Alhamisi, 26 Muharram 1446 | 2024/08/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukosefu wa Urasilimali wa Kuwathamini Wazee unatokana na Pesa kuwa Muhimu zaidi kuliko Thamani ya Utu

Habari:

Bi kizee mmoja wa Marekani mwenye umri wa miaka 87 alikamatwa hadharani kwa kutolipa bili ya ukusanyaji wa taka. Faini ya dolari 77 iliyokuwa haijalipwa ilizingatiwa inastahili zaidi kwa maafisa wawili kumkamata nyumbani kwake asubuhi, kumtia pingu hadharani na kumpeleka gerezani. Aliwekwa katika seli ndogo kwa siku nzima hadi kuachiliwa kwake kulipojadiliwa. Mmoja wa maafisa wa kike, aliyeathiriwa waziwazi na uzito wa kile kilichokuwa kinatokea, alikuwa na wasiwasi wa kutosha kumshauri asilie mbele ya majirani walioshuhudia tukio hilo la kusikitisha. (Live 5 News)

Maoni:

Uhalifu huu wa kinyama dhidi ya mwanamke maskini na dhaifu haikuwa kosa la kiidara. Kwa kweli ilikuwa wazi kwa watu wote kwamba “sheria” lazima itekelezwe kwa gharama zote kwa sababu gharama halisi ya kupoteza pesa ndiye “Mungu” anayehudumiwa.

Wanawake wanaoishi ndani ya utamaduni huria wa kisekula wanakabiliwa na hatma ya kubandikwa majina ya kutokuwa na maana na mzigo kwa jamii mara tu wanapokuwa hawachangii katika uchumi. Maisha yao hayana hadhi ya kuhitaji uchungaji. Wazo kwamba kufukuzia dolari chache inahitaji muamala mkali ni sifa ya kawaida katika sekta zote za jamii. Wanawake wajawazito hupoteza taaluma zao wanapotaka likizo ya uzazi. Wanawake aghlabu huchelewesha miaka yao ya kuzaa kwa kuhofia kupoteza kiuchumi. Dori yao kama kina mama na walezi haipewi ujira. Kwa hakika, wanawake hudhalilishwa na kuadhibiwa kwa sababu ya sifa zao za kike. Simulizi za usawa kwa kweli ni seli yake ya kijamii inayodhibitiwa na wanawake wanaowasaliti wanawake wa Kiislamu wanapotekeleza uhuru “wa kimakosa”.

Tunazikashifu hatua hizi mbaya na kutambua kwamba Quran na Sunnah zinathamini wanawake kama heshima ya kuthaminiwa. Katika Uislamu, wanawake wazee wana funguo za Pepo, na raha yao lazima iwe hamu kubwa. Hekima na uzoefu wao zitakuwa ni hazina kwa kizazi kijacho, na ni kwa kurudi kwa Sharia ya Kiislamu pekee ambapo wanawake wa kila imani watahisi usalama wa sheria za Muumba.

[وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ لِمَنْ أَرَادَ أَنْ يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ]

“Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada.” [Al-Baqarah, 2:233]

[الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ]

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake” [Al-Nisa, 4:34]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu