Alhamisi, 03 Sha'aban 1447 | 2026/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mwenye Hekima si Yule Anayesitasita Kati ya Mema na Maovu, Bali Yule Anayechagua Mema
(Imetafsiriwa)

Ni sababu gani za udhaifu wa Waislamu leo? Kwa nini heshima yao inavunjwa, ardhi yao inanyakuliwa, na wanamefukarishwa na kutiwa njaa, lakini hawajitetei dhidi ya dhulma, udhalilifu, na kudunishwa? Kwa nini wanatazamana wakifa kwa njaa, mauaji, na mateso mikononi mwa makafiri wahalifu bila kuinua kidole? Kwa nini wanahisi hawana msaada, dhaifu, na watiifu kwa Magharibi mbele ya majanga na vitisho vyote vinavyowapata?

Umma wa Kiislamu uliunganishwa chini ya bendera ya Dini yake, na Khalifa mmoja aliyetekeleza sheria za Mola wake Mlezi, na ambaye aliitikia na kutii amri zake. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Kitabu chake kitukufu:

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً]

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. [Aal-i-Imran: 103].

Amri ya kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa pamoja ni wito kwa Ummah wa Kiislamu katika kila zama na mahali... wito wa kudumu, na unaoendelea. Waislamu lazima wakusanyike kukizunguka Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw), na wasifarakane, kwani hiyo ndiyo sababu ya kushindwa, udhaifu na unyonge:

[وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَأُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ]

Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. [Aal-i-Imran: 105].

Hii ilikuwa hali ya Waislamu chini ya Khilafah: wenye nguvu na kuogopwa na maadui zao, ambao hawakusubutu kuwashambulia au kuwadhuru. Walikuwa raia wa dola yenye nguvu ambayo sifa yake ilienea mbali, ikijulikana miongoni mwa mataifa. Khalifa wake hangesita kuandaa jeshi kubwa kupigana na yeyote aliyesubutu kushambulia raia wake yeyote.

Mwenyezi Mungu (swt) alisisitiza umuhimu wa kundi la Waislamu kuwa Umma mmoja; kwani katika umoja wake kuna nguvu yake, na katika kushikamana kwake na Dini na sheria yake kuna mwendelezo wake, ubwana wake, na kheri yake. Kwa hivyo, “Umma,” inamaanisha nini na inamaanisha nini kwa Waislamu kuwa Umma mmoja?

Amesema Mwenyezi Mungu (swt) akizungumzia kuhusu bwana wetu Ibrahim, rehma na amani ziwe juu yake, na wafuasi wake walioamini Dini moja na kushikamana katika itikadi moja:

[تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُمْ مَا كَسَبْتُمْ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ]

Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao. [Al-Baqarah: 134].

Kwa maana hii, Ummah (taifa) ni kundi la watu wanaoamini dini au itikadi moja, na kwa hiyo hisia zao ni moja. Kwa hivyo tunasema, “Hili ni taifa la kibepari,” “Hili ni taifa la kikomunisti,” na “Hili ni taifa la Kiislamu.” Hatuwezi kusema, “Hili ni taifa la Kiarabu” au “Hili ni taifa la Kituruki,” kwa sababu ingawa wako chini ya mfumo mmoja, watu wake hutofautiana katika imani na fikra zao.

Al-Saadiy anasema katika tafsiri yake ya Aya:

[وَإِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ]

Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. [Al-Mu’minun: 52], “[وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أمَّةً] Na kwa yakini huu Umma wenuyaani, jamii yenu – Enyi Mitume - jamii [وَاحِدَةً ] “Moja” Wanaafikiana katika Dini moja, na Mola wenu Mlezi ni Mmoja. [فَاتَّقُونِ] “Basi niogopeni Mimi pekee” Kwa kutii amri Zangu na kuepuka makatazo yangu. Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume, kwani wao wanafuata mfano wao na wanafuata nyayo zao. Anasema (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ]

Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu. [Al-Baqarah: 172]. Kwa hivyo, ni wajibu kwa wale wote wanaojinasibisha na Mitume na wengineo kufuata hili na kutenda ipasavyo.”

Tunapozungumzia kuhusu Waislamu, ni lazima tuwaregelee kama Ummah wa Kiislamu (taifa), kwani ni kundi lililounganishwa na Uislamu, fikra, fahamu, na hisia zake zikiwa taifa moja; taifa bora lililotolewa kwa ajili ya wanadamu, likiwalingania mema, yaani, Uislamu, hivyo kuwatoa gizani na kuwaingiza kwenye nuru, na kuwaokoa kutokana na taabu ya dunia hii na mateso ya Akhera. Ummah wa Kiislamu ndio taifa bora zaidi ambalo Mwenyezi Mungu (swt) alilituma ili liwe na sifa ya uongozi na mamlaka, likifanya kazi ya kuondoa sababu za ufisadi duniani kwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Al-Bukhari amesimulia kutoka kwa Abu Hurairah, ambaye alisema: كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ] Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu [Aal-i-Imran: 110], yaani wao ni watu bora kwa wengine, kwamba mnawafunga minyororo shingoni mwao hadi waingie katika Uislamu?”

Mwenyezi Mungu (swt) ameupamba Ummah wa Kiislamu kwa fungamano lisilovunjika: fungamano la Aqida (itikadi). Fungamano hili limewafanya kuwa taifa lenye nguvu, linaloogopwa na mataifa mengine, na linalotofautishwa kwa udugu unaotawala miongoni mwa watu wake, likiwafunga pamoja ili washirikiane, wasaidiane, na waonyeshe huruma... Wao ni mwili mmoja; endapo sehemu moja itaumia, mwili mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa. «مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ، وَتَرَاحُمِهِمْ، وَتَعَاطُفِهِمْ، مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى» “Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuoneana upole kwao ni kama mfano wa mwili mmoja. Pindi kiungo kimojawapo kinapoumia, mwili wote huitikia kwa kukosa usingizi na homa.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema ukweli katika maelezo yake na maneno yake kuhusu Ummah wake.

Licha ya mfarakano, mgawanyiko, udhaifu, na udhalilifu ambayo Ummah wa Kiislamu unapata, mshikamano wa mwili wake mmoja katika kujibu malalamiko ya mmoja wa wanachama wake hapa au pale unaonyeshwa katika dua na machozi ya Waislamu kwa mateso ya ndugu zao huko Gaza, Syria, Sudan, Turkestan, Kashmir, na nchi zengine za Kiislamu ... licha ya uwezo wao mdogo wa kuwanusuru kutokana na mipaka hiyo na ushirikiano wa watawala wao wanaouzuia Ummah kuinuka na kuasi ili kuvunja minyororo na kujikomboa kutoka kwa ukoloni.

Katika vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu, Kafiri Magharibi ilikuwa na uhakika wa kushindwa kwake katika kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Ummah wa Kiislamu ulioungana, ukiwa umefungwa na bendera moja na dola moja inayotawala nchi zote za Kiislamu. Kwa hivyo, iliamua mkakati wa “gawanya utawale”, ikifanya kazi ya kuivunja dola kwa msaada wa wasaliti kutoka ndani ya Ummah wa Kiislamu. Ili kuimarisha mshiko wake kwa Waislamu na kumshinda adui wake hodari, iligawanya dola ya Kiislamu iliyoungana katika vijidola vingi vidogo, ikiweka kibaraka wake mkuu wa kila moja kulinda mipaka, kutekeleza vikwazo, na kusambaza fahamu na thaqafa yake ya Kimagharibi miongoni mwa Waislamu. Adui huyu alifanikiwa katika kudhoofisha Waislamu kila mahali, akitumia silaha zake zote za kinguvu na kiakili kuvunja umoja wao na kuwalisha fikra zenye sumu kama vile “utaifa” na “uzalendo,” akibadilisha fahamu ya “Ummah” (taifa la Kiislamu) ili kuuvunja mwili huu mmoja.

Huu ndio ugonjwa ulioupata Ummah wa Uislamu, ambao maadui walikuwa wakiuogopa kwa sababu ya nguvu na izza yake... Lilikuwa taifa lililoshikamana na Dini yake, likafuata mwongozo wa Kitabu cha Mola wake Mlezi na Sunnah ya Mtume wake (saw), na kueneza kheri miongoni mwa watu. Kisha likasibiwa na udhalilifu baada ya kupotoka kutoka kwenye mwongozo huu na kufuata Magharibi na sheria zake, ambazo ilizilazimisha juu yake kwa chuma na moto (nguvu), na kueneza fahamu zake zenye sumu miongoni mwao baada ya kuvunja dola ya Kiislamu, “ngome isiyoweza kuingiliwa.”

Ummah (taifa) ukawa dhaifu, hatarini, na kukiukwa, watu wake wakiteseka kwa taabu, dhulma, na giza. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فِلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعاً]

Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. [Fatir: 10].

Umar ibn al-Khattab alifafanua njia ya kweli ya heshima, akisema, “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu ametupa izza kwa Uislamu. Tukitafuta izza kupitia kitu chengine chochote kisicho chake, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.” Kwa hivyo, kwa Waislamu kuwa umma mmoja unaoongoza ulimwengu na kueneza kheri miongoni mwa watu ni faradhi ya Shariah juu yao. Umoja si chaguo bali ni amri ya mungu na ya Quran, na kuuacha ni kutotii amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]

Hakika Waumini ni ndugu [Al-Hujurat:10].

Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alisema: “Hakika, mafungamano ya kikazi hukatwa, na baraka hukutana na kutoshukuru, na pindi Mwenyezi Mungu anapoziunganisha nyoyo, hakuna kinachoweza kuzitenganisha.” Kisha akasoma aya hii:

[لَوْ أَنْفَقْتَ مَا فِي الأَرْضِ جميعاً مَا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبـِهِمْ ولـٰـكِنَّ اللهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ]

Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao [Al-Anfal: 63].

Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha Waislamu wasifarakane, kwani ndani yake yamo maangamivu yao na hasara ya Umma wao.

[وَلاَ تَنَازَعُوْا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيْحُكُمْ]

“…wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. [Al-Anfal: 46].

Ili Ummah wa Kiislamu uweze kudhihirisha sifa ya kuwa na kheri uliopewa na Mwenyezi Mungu (swt), na kumtii na kumwamini Mola wake Mlezi, lazima uwe na umoja, ukifuata njia ya Mtume wake (saw) na Maswahaba zake (Mwenyezi Mungu awe radhi nao), katika kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) Duniani. Lazima uwe ummah mmoja, ukimwabudu Mola wake mmoja, ukiinua bendera yake moja, na kumtii kiongozi wake mmoja anayeutawala kulingana na sheria adilifu ya Mwenyezi Mungu (swt). Hapo ndipo utakapopata nguvu tena na kupata mwamko wake.

Umoja wa Waislamu ni sharti linalowekwa na uhalisia, ambao kamwe haujawahi kuwa, na hautakuwa sahihi kamwe isipokuwa chini ya chombo chenye nguvu ambacho kimewakilisha Ummah wa Kiislamu katika historia yote: Dola ya Khilafah. Maisha kamwe hayajawahi kuwa, na hayatakuwa, matamu kweli isipokuwa chini ya utawala wake, kwani ni ndani yake tu ndipo sheria adilifu za Mwenyezi Mungu (swt) zitatekelezwa, na ni ndani yake pekee ndipo watu wake wataishi kwa amani na heshima.

Hivi ndivyo ulivyokuwa Umma wa Kiislamu, na hivi ndivyo kipenzi chake Mtume Muhammad (saw) alivyouacha: Umma unaoongoza na wenye kutawala, na lazima urudi katika hali hiyo... Ni umma wa mwisho duniani na umma wa kwanza kuingia Peponi, kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «نَحْنُ الْآخِرُونَ الْأَوَّلُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَنَحْنُ أَوَّلُ مَنْ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ» “Sisi tulio wa mwisho tutakuwa wa kwanza Siku ya Kiyama, na tutakuwa wa kwanza kuingia Peponi ...”

Na Mwenyezi Mungu (swt) akaujaalia kwa fadhila zake uombezi wa Mtume (saw) Siku ya Kiyama. Kutoka kwa Abu Juma’ah, amesema: Tulikula pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na Abu Ubaidah bin al-Jarrah alikuwa pamoja nasi. Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, kuna aliye bora kuliko sisi? Sisi tulisilimu pamoja nawe na tukapigana pamoja nawe. Akasema: «نَعَمْ قَوْمٌ يَكُونُونَ مِنْ بَعْدِكُمْ يُؤْمِنُونَ بِي وَلَمْ يَرَوْنِي» “Ndio watakuja watu baada yenu wataniamini, ijapokuwa hawajaniona.”

Ni heshima ya kutosha kwa Umma wa Kiislamu kwamba ni Umma wa Muhammad (saw), Umma wa “Hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu,” taifa ambalo lazima lithaminiwe, liheshimiwe, na kuthaminiwa. Lazima lijitahidi kuiga na kuregesha sifa hizi ili liweze tena kustahili kuongoza ulimwengu kwenye kheri na mamlaka juu yake, kwa sababu ya heshima ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliyolipa kupitia “Dini ya Uislamu.”

Ni wadhifa wa juu sana muliyoupata, ewe Umma wa Kiislamu! Unawezaje basi kuacha heshima hii na cheo hiki cha juu? Imam al-Shafi'i alisema, “Mtu mwenye busara si yule anayesitasita kati ya mema na maovu lakini mtu mwenye busara ni yule anayechagua mema.” Alimaanisha kwamba mtu mwenye busara huchagua mema tangu mwanzo na hayapuuzi, kwani kupuuza mema humfanya mtu kuwa katika hatari ya kupotea au kujuta baadaye.

Umma wa Kiislamu ndio bora zaidi kati ya mataifa—wenye busara, wenye fikra, na wanaotafakari uumbaji wa Mwenyezi Mungu (swt). Umeongozwa kwa Mola wake Mlezi na umemwamini Yeye, Kitabu Chake, na sheria Zake. Basi unawezaje kuacha kheri hii ambayo Mtume wake (saw) ameukabidhi kuiwasilisha kwa mataifa mengine, ukiwaangazia njia yao, ukiwaongoza kwenye njia ya haki, na kuwatoa gizani?

Zaidi ya hayo, sisi—wana wa Ummah huu—tutakutana vipi na Mwenyezi Mungu (swt) wakati tumemuahidi kwamba hatutamwabudu yeyote ila Yeye na kwamba hakuna kitu isipokuwa Dini Yake na sheria Yake kitakachotawala dunia na vyote vilivyomo ndani yake?

[وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا بَلَىٰ شَهِدْنَا أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَٰذَا غَافِلِينَ]

Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo. [Al-A’raf: 172].

Enyi Ummah wa Kiislamu: Tunashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wetu Mlezi, hakuna mungu ila Yeye, na kwamba Yeye ndiye Muumba wetu, Mtengenezaji wetu, na Mtoaji wetu... Anatupa uhai na kutufanya tufe, na atatufufua ili tuweze kukutana Naye na kupata Pepo Yake, ambayo Aliwaahidi waja Wake waumini, waongofu, na wenye ikhlasi. Ushuhuda wetu huu lazima utekelezwe ili tuweze kuwa wakweli kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Yeye atatimiza ahadi Yake kwetu.

Hali ya Waislamu leo ​​ni ya uchungu na ya kusikitisha, lakini njia ya kuibadilisha iko wazi na dhahiri.

Ummah lazima urudi kwenye chimbuko la izza na heshima yake: chombo cha kisiasa kilichoungana kinachoutawala kulingana na sheria ya Mola wake Mlezi, kinacholingania hukmu Zake, na kuinua bendera ya Dini Yake, hivyo kuthibitisha ukweli wa Muumba wake. Lazima uungane chini ya kivuli cha dola moja inayotawaliwa na Kiongozi mmoja anayemcha Mwenyezi Mungu (swt) na mkweli kwake, akifanya kazi ya kueneza Dini Yake na kuinua neno Lake hadi liwe juu na neno la makafiri lishushwe chini, hadi hukmu iwe ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Ummah lazima uwatie moyo wanawe kuvunja mipaka, kuvunja minyororo, na kujikomboa kutokana na mshiko wa ukoloni.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba tuweze kuwa miongoni mwa wale wanaofanya kazi ili kufikia izza hii, na tunamwomba Yeye, Aliyetukuka, kwamba tuweze kuwa miongoni mwa wale wanaojitahidi kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili, ambayo itaregesha izza na hadhi ya Ummah, ikiuwezesha kupata tena sifa yake ya kuwa mwema iliyoutofautisha na kuuinua juu ya mataifa mengine. Ewe Mwenyezi Mungu (swt), waunganishe watu wake, waondolee kutoka kwao yote yanayosababisha mgawanyiko, na uwaongoze kurudi kwenye Dini Yako, ambayo umeichagua, kwa njia nzuri.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeina As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu