Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1443 | 2021/12/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Teknolojia Mpya ya Kijani ndio Suluhisho la Mgogoro wa Mazingira, au Wembe ni Ule Ule?

(Imetafsiriwa)

Wakati Rais wa Amerika Joe Biden alipokuwa kwenye kampeni mnamo 2020, alisema, "Mabadiliko ya hali ya hewa ndio tishio lililopo kwa wanadamu. Ikiwa hayataangaliwa, yataioka sayari hii. Hii sio chuku. Ni ukweli. Na tuna wajibu wa kimaadili.” Baada ya kuchaguliwa, ameendelea kushinikiza wazo la kupanua matumizi ya teknolojia ya kijani kwa kuidhinisha Sheria yake ya 'Build Back Better', mpango wa $ 2 trilioni ambao unawekeza katika nishati safi katika sekta ya usafiri, umeme na ujenzi, kupunguza utoaji wa mafuta ya fossil na kuboresha miundombinu.

Baada ya miongo kadhaa ya kuahidiwa kwamba serikali za ulimwengu wa kwanza zitafanya kazi pamoja kupunguza utoaji wa gesi chafuzi, kuunda nishati safi, maji safi, nk, itakuwa kama Greta Thunberg alivyosema hivi majuzi, "Blah, blah, blah," zaidi, kutoka kwa viongozi wa ulimwengu wenye nguvu? Ukweli wa mambo ni kwamba mfumo wa ulimwengu uliopo sasa umeegemezwa juu ya Urasilimali na mfumo wa kirasilimali haukuundwa kufanya kazi kwa manufaa makubwa zaidi ya maisha ya mwanadamu, achilia mbali kufanya kazi ya kulinda mazingira. Urasilimali hauangalii kile ambacho ni cha manufaa kwa wanadamu na mazingira, lakini kile kinachotoa manufaa zaidi ya kifedha kwa serikali, makampuni na kwa Wakurugenzi Wakuu Watendaji na wanasiasa ambao wanalipwa kutunga sheria ambazo ni kwa maslahi yao bora.

Sera za mazingira za urasilimali zimesababisha ukosefu wa usawa wa kushangaza ulimwenguni; upande mmoja kuna matumizi ya kupindukia na ubadhirifu na upande mwingine kuna kunyimwa na unyonyaji. Matumizi ya kupita kiasi yanachochewa na kuzalisha bidhaa za bei ya chini zinazotokana na unyonyaji wa maliasili na vibarua nafuu katika ulimwengu unaoendelea. Unyonyaji unaounyenyekesha ulimwengu unaoendelea kwa mzunguko mbaya wa mizozo na machafuko. Njaa, umaskini, kuhama, uharibifu wa maisha na mali yanayosababishwa na wanadamu katika ulimwengu unaoendelea ni giza tororo la mfumo wa Kirasilimali. Unaiba rasilimali kutoka kwa nchi, bila shaka, ukiwemo ulimwengu wa Kiislamu. Unawaacha watu katika umaskini hohe hahe wakiwa hawana hata punje mchele kama chakula, choo cha kibinafsi cha kutumia, maji safi ya kunywa, unatuma kiasi kikubwa cha nguo kuukuu na vitambaa kama "hisani" na kuviangusha viwanda vyao wenyewe vya nguo kwa sababu ya gharama ya chini, lakini pia unasababisha tani za taka na uchafuzi wa mazingira.

Uhalisia ulipo uwanjani haulingani na ahadi zote zilizotolewa na wanasiasa wa Kimagharibi bila kujali ni sheria na matendo gani waliyopitisha huko nyuma, au wanapanga kupitisha katika siku zijazo kwa sababu haziendani na sifa ya kimsingi ya Urasilimali; kupata faida kwa wachache kwa gharama ya wengi. Hakuna motisha kwa serikali za Magharibi kushughulikia tatizo hili la kimataifa na ni dhahiri kwa sababu hawawezi hata kulishughulikia ndani ya nchi isipokuwa kuleta suluhisho la viraka. Suluhisho la viraka ambalo linahusisha zaidi kuweka mzigo kwa mtu binafsi. Kwa mfano, nchini Amerika, wao huongeza gharama za huduma ili kufadhili mabadiliko ya miundombinu ambayo kampuni binafsi inahitaji kufanya, kuongeza kodi, kuhimiza ununuzi wa paneli za jua za gharama ya juu, kununua gari linaloendeshwa kwa umeme, kununua vifaa vinavyotumia nishati, au kuchukua usafiri wa umma, ambao kwa kweli ni wa kuchukiza kwani miundombinu ya usafiri wa umma ni duni kando na miji mikuu michache. Sasa, ikiwa mabadiliko haya hayawezi kutokea bila ya kuyaweka mabegani mwa watu wa nchi za Magharibi, yatafanya kazi vipi kwa wale wanaoishi katika ulimwengu unaoendelea? Je, paneli za jua, mitambo ya upepo, na magari ya umeme yana manufaa gani kwa watu ambao hawawezi kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na hawana usalama? Yatasaidia nini kwa dada zetu kote ulimwenguni ambao hawawezi kulisha watoto wao, au kuwapeleka shule? Je, watawasaidia nini watoto wao wanaougua magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu ya maji taka yanayomwagika ndani njia za maji safi, au kufa kwa njaa?

Mgogoro huu wa kimazingira unaweza tu kutatuliwa kupitia utabikishaji wa mfumo wa Kiislamu. Mfumo ambao hutatua matatizo kwa kuzingatia maadili ya kiroho, ya kiutu ya kimaadili na ya kimada. Kwa hivyo, kanuni ya kimada haifadhilishwi juu ya maadili mengine na hakuna yanayopuuzwa kwa faida ya mengine. Ni mfumo ambao msingi wake ni sheria zilizotolewa na Muumba wa mbingu na ardhi. Mfumo ambao utahakikisha kwamba mahitaji yote yanatimizwa bila kuweka mzigo wa kifedha mabegani mwa watu, au kusababisha uharibifu wa mazingira.

 [وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ‏]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiyaa’: 107]

#أزمة_البيئة     #EnvironmentalCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu