- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuyumbayumba kwa Dola Kuu za Kiulimwengu na Kuanguka Kwake kuliko Karibia
(Imetafsiriwa)
Taswira ya China Kimataifa
China inaonyesha kuwa dunia hivi sasa ni yenye sehemu mbili na hali hiyo ni nzuri kwa dunia, na kuwa China ni bora kuliko Amerika katika upande wa sera za kiuchumi. Inafanya miamala na kila aina ya tawala, ima uwe wa kidikteta, wa kiimla, nk. China ipo tayari kufanya biashara na yeyote, haki za binadamu sio tatizo kwao. China inahitaji nishati na rasilimali kwa ajili ya kuinuka kwake, na upande wa pili inapeleka ukuaji wa miundombinu kwa nchi wateja wake. Mradi muhimu wa China kwa dunia ni ule Mpango wa Ukanda na Barabara (Belt and Road Initiative/BRI). Ni njia ya kiuchumi inayounganisha sehemu moja ya dunia na sehemu ya pili kupitia barabara, reli na njia za bahari. Maeneo ya Asia ya Kati, Asia ya Kusini na Mashariki ya Kati yote yataunganishwa kwa BRI na China. Hii ndio picha ambayo Wachina wameileta kwa dunia na Amerika inashughulishwa kwa kiasi fulani kwa kuona mataifa ya Mashariki yakikua kiviwanda, kiuchumi na teknolojia. China na Amerika zinakabiliana baina yao kimya kimya katika maeneo mengi ya dunia ikiwemo Afrika na Asia ya Kati. China inaamini kuwa mpango wa kisiasa wa Dunia uliobuniwa na Amerika na washirika wake haufanyi kazi kwa wengi duniani, na China inaelekea kutaka kuibadilisha na kuleta mpango wa dunia kwa kuwepo mataifa mengi yenye nguvu duniani, ambapo kutakuwa na uzani wa nguvu.
Je, kuna tofauti baina ya ubepari wa Amerika na ubepari wa China?
Kama tunavyoona kuwa ubepari wa Amerika una baadhi ya msingi wa itikadi, unaoegemea juu ya maadili ya usekula lakini kwa upande wa China hali ni tofauti. China haitetei itikadi yoyote duniani, inajali zaidi biashara. China inaelekea kuwa kama ni nchi ya kikomunisti lakini sio hivyo. Hakuna tafsiri maalum ya ubepari ya China kwa sababu uongozi wa China upo tayari kufanya kazi na muundo wowote wa kiuchumi ikizingatiwa kuwa ukomunisti umeshindwa vibaya na China ikaelekea kwenye ubepari ili iendelee kiuchumi. Wachina wanajiona kuwa ni wenye hadhara ya zamani waliobeba ukomunisti, ambao haukuleta mafanikio, hivyo wakaamua kuchukua urasilimali. Amerika inajaribu kupambana vita vya kiitikadi na kuiambia dunia isikubali utawala wa kimabavu wa China bali waiamini demokrasia ya Amerika na kile kiitwacho uhuru. Lakini kinyume na haya tunamuona Trump, kuwa ni kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia zaidi katika dunia, nidhamu ya demokrasia ya Amerika ni ya kidikteta katika maeneo mengi kuliko ya China. Lakini katika taswira ya China, tunaona uchumi wa China ni mdogo kuliko wa Finland lakini hivi sasa tunauona upo sawa na Amerika. Amerika ambayo watu wa dunia huiangalia, mfumo wake wa kisiasa umejaa vurugu, kama tulivyoshuhudia kwa uwazi hali ya Amerika baada ya tukio la Capitol Hill. Kuna watu walio madarakani Amerika ambao wameishika demokrasia ili kuhifadhi maoni yao na uhakikisho wao binafsi. Tunashuhudia sura halisi ya demokrasia hii iliyoundwa na binadamu ambayo inatekwa nyara siku baada ya siku na watu ambao watapiga kura tu ilimradi malengo yao ya kisiasa na kirasilimali yatimizwe na serikali husika. Imani kwa Amerika na mfumo wake unaojisifia imepotea kwa watu wa dunia. “Ndoto ya Amerika” haichukuliki au haiwezekani tena kwa dunia takriban kwenye kila nyanja, iwe katika uchumi, mahitaji ya mwanadamu na jamii imara. Ndio tunaona hakuna yeyote anayetaka kuwa kama Amerika.
Je, ombwe hili linazibwa na China na mandhari ya miji yake mizuri?
Ni uchumi wake wa kiviwanda? Au maendeleo yake ya teknolojia. Tunaona Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou, nk. ni miji ilioendelea sana lakini hali halisi ni tafauti, tunapokwenda maili 200 hadi 300 ndani ya China, wengi ya Wachina wanaishi maeneo ya vijijini. Watu wa Hong Kong hawajioni kuwa ni watu wa China bara, pia Taiwan ni jimbo lililo asi la China. Hivyo kuna masuala nyeti ya ndani nchini China. Lakini picha wanayoileta mbele ya dunia ni ya kuwa nchi kubwa yenye nguvu iliyoshikamana, lakini ukweli uko mbali nao. Tumeshuhudia maandamano ya umma China dhidi ya sera za COVID na ukandamizaji na mauwaji ya kimbari ya Waislam wa Uyghur.
Kwa kukosekana utulivu wote huu je, China inaweza kuwa dola kuu duniani?
Je, inaweza kuwa katika nafasi ya kuitawala dunia? Tunaona kuwa China ni dola kubwa ya kiuchumi tu na sio zaidi ya hapo. Ili China iwe nchi kuu duniani inahitaji kuwa na mfumo wa kilimwengu. Badala ya kuwa na mfumo, China ina ubaguzi tu ambao inautoa na ambao unadhihirishwa wazi na matendo yake dhidi ya Waislamu wa Uyghur hivi leo na dhidi ya Watibet miongo kadhaa nyuma. Kwa kuwa China sio dola ya kimfumo basi imekuwa ni kitisho cha kieneo tu kwa Amerika. Kihistoria China haijatanua mipaka yake katika miaka 4000 ya historia yake. China haina makoloni yoyote kihistoria wala kambi za kijeshi katika nchi za kigeni. Wachina hawaamini kuwa desturi na maadili yao kuwa ya kilimwengu, bali ni ya kwao, ya kipekee kwa watu wao. Hivyo tunaona kuwa mbali ya uchumi na teknolojia, China haielekei kuwa na ndoto yoyote ya utawala wa dunia. China inaelekea kuchukua nafasi ya IMF na kujenga benki yao AIIB (Asian Infrastructure Investment Bank) lakini ukweli ni kuwa China ina idadi kubwa ya watu zaidi ya bilioni 1.4 kuwalisha. Kwa kiasi hicho kikubwa China inahitaji nishati na rasilimali. Uchumi wa China kimsingi umeegemea juu ya kugeuza rasilimali kuwa bidhaa na kusafirisha nje. Kama uagizaji na uuzaji huu wa rasilimali ghafi na bidhaa ukisimama basi itakuwa ni suala kubwa kwa China, wakati Amerika inadhibiti biashara ya kimataifa na Benki ya Dunia na IMF, inaweza kwa urahisi kuisimamisha China. Ndipo tunaiona China ikitumia njia mbadala, kubuni BRI kujiingiza Afrika na Asia ya Kati ikikwepa udhibiti wa kiuchumi wa Amerika. China inataka kuepuka mashaka na Amerika na washirika wake, ndipo tunaona katika vita vya Ukraine, China haipo moja kwa moja na Urusi. Amerika inajaribu kuibana mbavu Urusi, pindi hali kama hiyo ikitokea kwa China, itawezekana kabisa kuangamizwa.
Je, China na Urusi ni washirika?
Kwa kuwa msimamo wa China kwa Urusi sio imara kiasi hicho na Urusi haiwezi kuitegemea China kwenye vita vya Ukraine, vilevile China kama China itatokezea kuivamia Taiwan, utegemezi juu ya Urusi ni suala lenye shaka. Hivyo kiujumla hakuna washirika wa China pindi itapojaribu kupeleka ushawishi wake kwa majirani zake, utawala wa dunia uko mbali sana sana. Nchi kama Pakistan, Bangladesh na nchi nyengine za Afrika, zote zinataka fedha za China lakini kifikra hakuna inayosimama nayo bega kwa bega dhidi ya Amerika na Magharibi. Tumeona pia Amerika ikiunga mkono na kujenga mahusiano ya biashara na China wakati wa Vita Baridi kuigawa kambi ya Sovieti. Amerika ilikuwa moja ya washirika wazuri sana wa biashara na China wakati huo, lakini baada ya kuvunjika Umoja wa Kisovieti, China ilipuuzwa na Amerika kuwa kama nchi nyengine ya ulimwengu wa tatu ambayo kutumika kwake kumekuwa na manufaa kwa wakati huo tu. China imeendelea na kutajirika na kuwa na nguvu na hivi leo imekuwa mshindani wa kiuchumi wa Amerika. Kwa hivyo leo tunaona Amerika ili iweze kuidhibiti China jambo ambalo inaelekea kuwa ni mzozo wa baadaye, imewapatia silaha majirani wa China, kama Japan, Korea Kusini, Australia na India, nk. Pindi China ikitaka kuivamia Taiwan itabidi kufanya hivyo wakati ambao itahakikishiwa ushindi, vyenginevyo muingizo wa muda mrefu utaiangusha China. Tunaona Taiwan ipo masafa ya saa moja tu kutoka China, na kwa Amerika itahitaji kuvuka Bahari ya Pasifiki, kwa hiyo ushindi wa haraka utakuwa rahisi kwa China, lakini ushiriki mrefu zaidi huenda ukawa wa gharama kubwa zaidi kwa China kwa sababu ya kupatiwa silaha kwa majirani wa China na Amerika. Majirani wa China wakiwa nchi moja moja hawako imara kama ilivyo China, lakini kwa pamoja wanaweza kuwa tisho kubwa. Hivyo Amerika imejenga upinde wa kinga kuizunguka China pindi vita vikizuka na wameweka mawakala katika eneo. Kwa China, Taiwan ni jimbo lake lililo asi. Wachina hawataki kuipiga mabomu Taiwan ili ijisalimishe bali kugeuza rai jumla ya watu na kuiunganisha tena na China bara. Lakini upande huo wa China ni mbovu sana kama tuonavyo hali katika Hong Kong ambao ni Wachina lakini imekuwa vigumu kwa China kuchanganyika nao kiitikadi. Hivyo hivyo, Wa-taiwan ni Wachina lakini wana hali hiyo hiyo, unapokuwa kwenye masuala ya kijamii unahitaji maadili na fikra iliyo imara, ambayo China hawanayo. Hivyo tunaona nchi zikija upande wa Amerika ambayo ina uoni wa kiulimwengu kuliko China. Watu wa Hong Kong na Taiwan pia wanataka kuwa Waamerika kuliko kuwa Wachina.
Je, urasilimali umeshindwa kuiunganisha dunia?
Tunapo iangalia China, Amerika na Magharibi nchi zote hizi ni za kirasilimali. Tunaiona Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zote ni nchi za kirasilimali lakini zote hizo zimeingia vitani wao kwa wao mara kadhaa. Tunaiona Amerika mshika bendera wa Mfumo wa Urasilimali ikiwa katika mabishano na China ambao wapo sambamba na walio mstari wa mbele wa fikra hiyo hiyo, lakini tunaona mataifa yote haya yanajitambulisha yenyewe kuwa ni ya asili na Hdhara tafauti, kwa hivyo kunakuwa na tafauti kubwa baina ya mataifa yanayofuata mfumo huo wa kirasilimali. Hapa tunaona utaifa umeutangulia urasilimali kuwa ni uoni wa dunia. Ufaransa ni yenye utamaduni wa zamani zaidi ya uasisi wa Amerika, sawa pia kwa China ni taifa la zamani zaidi kuliko mfumo wa urasilimali. Tunaiona Amerika kuwa ni taifa jipya kulinganisha na ustaarabu wa mataifa mengine. Imeundwa na watu kutoka Uingereza walioanzisha koloni katika Amerika Kaskazini kwa sasa inajulikana jimbo la Virginia na hatimaye wakawa waasi na wakaanzisha makoloni kumi ya mwanzo na kuyaita ‘United States of America’.
Je, China inakabiliana na matatizo ya ndani?
Tunaiona India ikielekea kuwa taifa maarufu zaidi duniani, ambapo China kwa upande mwengine inaelekea kwenye mzozo mkubwa wa kidemografia. Rasilimali kubwa zaidi ya China ambayo ni kundi la vijana, nguvukazi rahisi zaidi duniani inaangamia. Mtindo wote wa kiuchumi wa nchi unaegemea juu ya njia hii. Kasi ya uongezekaji wa watu China imepanda kwa kiasi kidogo zaidi mnamo 2021 kwa kipindi chote cha historia yake, na katika miaka miwili ijayo idadi ya ongezeko la Wachina itaanza kupungua. Hivyo idadi isiokadirika ya wafanyikazi rahisi kwa China itafikia mwisho wake. Tatizo kubwa zaidi ni la idadi ya wazee. Asilimia 20 ya idadi ya Wachina wana umri wa zaidi ya miaka 65. Katika miaka 20 ijayo pensheni ya wazee itaongezeka kutoka asilimia 30 hadi 40 ambayo itakuwa ni mzigo mkubwa kwa uchumi wa China. Hili kwa sasa ndilo jambo muhimu kwa China, badala ya kuwa taifa kuu la dunia. China inahitaji idadi ya vijana wanaoweza kusaidia wazee. China inahitaji watumiaji kwa bidhaa zake. China haiwezi kutegemea watu wa magharibi kuwa ni soko lake linaloongoza kwa watumiaji, bali linaiangalia Afrika ambapo itahitaji mageuzi ya kisiasa kwa China kuingia. Ni katika Afrika ambapo mapambano ya kisiasa baina ya China na Magharibi huenda yakaonekana.
Je, Kunaweza Kutokea Uasi Amerika?
Amerika imejiingiza katika vita vikubwa viwili na Iraq na Afghanistan ambapo inahisiwa vimeisha kwa miezi kadhaa lakini imechukua miaka mingi na vimekuwa vita vyenye kurefuka vilivyokausha rasilimali za Amerika na uchumi kwa kiasi kikubwa. Viongozi wa Amerika kwa sababu ya vita hivi, walipuuza masuala ya ndani na Amerika kwa jumla, hivyo nchi ipo katika hali ya kusimama kwa upande wa mageuzi ya kijamii na kiuchumi. Kuibuka kwa Donald Trump ni dalili ya kushindwa kisiasa na kuibuka kwa mgawanyiko mkali katika Amerika. Texas imekuwa suala nyeti katika mandhari ya siasa ya kijiografia inataka kujitawala wakati viongozi wameidharau Amerika. Amerika ina bahari mbili za kujikinga kutoka vikosi vya nje, ni mgawanyiko wa ndani tu utalivunja taifa la Amerika kama ilivyotamkwa na Abraham Lincoln. Majenerali wa jeshi wastaafu wanne walinukuliwa wakisema, kama Donald Trump hatoshinda uchaguzi ujao, jeshi huenda likafanya mapinduzi. Wanaamini hali iliopelekea Vita vya wenyewe kwa wenyewe (1861-1865) ni hii hapa leo.
Ripoti ya machafuko ya Capitol Hill inaeleza kuwa wanajeshi walikuwa ni sehemu ya machafuko yaliyopangwa kuikalia Ikulu ya Amerika. Watu katika jeshi walikataa kukubali kuwa Joe Biden alishinda uchaguzi na kwamba zilitumika hila. Tunaona mchezo wa kisiasa wa Amerika ukienea katika ‘makoloni’ yake, kama Saudi Arabia. Mohammed bin Salman (MBS) alifanya maamuzi ya kupunguza uzalishaji wa mafuta ili kuwasaidia Wana Republican nchini Amerika waweze kushinda. Tunaona ubinafsi wazi wa wanasiasa wa Amerika wakifanya dhidi ya wanasiasa wenzao kwa kutumia watawala wa kigeni. Wanasiasa wengi wanatayarishwa kufanya kila kinachowezekana ili kubakia katika utawala. Inaelekea kama historia inajirudia yenyewe kwani mambo haya haya yalitokea wakati wa Himaya ya Roma kabla ya kuvunjika kwake, ambapo wanasiasa walianza kufanya mambo ya kuwanufaisha katika kiwango cha kibinafsi. Wanasiasa wahafidhina mambo leo kati ya 10 na 11 ndio waliofanya maamuzi ya kuingia vitani Iraq ambapo walidhani vita vitamalizika ndani ya miezi kadhaa. Donald Trump aliwaaminisha nusu ya watu wa Amerika kuwa nchi inaendeshwa na kundi la siri la watu wachache. Aliwaambia watu kile walichotaka kusikia na kuwaghilibu watu wa Amerika wampigie kura. Aliahidi mabadiliko lakini kumbe alihitaji tu kubakia madarakani. Tunaona jeshi la Amerka likikataa kutumika dhidi ya harakati ya (BLM) Maisha ya Mtu Mweusi Yanathamani.
Hitimisho Muhimu
Kama matatizo ya ndani ya Amerika yanaongezeka kiasi hiki, masuala ya nje hayatokuwa kipaumbele kikuu kwa uongozi wa Amerika. Kama kutatokea chochote katika ulimwengu wa Kiislamu katika hatua hiyo hakitokuwa tena kipaumbele kwa Amerika. Kama Mapinduzi ya Waarabu ya Pili yatatokea, Al-Sisi akiondolewa madarakani Misri, Pakistan zikikumbwa na mapinduzi ya kijeshi, au Asia ya Kati ikishuhudia mapinduzi ya Kiislamu, Amerika haitokuwa katika wasaa wa kujiingiza humo.
Enyi Waislamu! Tunaiona Amerika ikiwa na masuala yake ya ndani, China ikiwa na matatizo yake makubwa ya ndani, Urusi ikiangamia katika Ukraine. Eneo pekee lenye nguvu ya kuuondoa mfumo uliopo na kuleta mapinduzi ni ulimwengu wa Kiislamu. Mfumo uliopo wa kikafiri wa kirasilimali unadhibitiwa na kulindwa na Amerika, lakini tunaiona Amerika ikishughulishwa katika masuala yake ya ndani na haitokuwa tayari kujiingiza kwenye mizozo ya nje. Nafasi pekee na muafaka kwa Waislamu imewadia ya kuleta mabadiliko yanayohitajika na dunia hii inayokufa, na kuusimamisha Uislamu. InshaAllah tutaona kwa macho yetu wenyewe utimishwaji wa ahadi ya Mtume (saw): Tamim al-Dari (ra) ameeleza: nilimsikia Mtume (saw) akisema,
«ليَبْلغنَّ هذا الأمرُ ما بلغ الليلُ والنهارُ، ولا يترك اللهُ بيت مَدَر ولا وَبَر إلا أدخله الله هذا الدين، بعِزِّ عزيز أو بذُلِّ ذليل، عزا يُعِزُّ الله به الإسلام، وذُلا يُذل الله به الكفر»
“Jambo hili (Uislamu) litafikia kila pale ambapo usiku na mchana vinafikia. Na Mwenyezi Mungu hatoacha nyumba au makaazi isipokuwa ataiingiza Dini hii humo, ambapo mtukufu atatukuzwa na dhalili atadhalilika. Mwenyezi Mungu atamtukuza mtukufu kwa Uislamu wake, na atamfedhehesha dhalili kwa ukafiri wake.”
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeeshan Akhtar
Marejeo:
- The Muslim World Between China & US | Adnan Khan | ISLAMIC OASIS LIVE #56
- https://www.bbc.com/news/world-asia-china-49317695
- https://www.bbc.com/news/world-asia-china-59900139
https://www.theguardian.com/us-news/2022/jan/09/is-the-us-really-heading-for-a-second-civil-war