Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Amerika:

Amali Zilizo Ratibiwa wakati wa Kampeni ya Kiulimwengu, “Ukombozi wa Kontantinopoli Bishara Njema Ikatimia… Ikifuatiwa na Bishara Njema!”

Chini ya muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir ilizindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio la Kumbukumbu ya Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli #Konstantinopoli (mji wa Hirakila) ambao ulizungukwa kuanzia mnamo 26 Rabii’ al-Awwal mpaka 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na tarehe 5 Aprili mpaka 29 Mei 1453 M na hivyo bishara njema ya Hadith tukufu ya Mtume (saw) ikapatikana:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِير ُأَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Kwa yakini Mtaifungua Konstantinopoli, Amir bora ni Amir wake, na Jeshi bora ni jeshi hilo.”

Hizb ut Tahrir / Amerika imezindua amali zake katika kampeni hii ya kiulimwengu. .Sifa njema zote anastahiki Mwenyezi Mungu (swt).

Ijumaa, 20, Jumada al Awwal 1441 H - 15 Januari, 2020 M

Katika kumbukumbu ya Ukombozi wa Kostantinopoli

Hizb ut Tahrir / Amerika Imefanya Kongamano lake kwa Anwani: “Msaada wa Mwenyezi Mungu Upo Karibu”

24 Jumada al-Awwal 1441 H  -  19 Januari 2020 M

Kama sehemu ya kampeni ya kiulimwengu iliyo zinduliwa na Hizb ut Tahrir, chini ya muongozo wa Amir wa Hizb ut Tahrir Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu (swt) amuhifadhi, “Ukombozi wa Kostantinopoli Bishara njema ikatimia …ikifuatiwa na Bishara”

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu ikiadhimisha tukio la Kumbukumbu Hijiria ya Ukombozi wa Konstantinopoli #Konstantinopoli (mji wa Hirakila) ambao ulizungukwa kuanzia 26 ya Rabii’ al-Awwal mpaka tarehe 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M.

Kongamano lilianza kwa aya kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuanzia mwishoni mwa Surat Aali-Imran, kisha Dkt. Abdur Rafay akazungumzia majanga ya Waislamu kwa jumla na hususan kwa Waislamu wa India. Alionesha kwamba majanga ya Waislamu nchini India ni matokeo ya wao tu kuwa Waislamu. Alizungumzia namna India ambayo inaitwa nchi kuu ya demokrasia inaonesha watu ukweli wa uongo wa demokrasia ambayo kamwe haiwakingi watu dhidi ya unyanyasaji wa watu, hususan unyanyasaji dhidi ya Waislamu.

Kisha ikafuatia hotuba iliyo wasilishwa na Ustaadh Taiseer Hussein, ambaye aliongelea kuhusu Ukombozi wa Kostantinopoli, nao ulikuwa ni kutimia kwa bishara njema ya kwanza ambayo ilitimia baada ya kukombolewa Waajeni na Warumi na itafuatiwa na kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume na ukombozi wa Roma, na ukombozi wa Ardhi iliyo Barikiwa – Palestina. Ndugu Taiseer alisisita kwamba bishara njema hizi hazimaanishi kwamba tukae chini na kusubiri, bali kutulingania na kutuhimiza kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Khilafah.

Kisha ukawadia muda wa maswali na majibu, kisha Kongamano likahitimishwa kwa dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) ushindi na nusra, na kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Na Sifa Njema zote zamstahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru tovutiza Hizb ut Tahrir / Amerika:

Ukurasa Rasmi wa Hizb ut Tahrir/ Amerika
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir/ Amerika
Akaunti ya Twitter ya Hizb ut Tahrir/ Amerika
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir/ Amerika

Alama za Kampeni

#فتح_القسطنطينية

#القسطنطينية

#İstanbulunFethi

#istanbul

#ConquestofIstanbul

#Constantinople

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 25 Juni 2020 09:37

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu