- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mauaji Mapya mjini Gaza: Uungwana wa Ummah Utaamshwa Lini?!
(Imetafsiriwa)
Licha ya kuongezeka kwa wito wa kusitisha vita vya Mayahudi mjini Gaza, jeshi la Mayahudi linaendelea kumwaga damu ya watu wasio na hatia katika kambi za watu waliokimbia makaazi yao huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kufanya mauaji mengine ili kuongeza rekodi yake nyeusi.
Shambulizi hili la kikatili, lililotokea mnamo 4 Julai 2025, sio la kwanza, na halitakuwa la mwisho. Jumuiya ya kimataifa, na hasa Marekani, wanajua vyema kwamba umbile la Kiyahudi halizingatii makubaliano na haliyapi uzito wowote. Lakini, Amerika, muungaji mkono mkuu wa umbile hilo nyakuzi, inaendelea kucheza dori ya mpatanishi muongo na ulaghai wa kisiasa, kumwaga machozi ya mamba na kuusambaza uvamizi huo silaha na habari ili kuendeleza mauaji yake.
Enyi Waislamu, nyinyi ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewaunganisha kupitia Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (saw) mnaamini kwamba kunyamaza kwenu kuhusu mauaji haya kutawaweka salama kutokana na kuhesabiwa? Je, munadhani damu ya watoto, vilio vya kina mama waliofiwa na machozi ya kina mama yatapita bila kuandikwa kwenye vitabu vyenu vya matendo? Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa...” [Surah An-Nisaa 75]. Na Yeye (swt) asema,
[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]
“Hakika Waumini ni ndugu” [Surah Al-Hujarat 10].
Majeshi makubwa yako wapi? ziko wapi ndege na makombora ambayo tawala za kiarabu hujivunia? Wako wapi Maulamaa ambao wametutesa kwa mazungumzo ya hekima na Dawah, ilhali hatujapata kuwaona wakichukua msimamo wowote zaidi ya kuwaunga mkono watawala wa khiyana?! Wafanyibiashara na matajiri wako wapi? Je, wametoa mhanga chochote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) kama wanavyojitolea kulinda mali na mamlaka?!
Heshima ya Ummah ingali hai katika nyoyo za waliokombolewa, lakini ushindi kamili hautapatikana isipokuwa kwa kitendo cha Ummah mzima. Kwa kuyakusanya majeshi yake nchini Misri, Uturuki, Pakistan na kwengineko, Ummah utabomoa viti vya uhaini na uhalalishaji mahusiano vilivyoiuza Palestina sokoni, kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, ambayo itauunganisha Ummah kama kitu kimoja na kuupeleka Uislamu ulimwenguni kote kupitia Da’wah na jihad, kumfurusha mvamizi, na kukata mkono wa mvamizi huyo.
Suluhisho halipo katika makongamano au mipango, bali katika kuasisi mamlaka ya (sultan) ya Uislamu. Kila mpango wa kisiasa, unaopatanishwa na Amerika au Magharibi, ni kifuniko tu cha kuendeleza uhalifu. Udhalilifu wa Umma hautaondolewa, Al-Masjid Al-Aqsa haitaregeshwa, na umwagaji damu wa watu wa Gaza na Palestina hautakoma isipokuwa kwa harakati ya Ummah yenye utambuzi, chini ya uongozi wenye utambuzi na ikhlasi unaokumbatia mradi wa Shariah ya mungu ambao haukufuru kwa ukafiri na kutokubali hatua nusu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume” (Imepokewa na Ahmad).
Enyi Umma wa Uislamu: Je, sio wakati wenu wa kuamka? Je, sio wakati wa sauti za Al-Mu’tasim na Salahuddin kusikika tena? Je, sio wakati wa nyinyi kuitakasa ardhi yenu kutokana na uchafu wa Mayahudi na vibaraka wao? Naapa kwa Mwenyezi Mungu (swt), mtaulizwa, na historia haitakuwa ni yenye kusamehe, na Mwenyezi Mungu (swt) atakuulizeni juu ya kila upungufu na kufeli.
[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ]
“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shuara 227]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Baha’ al-Husayni – Wilayah Iraq