Alhamisi, 26 Muharram 1446 | 2024/08/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Siasa Zisizo na Utendaji za Marekani Zinasisitiza Ugumu wa Mamlaka ya Kisekula

(Imetafsiriwa)

Habari:

Baada ya duru mfululizo za upigaji kura kumpata mgombea wa Republican Kevin McCarthy kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, wana Republican 20 wenye msimamo mkali wamesalia kupinga azma yake. Mzozo katika Chama cha Republican umeifanya Washington kukwama na hali hiyo inabeba alama zote za mgogoro mbaya zaidi wa kikatiba kwa zaidi ya miaka mia moja. [The Guardian] Waangalizi tayari wanajadili iwapo uasi huu ni ishara ya mambo mabaya zaidi yajayo kwa siasa za Marekani.

Maoni:

Hii sio mara ya kwanza kwa chama cha Republican cha Marekani kutishia mamlaka ya GOP. Kupibuka kwa Chama cha Chai na kufuatwa na urais wa Trump yote mawili yamelijaribu azimio la chama cha Republican. Lakini pengine tukio gumu zaidi lilikuwa uasi wa Januari 6 kwenye Capitol Hill mwaka wa 2022. Hili halikufichua tu mpasuko mkubwa kati ya Republican na Democrats lakini pia lilichochea mivutano kati ya safu na faili za vyama vyote viwili.

Kwa chama cha Republican, chama cha mrengo wa kulia kinacholishwa na wahafidhina wa Kikristo kimefanya maisha kuwa magumu sana ili kudumisha umoja wa upinzani. Wanarepublican ishirini au zaidi wanaompinga McCarthy wanatoka katika Baraza la House Freedom Caucus—kundi la mrengo wa kulia zaidi wa Chama cha Republican.

Kundi hili linapinga mabadiliko ya uhamiaji na bunduki, linahubiri sera za kihafidhina za kifedha, linafuata maadili ya Kikristo, linapingana na serikali kubwa na lina uhusiano wa karibu na kampuni ya mafuta ya big oil na jumba la kiwanda cha kijeshi. Baadhi ya wafuasi wake wanaunga mkono imani ya QAnon, wanapinga vikali ndoa za jinsia moja na ni wafuasi waaminifu wa Trump.

Waasi hawa wanaamini kwamba McCarthy hana nguvu za kutosha kukabiliana na utawala wa Biden na wanahofia kwamba atawapa Wanademokrasia faida isiyo ya haki kuelekea uchaguzi mkuu wa 2024. McCarthy amefanya makubaliano kadhaa ili kuwaweka sawa waasi wa mrengo wa kulia, lakini mvutano huo umesababisha kusimama kwa mchakato wa kutunga sheria, na hii inaathiri sana biashara ya serikali.

Chama cha Kidemokrasia pia kinakabiliwa na mrengo wake mkali wa kushoto ambao unaendeshwa na ajenda ya uyakinifu chini ya kivuli cha baada ya usasa. Mamlaka ya Chama cha Kidemokrasia inaendelea kukubaliana na maswala yaliyosalia zaidi kama vile LGBTQ+, siasa za utambulisho, na maadili yanayopinga dini kama vile kuunga mkono uavyaji mimba. Kundi hili lina uhusiano wa karibu na kampuni ya Silicon Valley na big tech.

Tunachoshuhudia katika siasa za Marekani hivi leo ni kwamba mamlaka (katikati) ya vyama vyote viwili mara kwa mara inalegeza msimamo na upande wa kulia na wa kushoto kupitisha sheria ambazo hazina uwezekano wa kudumu na zitapinduliwa pindi chama chengine kikiwa madarakani. Mapambano haya ya nguvu kati ya kulia, kushoto na mamlaka sio mapya. Ni zao la uhasama mkali kati ya dini na fikra ya mada iliyoanza Ulaya karne chache zilizopita.

Katika karne ya 17 Uingereza, kipote cha watawala walitumia wanafalsafa wa mamlaka kufanya maelewano kati ya vikosi vya kidini vinavyofanya kazi chini ya mwavuli wa makasisi na utawala wa kifalme, na nguvu za chini kwa chini za kimada zinazo wakilishwa na wanafalsafa wa kipagani. Hatimaye, maridhiano ya kihistoria yaliafikiwa katikati ya karne ya 18 na dini ikatenganishwa na mambo ya maisha haya mafupi. Hii baadaye ilijulikana sana kama usekula na inaendelea kufafanua siasa za Magharibi hadi leo.

Maridhiano yaliyobuniwa nchini Uingereza yalikusudiwa na mamlaka za Kimagharibi ili kukomesha ajenda ya kimada na kuhifadhi usawa kati ya dini katika uwanja wa kibinafsi na umbo la wastani la fikra ya mada katika maisha. Hata hivyo, watu wa kimada walihisi kulaghaiwa na maridhiano hayo, ambayo yalikubali tu ajenda yao ya kimada iliyo yeyushwa. Baadaye, watu wa kimada waliendelea na mapambano yao dhidi ya mamlaka za Magharibi kuondoa Ukristo na usekula, na kuubadilisha kwa utukufu wa fikra ya kimada katika nyanja zote za maisha.

Kwa karne nyingi, hali ya ulegevu ya Wakristo iliwawezesha watu wa kimada kupata maafikiano makubwa zaidi kutoka kwa mamlaka za Magharibi. Kiasi kwamba mamlaka hizo (katikati) zilionekana kutomuamini Mungu kwa wachunguzi wengi wa siasa za Kimagharibi.

Leo, mapambano yaya haya yanaendelea nchini Amerika, na ni kati ya Wakristo wa mrengo wa kulia wa kihafidhina na wale wa mrengo mkali wa kushoto wa baada ya enzi ya kisasa. Mamlaka ya kisekula ya GOP na Chama cha Kidemokrasia mara kwa mara wanafanya makubaliano na vikundi vyao vyenye msimamo mkali ili kudumisha Amerika ya kisekula. Uchaguzi wa McCarthy kama Spika hauna uwezekano wa kusitisha vita kama hivyo na haitachukua muda mrefu kabla ya mamlaka ya Amerika kuzidiwa na nguvu hizi. Wakristo wa mbali wa kulia na wana mada wa mrengo wa kushoto wanachukia usasa na wanatafuta kuuangusha.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu