Jumamosi, 25 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kitengo cha Wanawake “Kongamano la Kimataifa la Wanawake: Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”

Mwaka mzima umepita tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vikali vilivyofuata huko Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wa Gaza wamevumilia mitihani mikubwa, wakiishi katika machungu, mateso, na majanga yasiyohesabika: kuhamishwa, mauaji, njaa... mabaki yaliyotawanyika ya watoto na wanawake yaliyokusanywa kwenye mifuko, na mashahidi walionaswa chini ya vifusi, wasiowezekani kutolewa, na kuongeza katika maumivu na huzuni kutokana na kushindwa kuwaheshimu na kuwazika. Mauaji ya kikatili ya halaiki yanafanywa na umbile halifu kwa mtazamo kamili wa ulimwengu ambao unashiriki na kupuuza. Hata hivyo, licha ya mikasa na majonzi ya vita hivi, vimejaa mafunzo na tafakari zinazotolewa na kundi aminifu, vumilivu na thabiti linalosimama kidete dhidi ya njama za maadui na khiyana za watawala na wale wanaodai kuwa marafiki. Kundi hili dogo, bila kukatishwa tamaa na wale waliowatelekeza, linabaki stahimilivu, bila kupoteza kamwe tumaini la ushindi wa Mola wa mbingu na ardhi. Licha ya vilio, maombi, na wito wa kuomba msaada kutoka kwa watu wa Gaza, majibu yamefichua na kudhihirisha usaliti wa watawala wa Waislamu ambao wamekaa kwenye viti vyao vya utawala, viziwi, mabubu na vipofu kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile hilo halifu dhidi ya watu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Watawala hawa wamejitolea kuonyesha uaminifu na utiifu kwake, kuhalalisha mahusiano nalo, na kuimarisha uwepo wake.

Vita hivyo pia vimewafichua sura za wanazuoni wengi, na kuwafichua wakweli kutoka kwa wadanganyifu. Vimefunua pazia machoni, vikionyesha ukweli wa kile kinachotokea. Asili ya halisi ya mzozo wa Palestina imekuwa wazi: mapambano kati ya haki na batili, kati ya Waislamu wa Palestina na umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, nyakuzi, la kikafiri. Ndiyo, watu wa Palestina kwa jumla, na hasa Gaza, wameuita Ummah. Hivyo, je jibu lilikuwaje?! Lilikuwa dhaifu, likidhihirika katika maandamano machache, au kususia baadhi ya taasisi na maduka yanayounga mkono umbile hilo, au kutuma chakula na nguo kama msaada! Licha ya umbile hilo vamizi kuendelea kutekeleza uhalifu wa kivita mmoja baada ya mwingine, na licha ya maombi yote hayo yanayokaririwa, vilio vya kuomba msaada, na matukio ya kuhuzunisha, kimya cha dunia nzima, usaliti wa serikali, kimya cha Umma wa Kiislamu na majeshi yake, na ukosefu wao wa kuchukua hatua yamekuwa, na bado yangali, kama majibu yao!

Haya yote yanazua maswali kuhusu sababu za kuzuia kumalizika kwa mauaji haya ya halaiki na ukombozi wa Palestina! Je, ni suluhisho gani la msingi ambalo kwalo kadhia hii inaweza kutatuliwa milele? Maswali haya na mengine yatashughulikiwa na kujibiwa mnamo Jumamosi, Oktoba 5, 2024, wakati wa kongamano la kimataifa la wanawake la mtandaoni lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote duniani, chini ya kichwa: “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema” Kongamano hili litaainisha njia sahihi ya kutatua kadhia hii na mambo mengine yanayohusu Umma wa Kiislamu. Litaangazia nukta muhimu za kadhia ya Palestina na kutoa suluhu zinazohitajika ili kukomesha mateso ya watu wa Palestina na Waislamu kwa jumla, kwa kuzingatia kuwa ni kadhia ya Ummah mzima na sio kadhia ya kitaifa inayofungamana na mipaka bandia iliyoundwa na dola za kikoloni. Wazungumzaji kutoka Palestina, Tunisia, Syria, Lebanon, Indonesia, na Amerika watashiriki. Kongamano hili litawafichua wale wanaozuia kumalizika kwa mauaji hayo ya halaiki, kufafanua sababu za kuzuia kukombolewa Palestina kutoka kwa Mayahudi, na kujadili dori ya taasisi za kimataifa na maamuzi yao katika kula jama dhidi ya kadhia ya Palestina. Zaidi ya hayo, litazungumzia dori ovu ya vyombo vya habari katika kupotosha na kuficha ukweli, na kuionyesha kama ni kadhia ya kitaifa au ya kikabila, ili kuwapotosha Waislamu kutoka kwenye njia sahihi ambayo wanapaswa kufuata ili kuitatua kimsingi.

Kongamano hili pia litazungumzia dori ya Umma wa Kiislamu katika kufikia suluhisho hili la kimsingi, ambalo lazima litoke kwenye Aqida (itikadi yake). Litaangazia kwamba masuluhisho yaliyopandikizwa na maadui na wakoloni ni silaha tu zinazotumiwa kuupiga vita Ummah, kuupotosha kutoka kwenye njia sahihi. Masuluhisho ya kivipande na ya muda yanayopendekezwa si chochote zaidi ya njia ya kuutia ganzi Ummah, kuuzuia kuchukua dori ambayo lazima uicheze. Kongamano hilo pia litaelezea vikwazo vinavyowazuia watu kutabanni ruwaza ya Kisharia kwa ajili ya ukombozi wa Palestina, na litafafanua kwa nini majeshi yanasalia katika kambi zao, kutoitikia wito wa mara kwa mara wa kuchukua hatua.

Zaidi ya hayo, kongamano hilo litafichua juhudi zinazolenga kupanua mwanya kati ya Ummah na majeshi yake kwa kuyaonyesha majeshi hayo kuwa hayana nguvu, tiifu kwa tawala, na hayana uwezo wa kutoa nusra au ushindi. Madai na tuhma hizi zitakanushwa kwa kutoa mifano ya watu wenye ikhlasi ndani ya jeshi waliojitolea mhanga kwa ajili ya dini yao na ushindi wake, na kubainisha dori ya ufahamu na rai jumla katika kuwahamasisha watu wengi wenye ikhlasi katika majeshi kuchukua hatua.

Aidha, kongamano hilo litafichua sababu msingi zilizo nyuma ya kuweka mzigo wa kukomboa ardhi takatifu kwa watu wa Palestina pekee, huku zikificha mjadala kuhusu dori ya Umma na majeshi yake, ambayo yana vifaa vya kutosha na yako tayari.

Kongamano hilo pia litaangazia dori ya kila Muislamu katika kutatua kadhia hii, kwa kuzingatia makhsusi wanawake wa Kiislamu na hatua wanazopaswa kuchukua ili kuchangia kukomesha mauaji ya halaiki na uchinjaji unaofanywa dhidi ya watu wetu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Litasisitiza wajibu wao wa kufanya kazi pamoja na wengine wanaopigania ukombozi wake. Kongamano hilo litasisitiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi na tamkini, na kutukumbusha kwamba faraja huja baada ya dhiki, na kwamba ushindi hufuata mitihani. Litasisitiza tena utukufu wa Ummah huu, wenye uwezo wa kupata ushindi Inshallah.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba kongamano hili litaangaza njia sahihi ambayo Ummah unapaswa kuchukua ili kuregesha tena mamlaka yake, uongozi, na kufikia ukombozi wa Palestina kutoka mikononi mwa maadui na makafari. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ] 

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj:40].

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumatano, 22 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 25 Septemba 2024 M

Matangazo ya Moja kwa Moja ya Amali za Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Kuinusuru Gaza

https://iframe.dacast.com/live/c343b814-2e78-5078-f235-896b95bc27fa/75dc1b99-b211-0bb4-085f-627b8863df4f

Video ya Ualishi wa Kongamano

Mialiko ya Kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake Kuinusuru Gaza

[Mwaliko kutoka Lebanon]

Kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake

Mtandaoni chini ya kichwa Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”

Kwa kuzingatia aqida iliyoijaalia Gaza na Palestina yote kuwa jiji kuu la Waislamu na kito katika taji la Umma huu, na kuifanya kuwa mwana wa Mashariki na Magharibi yenye kushuhudia huku tukishuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, imewafanya wote kuwa watu wa kadhia hii na wenye kuulizwa kuhusu Palestina na pia watu wake, na hata zaidi. Kwa kuzingatia shahada hii tukufu, ambayo imetufanya sisi sote, bila kuzingatia makabila yetu mbalimbali, jinsia, na nchi, ndugu katika imani, na fungamano hili la pekee likawa ni lenye nguvu na la kudumu, tunapaswa kufanya nini kama Waislamu ili kuinusuru Gaza? Kama wanawake wa Kiislamu, vipi tutainusuru Gaza? Haya ndiyo tutakayoyaweka wazi na kuyafafanua katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir duniani. Tunakualikeni kutoka Lebanon kufuatilia shughuli za kongamano hili chini ya kichwa Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema” siku ya Jumamosi, 5 Oktoba 2024.

Saa kumi kamili jioni, kwa saa za Madina Al-munawwara, hivyo basi fikeni kwa wakati.

Alhamisi, 23 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 26 Septemba 2024 M

Ili kuhifadhi nafasi katika ukumbi wa mikutano:

https://us06web.zoom.us/j/81685047416

Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Mapendekezo

*Maeneo ni machache kwa hivyo tafadhali jisajili mapema ili kupata nafasi yako katikahafla hii muhimu

* Kushiriki ni kwa wanawake pekee

* Hotuba za kongamano zitakuwa kwa lugha ya Kiarabu

(Kuingia katika ukumbi wa mikutano ni kuanzia saa 15:30 Alasiri kwa saa za Madina Al-Munawwara)

Wito kwa Majeshi

Kutoka kwa kina Mama, Mabinti na Dada wa Umma wa Kiislamu

ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)!

Wanawake wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanawataka watoto katika majeshi ya Kiislamu kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu katika kuwalinda Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na najisi ya umbile la Kiyahudi linaokalia kwa mabavu, na kukomboa kila shubiri ya Ardhi hii Iliyobarikiwa kutoka kwa makucha ya uvamizi huu wa kikatili.

Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M

Kusoma Taarifa ya Kitengo cha Wanawake

ambayo ilitangaza Kongamano la Kimataifa la Wanawake lenye kichwa:

“Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”

Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Mtandaoni kuhusu Palestina lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir duniani kote

Jumatano, 22 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 25 Septemba 2024 M

Bonyeza Hapa

Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha Wanawake

Barua ya Wazi

Kwa kina Mama wa Watu wenye Nguvu katika majeshi ya Kiislamu, Wake zao, Dada zao na Binti zao

Jumamosi, 18 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 21 Septemba 2024 M

Bonyeza Hapa

Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha Wanawake

Ujumbe wa wazi kutoka kwa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

kwa Majeshi ya Waislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M

Bonyeza Hapa

Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha wanawake

Barua ya wazi kwa Watu wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu

Kutoka kwa kina Mama, Dada na Mabinti wa Umma wa Kiislamu ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M

Bonyeza Hapa

Alama Ishara za Kongamano

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Bonyeza Kufuatilia kwa Lugha Nyenginezo

Mabango, picha na vitu kutoka katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu