wa Yemen hasa, na Waislamu kwa jumla, uhalisia wa shughuli za kisiasa zinazotokea nchini Yemen ambazo zimefichika kwa watu, na kubainisha hukmu husika za Kiislamu. Tunafanya kazi na tunatoa wito kwa watu wa Yemen kufanya kazi pamoja nasi ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume; kutabikisha Uislamu na kupanga nyanja zote za maisha kwa mujibu wa sheria na fikra zake—sio kwa mujibu wa mfumo au sheria nyengine zozote. Hizb ut Tahrir imetayarisha watawala na njia ya kina kwa ajili ya dola inayokuja ya Khilafah—hivi karibuni, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur:55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu