Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafunzo Kutoka Historia ya Balkan: Uislamu Huleta Amani na Usalama – Utaifa Huleta Mauwaji na Uharibifu

Licha ya udogo wake wa eneo, katika kipindi chote cha historia yake eneo la Balkan lilikuwa ni medani ya mivutano, vita vya kikatili, na uhamaji wa kimakundi. Huenda ikawa hakukua na eneo jengine duniani kama hili ambalo limekuwa ni la matukio ya kihistoria, sehemu ya kuibuka na kutoweka kwa mataifa mengi na ya aina tofauti, makabila, jamii na himaya. Ardhi hizo na watu wake, ambao hawakushuhudia chochote isipokuwa umwagaji damu, unyonyaji na kutokuwa na usalama kwa karne nyingi, hatimaye wamekuja kuonja ustawi, amani na maendeleo kwa takriban miaka 600 kupitia kuingia kwa Uislamu.

Muundo wa kipekee wa Kiislamu wa kuunganisha (wanaadamu) umejenga picha ilio hai yenye rangi, ilio changamfu ya lugha tofauti, makabila, jamii na dini. Lakini watu wa Balkan waliporudia tena kwenye utaifa na kuwacha mtindo wa maisha ya Kiislamu, waliangukia kwenye, kubaguana, ukabila, kampeni za uoanishwaji, na kuendea katika machinjio ya vita vya umwagaji damu na mauwaji ya kimbari. Vita vya Bosnia na hasa mauwaji ya kimbari ya Srebrenica miaka 25 iliopita hayakuwa ya kwanza baada ya kuanguka kwa Dola ya Khilafah. Hata kwa mtazamo wa haraka haraka tunagundua hasara na maumivu ambayo sisi kama Ummah wa Kiislamu tumekumbana nayo: uoanishwaji kwa nguvu, kufukuzwa na kuuliwa kwa wingi kwa Waislamu wa Kibulgaria walio wachache kutoka 1944 hadi 1989, na uangamizaji wa kikabila mwaka wa 1989… Mauwaji ya kikabila na uhamishwaji kwa nguvu wa maelfu ya Waalbania wa Cham kutokea sehemu za Ugiriki ya eneo la Epirus ya mashariki kuelekea Albania mwaka 1944-45… Yale yanayoitwa Damu ya Krisimasi mwaka wa 1963, ambapo raia Waislamu 364 wasio na silaha, wanawake na watoto, waliuliwa nchini Cyprus…

Hii ni mifano michache tu ya maafa tuliokumbana nayo… Pamoja na kuwa historia ya Balkan inatoa mafunzo kwetu, lakini pia ni habari ya mafanikio ya utekelezaji wa nidhamu ya utawala ya Kiislamu… Kwa hivi sasa eneo la Balkan linajulikana kuwa ni eneo linalojumuisha Bosnia-Herzegovina, Croatia, Serbia, Kosovo, Slovenia, Albania, Macedonia, Montenegro, Bulgaria, Romania, Ugiriki na Thrace.

Ukombozi wa mwanzo kwenye Balkan ulianza kupitia majeshi ya Sultani Orhan I, aliye ongoza Khilafah ya Abbasiya mwaka wa 1352 wakati vikosi vyake vilipodhibiti ngome ya Tzympe (Cimpe) nchini Bulgaria. Kutokea hapo na kuendelea, kutoka 1352 hadi katikati ya karne ya 16, Balkan ikawa chini ya Uislamu kupitia mikono ya Utawala wa Uthmaniya. Hata hivyo, Balkan haikukombolewa kupitia upanga kama wengi wanavyodai. Majeshi ya Uthmaniya ya Dola ya Khilafah yalipigana dhidi ya watawala wa kienyeji na makruseda wa Kanisa Katoliki, bali ukombozi kwa watu wa eneo uliwezeshwa kupitia “Sera ya Istimalet” na sio kupitia mapambano.  Ni kutokana na Sera hii ya Istimalet ndipo Wabalkan walionja utulivu wa kweli, amani na usalama kipindi chote cha historia. Na ilikuwa Sera hii ya Istimalet ambapo mamilioni ya watu, hadi makabila yote, yameweza kuukubali Uislamu kwa hiyari katika karne zilizo fuata.

Maana ya msamiati wa “Istimalet” ni “chenye kufurahisha, kuvutia, kushinda mioyo”. Kwa mujibu wa taratibu za Utawala wa Uthmaniya neno hilo lilitumika kwa maana ya “kuwasimamia watu na hasa raia wasio Waislamu, kuonyesha uvumilivu maalum na upole katika kushughulika nao”. Misingi muhimu ya Sera ya Uthmaniya ya Istimalet ni kuwatendea wema, ulinzi wa watu wa maeneo yaliokombolewa, kuhifadhi maisha yao na mali dhidi ya maadui, kuwapatia uhuru katika masuala yao ya kidini, kuwapatia unafuu katika masuala ya kodi. Sera hii kwa hakika ni utekelezaji wa kauli ya Quran ya “Muallafat Qulub وَٱلْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ katika Sura At-Tawba 60, inayo maanisha “kuzileta nyoyo pamoja (kwenye Uislamu)”… Ufunguzi wa ardhi za Balkan zaidi ulifanikishwa kupitia sera hii ya upendo ya kuwahifadhi Wakristo wenyeji, kuwahakikishia haki zao, kuwapatia uhuru katika imani zao za kidini, na hata kuwasamehe kodi… Ikiwa ni matokeo ya kimaumbile kwa raia wasiokuwa Waislamu kuwa waliwazingatia Wauthmani kuwa ni waokozi wao. Hivyo sera ya istimalet ilikuwa ni katika jambo muhimu lililousaidia Uislamu katika kuupata na kuudhibiti utawala kwa Wabalkan kwa karne nyingi.

Moja ya sifa muhimu za historia ya Bosnia ni kuwa, chini ya utawala wa Kiislamu, sehemu kubwa ya watu wake walichagua kuingia katika Uislamu. Pia mapambano baina ya imani tofauti za Wakristo yalifikia mwisho chini ya Utawala wa Kiislamu. Zaidi ya hayo, hata moja ya dhehebu la Kikristo lenye misimamo mikali la Bogomils, liliingia katika Uislamu, na kuunda jamii ya Waislamu ya kabila la Slavic pamoja na lugha ya Kiserbia na Kikroashia.

Kumbu kumbu za kihistoria zinathibitisha kuwa watu wasio Waturuki na wasio Waislamu katika Balkan waliishi katika kipindi cha amani zaidi na uhuru na wepesi zaidi wakiwa chini ya utawala wa Kiislamu. Ikielezea sura bora zaidi ya mfumo wa Dola ya Kiuthmani kuwa ulikuwa ni wa muelekeo wa “uvumilivu kwa raia wake”; Mwana historia wa Kifaransa Robert Mantran ameelezea katika kitabu chake, Historia ya Utawala wa Uthmaniya: “Hasa katika vitongoji vya Wakristo, lugha za kigeni, dini na hata matabaka ya kisiasa na kijamii yalihifadhiwa; makubaliano yalifanyika pamoja na makanisa na viongozi wa dini, yakiwapatia hata unafuu wa kodi. Pamoja nayo kukomesha mizozano/mapigano miongoni mwa Wakristo katika eneo, hasa uvumilivu wa Dola ya Uthmaniya na muelekeo kwa wana jamii wa Bogomolism, uliweka misingi ambayo waumini wa dini hii hatimaye waliweza kusilimu. Hakukuwepo kabisa kwa jaribio la kusimilisha watu wa maeneo ambapo waliweza kuwa na utawala, wala kufuata sera ya Kuwafanya Waturuki au kuwasilimisha kwa nguvu. Kama isingekuwa hivyo, isingewezekana kuelezea namna ambavyo watu wa Ugiriki, Bulgaria, Serbia na lugha nyenginezo, madhehebu ya Kikristo na watu wa asili waliweza kubakisha utamaduni wao hadi hivi leo.”

Mtangazaji wa Kimagharibi amedokeza kuwa “ki-Slavic” huenda ilikuwa ni lugha ya tatu rasmi katika Dola ya Uthmani mwaka wa 1595. Familia mashuhuri ya Kibosnia, Sokollu ni familia mashuhuri ya jamii asili ya Kiserbia. Wana familia wenye kutajika wa familia hizi, kama Grand Vizier Sokollu Mehmed Pasha, Ferhad Pasha Sokolovic, walikuwa ni maafisa wa juu wa dola katika Utawala wa Uthmaniya kipindi cha karne ya 16. Katika karne ya 16 na 17 dola ya Uthmaniya ilikuwa na Waziri Mkuu 8 wa Kibosnia.

Wanapogusia juu ya mafanikio ya Uislamu, wanahistoria mara nyingi hutilia mkazo muundo wa nguzo za Dola ya Uthmaniya.

Mwanahistoria wa Kibulgaria Maria Todorova, kwa mfano, amesema katika kitabu chake Ifikirie Balkan: “Kuna mambo mengi yaliyo changia mafanikio ya Uthmani katika kusimamisha amani na utulivu nchini Balkan. Zaidi ya hayo, dola ya Uthmaniya imekuwa na muundo wa nguzo ulio imara. Muundo huu imara ulihisiwa katika kila eneo la uwepo wa Uthmani. Muundo huu haukuwa wa kidhulma, kinyume chake ulifuata msingi wa uvumilivu na huruma. Kwa hivyo dola ya Uthmaniya muda wote iliheshimu maadili ya wenyeji na wakati wote ikimzingatia mwanaadamu kuwa ni mwenye thamani.”

Jambo lililounda na kuruhusu utekelezaji kamilifu wa sera hii ya uvumilivu ni muundo wa dola uliojengwa juu ya Quran na Sunnah. Ilikuwa ni uaminifu na kujifunga na Quran na Sunnah iliyoiwezesha Khilafah ya Uthmaniya kuitawala kwa wepesi Balkan kwa takriban miaka 600. Katika Uislamu, mioyo inakombolewa kupitia siasa. Na ili kuondoa vizuizi vyovyote ambavyo vinazuia ukombozi huu, Uislamu umeamrisha Jihad. Hivyo majeshi ya Waislamu yalipata ushindi mnono katika Vita vya Mwanzo vya Kosovo mwaka 1389, Kampeni ya Varna mwaka 1444, Vita vya Pili vya Kosovo mwaka 1448 na ushindi mwengine usio na idadi dhidi ya makruseda. Na kila moja ya (ushindi huu) umeganda ndani ya kumbu kumbu ya ulimwengu, na yameimarisha utawala wa Uislamu katika Balkan. Ilikuwa Jihad hizi zilizo wazuia Wamagharibi kuweza kuwapelekea msaada Constantinopoli na hivyo kufungulia njia za ufunguzi. Wakristo wa Ulaya hawakusahau na hawatosahau kushindwa huku kukubwa hadi mwisho wa ulimwengu. Na chuki hii iliyoganda katika mioyo na akili za Makafiri wa Kiserbia kutokana na kushindwa huku ndio sababu ya Vita vya Bosnia na Mauwaji ya Srebrenica.

Hata hivyo, kuanguka kifikra na kimfumo kwa Khilafah ya Uthmaniya katika karne za 17-18 ilipelekea kuzorota kimfumo iliosababisha kukosekana kwa utulivu kijamii na kiuchumi. Sambamba na hili, Vita vya Vienna mwaka wa 1683 vilimalizika kwa kushindwa jeshi la Uthmaniya, na iliashiria kipindi muhimu katika vita baina ya Uislamu na makruseda. Kushindwa huku kulihamasisha maadui.  Katika mwaka wa 1699 tayari Dola ya Uthmaniya ilijikuta ikilazimishwa kufunga Mkataba wa Karlowitz. Kusainiwa mkataba huu na Muungano Mtakatifu (Holy League) wa 1684, muungano wa Himaya Takatifu ya Waroma, Jumuiya ya Madola ya Polish-Lithuania, Jamhuri ya Venice, na Urusi, uliiengua Hungary kwenye Ufalme wa Hubsburg. Mkataba huu ulizingatiwa kuwa ni mwanzo wa kipindi cha kuanguka kwake.

Ama kwa makruseda … Kwao njia ilikuwa safi na wazi. Waislamu walikuwa katika hali ya kushindwa kutokana na fikra ovu zenye sumu. Hivyo waliunda muundo rahisi: Kueneza utaifa miongoni mwa Wakristo wachache, Kushajiisha shinikizo dhidi ya dola ya Uthmaniya, kisha kuingia katika utendaji na kushinikiza dola ya Uthmaniya katika mageuzi, ambapo iliwapatia haki zaidi wachache. Mageuzi haya yaliweza mwanzoni kupelekea uhuru wa kisiasa na hatimaye harakati za uhuru.

Muundo huu uliweza kufanya kazi…

Kwa mfano: Matatizo ya kilimo nchini Bosnia, ambayo yametokea kutokana na mipango isiofaa na isio endana na Uislamu katika mahusiano baina ya wamiliki wa ardhi na wakulima, yalikuwa ni miongoni mwa masuala  yaliyo wepesisha kuzalisha mbegu za kitaifa miongoni mwa watu wa Bosnia. Tatizo hili baadaye lilitatuliwa kupitia uingiliaji wa kanuni ya Khalifah (Khalifah’s Kanunname) mwaka wa 1859. Hata hivyo, kabila la Waserbia ambao walikuwa bado hawakuridhika na mapatano ilipelekea machafuko kadhaa ya wakulima dhidi ya Utawala wa Uthmaniya. Hasa Machafuko ya Herzegovina mwaka 1875 yalihamasishwa zaidi kisiasa na kupelekea uingiliaji wa mataifa ya kigeni. Hivyo Mkataba wa Berlin katika wa 1878, Bosnia na Herzegovina ziliwekwa chini ya Austria-Hungary. Licha ya upinzani wa Waislamu wa Bosnia, Austria-Hungary imeiangamiza Bosnia 1878. Hivyo utawala wa Uthmaniya kwa Bosnia-Herzegovina ulimalizika rasmi, ikatambuliwa rasmi kuwa Bosnia-Herzegovina kuwa ni himaya ya Austria-Hungary katika mwaka wa 1908.

Kwa msaada wa Wamagharibi, jamii zaidi za wasio Waislamu chini ya ulinzi wa Khilafah ya Uthmaniya zilianza kuasi, zikishutumu ukandamizaji wa dola, kutokuamiliwa kwa usawa, na kudai haki mpya. Hatimaye kutoka 1839 hadi 1876, Dola ya Uthmaniya ilianzisha mageuzi ya Tanzimat yakiwa pamoja na mageuzi mengine. Mageuzi haya yaliwapa raia wa dola wasio Waislamu haki mpya, za usawa kama Waislamu, kuwa maafisa serikalini, kuajiriwa kwenye shule za kijeshi, kodi sawa na Waislamu na kuondoa Jizyah.

Kama ilivyo pangwa, kufuatia mageuzi haya Wamagharibi walitilia nguvu harakati za uhuru. Hatimaye mwaka wa 1832, Ugiriki ilitambuliwa kuwa ni dola huru, 1859 Moldavia na Wallachia walijitangazia wenyewe uhuru wa Umoja wa Himaya za Warumania. Kufuatia Vita vya Urusi-Uturuki katika 1877-78, Mkataba wa Berlin uliyavua maeneo mengi ya Uthmaniya. Kwa msaada wa Urusi, ambayo lengo lake lilikuwa kuanzisha umoja wa Slavia kote katika Balkan, hatimaye Serbia ilijitangazia uhuru wake katika mwaka wa 1878, ikifuatiwa na Bulgaria katika 1908. Mwaka wa 1908 ilikuwa pia ni kuvunjika kwa Bosnia-Herzegovina kupitia Austria-Hungary kwa mkataba ulioidhinishwa wa Berlin. Vita vya Balkan vilivyo anza 1912, vilifuatiwa na Kongamano la London mwaka wa 1921, mamlaka ya Dola ya Khilafah na utawala dhidi ya Balkan ulifikia mwisho.

Kutokea hapo, kwa mara nyengine Balkan iliregea kwenye ukandamizaji wa kikabaila wa kabla ya karne ya 14. Wabalkani kwa mara nyengine walitishwa kwenye vita vya kimaslahi baina ya himaya na falme… Kuanzia hapo na kuendelea walishuhudia dhulma chini ya ukabila, upingaji dini, ujamaa, ukomunisti na mifumo mengine ya wanaadamu ya dola za kitaifa… Watu wa Balkan kwa mara nyengine wameporwa ardhi yao, lugha, dini, maisha, mali na heshima. Dhulma ya Ukomunisti na mauwaji katika Romania, Yugoslavia, Czechoslovakia, Bulgaria yamewakumba watu wa dini zote na mataifa. Sambamba na Waislamu, pia Mayahudi, Wakristo na waumini wengine katika Balkan walikumbwa na mauwaji ya halaiki, kuhamishwa, kunyanyaswa, kuteswa na kufungwa chini ya mifumo tofauti tofauti. Baada ya kumalizwa kwa uongozi wenye kuunganisha wa Uislamu, hakuna fikra nyengine, utawala, au shirika la kimataifa au taasisi, ilioweza tena kuleta amani, umoja, mshikamano, hifadhi, usalama, maendeleo na ustawi kwa watu wa Balkan. Kinyume chake, ilipokuwa mwishoni mwa karne ya 20, wakati wa kipindi ambapo Wamagharibi wakijigamba kuwa wapo katika kiwango cha juu cha ustaarabu, na kujitangaza kuwa wao ni walinzi wa wanaadamu, haki za wanawake na watoto, na walezi wa uhuru wa imani na dini, ambapo moja ya mauwaji maovu zaidi katika historia ya mwanaadamu yalitokea… Yalitokea katikati ya Ulaya.    

Ndio, sisi Waislamu tumepitia na tunaendelea kushuhudia ukatili wote huu… Lakini, kama ilivyotajwa mwanzoni mwa Makala haya: Historia ya Balkan ni somo kubwa kwetu. Pamoja na uzoefu katika mafunzo haya, tunamiliki wahyi kwa Mtume (saw). Wale waliojifunga na wahyi huu wameonja mafanikio katika muda wote wa historia.

Uislamu haumlazimishi yeyote kuwa Muislamu. Uislamu haumzingatii yeyote kuwa juu au chini kutokana na kabila lake, asili yake, au utajiri. Ahadi ya Uislamu na matumaini kwa wanaadamu ni ya uwazi na uhakika: Kwanza; furaha katika maisha ya dunia kwa kila mtu anayetaka hifadhi chini ya kivuli cha mfumo wa Kiislamu… Pili; kuibeba furaha ya maisha kuelekea kwenye furaha isio na mwisho katika maisha ya Akhera kupitia kuukumbatia Uislamu kwa hiyari na kujengwa juu ya dalili za kiakili… Hizi sio ofa na ahadi za Waislamu. Hapana, ni ahadi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema za Mtume wake (saw). Mwenyezi Mungu (swt) havunji Ahadi Yake, na ahadi za Mtume (saw) zinaendelea kuja moja baada ya moja…

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Zehra Malik

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

#Srebrenica25YearsOn                #Srebrenitsa25Yıl

#SrebrenicaMiaka25Baadaye         سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 14 Julai 2020 13:18

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu