Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utekelezaji wa Sharia Hatua kwa Hatua sio Njia ya Mabadiliko ya Kweli 

 (Imetafsiriwa)

Wazo la utekelezaji wa hatua kwa hatua wa hukmu za Mwenyezi Mungu duniani ni mojawapo ya mawazo hatari sana ambayo ni ngeni kwa Uislamu. Hakuna ushahidi wala uthibitisho kwamba Mtume (saw) aliakhirisha utabikishaji wa baadhi ya hukmu, au kwamba aliwataka Maswahaba zake (ra) kuzitekeleza hukmu na kuwaruhusu kuakhirisha nyenginezo ili waelewe kwamba kuna utekeleza wa hatua kwa hatua katika Uislamu. Kadhalika, haikupokewa kwamba Maswahaba (ra) wamefanya hivyo. Kila hukmu ya Sharia iliyoteremshwa ilitekelezwa mara moja. Uislamu ulikuwa ni mapinduzi kimsingi na ya kina katika maisha ya Waislamu.

Na ni dhahiri kutokana na ushahidi kwamba watetezi wa fikra ya utabikishaji wa hatua kwa hatua wanatumia kwamba hawafuati njia sahihi katika kufahamu, kwa sababu baada ya kusoma dalili ya Shariah, hawakuvua kwamba utabikishaji wa hatua kwa hatua unaruhusiwa, bali ni wazi kwamba waliamua kuwa fikra ya utabikishaji wa hatua kwa hatua ni muhimu na ndipo wakaanza kutafuta dalili ya kuruhusiwa kwake na kuiweka bila ya kuthibitisha kufaa kwake katika uhalisia wa suala lililodokezwa; kwa hivyo, walieneza wazo la utabikishaji wa hatua kwa hatua, ambalo lingezuia kazi ya Mashababu ambao ni watiifu kwa Uislamu, kupunguza azma yao, na kuwaweka mbali na misimamo ya ukweli. Kisha kunakuja unyenyekevu na kuridhika, kukubali uduni katika dini, na kuacha misimamo ya Shariah katika vitendo vyote vya kisiasa kiasi kwamba yeyote anayetekeleza hukmu za ukafiri kwa kisingizio cha fikra ya utabikishaji wa hatua kwa hatua anasifiwa kuwa ni misimamo mikali, na siasa kali.

Fikra ya utabikishaji wa hatua kwa hatua katika kutekeleza Uislamu kupitia kutekeleza sehemu moja na kuacha sehemu nyingine hairuhusiwi katika Shariah, na dalili ya hilo ni dalili ya kukatikiwa, kama inavyodhihirika katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

(وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’idah:49].

Mtume (saw) alikataa miito ya viongozi wa Maquraish ya kumtaka akubali hata baadhi ya hukmu za Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo makhalifa walivyofuata baada yake katika kuzitekeleza hukmu za Uislamu kwa nchi zilizofunguliwa. Utabikishaji wao wa hukmu, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, wote ulikuwa wa mara moja, bila kuakhirisha, kuchelewesha mambo au utekelezaji wa hatua kwa hatua. Hawakuwaruhusu wale waliosilimu kunywa pombe au kuzini kwa muda wa mwaka mmoja, kwa mfano, ndipo kisha baada ya hapo iwe ni haramu, lakini hukmu zote zilitekelezwa mara moja.

Na hoja ya baadhi katika fikra ya utekelezaji wa hatua kwa hatua kwamba kuharamishwa kwa pombe ilikuwa katika hatua kadhaa sio sahihi, na kuharamishwa kwake kwa njia hii kulitoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Waislamu walijitolea kwa hukmu mara tu ilipoteremshwa, hivyo hukmu ya Shariah katika kuwaepusha walevi kuswali ilifuatwa na Waislamu mara moja na hakuna hata mmoja wao aliyekaribia swala hiyo akiwa amelewa, na ilipoharamishwa kabisa, hakuna hata mmoja wao aliyeacha hatua kwa hatua, badala yake, kuacha kwao ilikuwa mara moja, kwani walimwaga mvinyo wote waliokuwa nao mikononi mwao au pamoja nao mara tu uharamu wake ulipowajia. Na Omar Ibn Al-Khattab (ra) hakusitisha adhabu ya wizi na hakuitekeleza hatua kwa hatua, bali alifanya kazi kwa mujibu wa hukmu ya Shariah kwa kutoweka adhabu ya wizi kwa wale walioiba wakati wa njaa.

Hivi sasa, Sharia nzima iko mikononi mwetu, na tunatakiwa kuitekeleza yote, na hii ni kupitia mabadiliko msingi ya kina katika nyanja zote za maisha ambayo Dola ya Kiislamu, Dola ya Khilafah (Ukhalifa) inaitabikisha. Na si kama wanavyodai watetezi wa fikra ya utekelezaji wa hatua kwa hatua kwamba haiwezekani kuzitekeleza hukmu za Uislamu zote kwa wakati mmoja, na kwa hiyo ni muhimu kuzitekeleza hukmu hizo kidogo kidogo; kwa maana nyengine ni kutekeleza hukmu za ukafiri katika baadhi ya masuala na hukmu za Uislamu kwa masuala mengine!! Watu hawa wanadai kuwa hawawezi kutabikisha Uislamu wote kwa sababu ya kutawaliwa na Magharibi na udhaifu wa nchi za Kiislamu, na kwamba kutekeleza baadhi ya hukmu ni bora kuliko kutozitekeleza kikamilifu!! Na mtawala ambaye pia anatawala katika mfumo wa ukafiri na kutabikisha baadhi ya hukmu za Shariah ima ni kafiri, dhalimu, au ni fasiki kwa mujibu wa yaliyokuja katika Qur'an Tukufu, kwani asiyehukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, haijalishi ni kiasi gani anavyojaribu kuipamba sura yake na kuwahadaa watu kwamba anafanya kazi kwa ajili ya Uislamu.

Tukiangalia baadhi ya makundi “ya wastani” ya Kiislamu ambayo baadhi yao yameingia madarakani, tutaona kwamba hayakuwa na lengo la kutawala kwa Dini ya Mwenyezi Mungu na Sheria yake, bali yaliangalia nyadhifa za maisha ya kidunia katika utawala bila kuzingatia hukmu za Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wanatekeleza demokrasia na Ukafiri wa usekula!

Nchini Sudan, kwa mfano, na kabla ya Mapinduzi ya Kiarabu, ilitajwa kuhusu utekelezwaji wa hatua kwa hatua wa Uislamu nchini Sudan, na hilo lilisifiwa na wale wanaojiita wenye msimamo wa wastani katika nchi za Kiislamu, hivi kwamba ilionekana wazi baada ya miongo kadhaa kwamba utawala wa Bashir uko mbali na Uislamu kama tawala zengine, ingawa mara zote ulikuwa unazungumzia utekelezaji wa sheria ya Kiislamu, na sisi hawa hapa tunaiona Sudan na hali yake; nchi isiyo na Sharia katika utawala wake, imegawanyika, watu wake wanateseka kutokana na umasikini ilhali ni tajiri kwa rasilimali zake zinazoporwa!

Na nchini Uturuki, ambako Chama cha Haki na Maendeleo kilivitangulia vyama vyengine vya Ikhwan al-Muslim katika nchi za Kiarabu, ambavyo wengi wanaviona kuwa ni mfano wa utawala uliopotea! Hatujui kuhusu mfano wowote wa kufuata! Usekula wa wazi na utiifu kwa Wamagharibi na Mayahudi haufichiki kwa mtu yeyote, huku wakizungumzia kufungua misikiti na kuhifadhi Quran na kuwaruhusu wanawake waliojifinika hijab kufanya kazi, na kuwahadaa wajinga kwamba wanatabikisha Uislamu, baada ya kuwatongoza kwa mtindo wa kiuchumi wa Kituruki!

Nchini Jordan, watu kama hao wenye msimamo wa wastani wanaoamini fikra ya utabikishaji wa hatua kwa hatua hawapigani kwa ajili ya Uislamu, bali kwa ajili ya kubadilisha sheria ya uchaguzi ili idadi kubwa zaidi kati yao waingie katika bunge jipya, na matakwa yao hayana thamani yoyote ya Shariah, kwani hawaweki hukmu za Shariah (au hata sehemu yake) kwenye meza ya masharti ya kisiasa au madai, wala kitu mfano wa hicho!

Ama Misri, al-Kinana walikwea kwa muda madaraka na bunge, hivi nini kilibadilishwa wakati huo kuelekea Uislamu?! Na hakuna yeyote anayesema hawakuwapa muda wa kutosha. Lengo lilikuwa ni kuwaridhisha Wamagharibi na sio kumridhisha Mwenyezi Mungu kwa kisingizio cha utabikishaji wa hatua kwa hatua, na hilo linathibitishwa na msimamo wa wakati ule kuhusu umbile la Kiyahudi, mikataba ya gesi, na kushindwa kuwanusuru watu wa Gaza isipokuwa kwa njia ya upatanishi baina yao na Mayahudi, mikopo yenye riba, na mambo mengine yaliyoharamishwa katika Uislamu. Kushajiisha kwao baadhi ya matendo na madhihirisho ya Kiislamu ya ibada hakuwatolei udhuru katika hili.

Ama kuhusu Tunisia, ina hadithi nyengine. Mbali na kutohukumu kwa Uislamu, hukmu za nususi zilizokatikiwa zilizo thubutu ndani ya Qur'an Tukufu zilikiukwa katika mfumo wa kijamii ambao ulikuwa ndio mfumo pekee ambao hukmu za Kiislamu zilitekelezwa, kama vile sheria za usawa katika mirathi baina ya wanaume na wanawake na kuharamisha ndoa za wake wengi, na kufuata kamba kupitia kutekeleza hukmu za sheria zinazotokana na mkataba muovu wa CEDAW.

Inafaa kutaja hapa kwamba wafuasi wa wazo la utekelezaji wa hatua kwa hatua wa Sharia ndio kimbilio la nchi kuu za kikafiri kuwasilisha kwa Ummah. Baada ya barakoa kuanguka kutoka kwenye nyuso za masekula, baada ya hitaji muhimu zaidi la umma kuwa ni utabikishwaji wa Uislamu. Kupitia fikra hiyo ovu, Waislamu wanahakikishiwa upya kuwa utawala umekuwa katika mikono salama inayotaka Uislamu kwa sababu mwonekano wake ni wa Kiislamu!

Kutokana na hili na mengineyo, tuna hakika na ubatili wa wazo la utabikishaji wa hatua kwa hatua na kwamba mabadiliko ya hatua kwa hatua hayatawahi kamwe kuleta mabadiliko yanayotarajiwa, na kwamba mabadiliko ya kweli yatakuwa tu kwa mabadiliko msingi, ya kina na kamili, na hili litakuwa tu kupitia Khilafah pekee inayotabikisha Uislamu kama mfumo na katiba ya maisha. Tunamuomba Mola Mlezi Mtukufu tuwe miongoni mwa mashahidi na askari wake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muslimah Ash-Shami (Um Suhaib)

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu