Jumamosi, 14 Shawwal 1446 | 2025/04/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 02/04/2025 M

Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.

Kwa ajili ya mabadiliko ya kweli... kataa Demokrasia... simamisha Khilafah Rashida.

Ewe Mola turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume...  Allahumma Amina.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 04 Shawwal 1446 H sawia na 02 Aprili 2025 M

1. Ni Mwana yupi wa Khalid bin Walid (ra) Ataifikisha Himaya ya Marekani kwenye Vita vya Yarmuk Leo?

 

Mnamo tarehe 25 Machi 2025, jeshi la umbile la Kiyahudi lilijaribu kuvamia kijiji kidogo cha Koayiah nchini Syria, kaskazini mwa Mto Yarmuk. Hata hivyo, vijana wa kijiji hicho walipigana kwa ushujaa na jeshi, na kuua maadui na kufikia kifo cha kishahidi katika mwezi wa Ramadhan. Enyi Jeshi la Pakistan! Katika zama za Khilafah Rashida, Mto Yarmuk ulishuhudia jeshi la Khalid bin Walid (ra) likilisaga saga jeshi la Himaya ya Kirumi. Hivi sasa imeshuhudia kundi dogo la waumini likiwaletea maadui hasara zenye uchungu. Hivyo basi ni udhuru gani uliosalia kwa jeshi la saba kwa ukubwa ulimwenguni? Ni nani anayepaswa kuifikisha Himaya ya Marekani na washirika wake wa Kiyahudi kwenye Vita vya Yarmuk leo, ikiwa si nyinyi? Waondoleeni watawala waoga, simamisheni Khilafah Rashida na msonge!

2. Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) sio Mwokozi. Ni Chombo cha Ukoloni wa Kiuchumi

 

Mnamo tarehe 25 Machi 2025, mfuko wa Fedha wa Kimataifa ulithibitisha makubaliano mapya ya kiwango cha wafanyikazi na mamlaka za Pakistan. IMF ndiyo mlinda lango wa mikopo ya riba kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha za wakoloni. Mikopo hii ya riba sio tu ukiukaji wa wazi wa Shariah, inaiingiza Pakistan katika mtego wa deni linaloendelea kuongezeka. IMF kisha hutumia deni hilo kupata usalimishaji wa ubwana. Tumeona katika miaka iliyopita jinsi IMF ilivyoamuru kila kitu kutoka kwa bei za matumizi na ushuru hadi ubinafsishaji wa mali muhimu na ya kimkakati. Ni dhahiri kwamba Waziri Mkuu wa sasa alipaswa kutambua dori ya IMF katika maandalizi ya bajeti ya kila mwaka. Kuna njia moja tu ya ukombozi (tahrir) kutoka kwa ukoloni wa kiuchumi. Ni kuasisiwa Khilafah Rashida.

3. Vilio vya Waliodhulumiwa Lazima Vijibiwe kwa Kupazwa Takbira na Majeshi ya Waislamu kwenye Viwanja vya Vita

 

Tangu kuregelea tena vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza mnamo tarehe 18 Machi, umbile la Kiyahudi limekuwa likiwaua kwa uchache Wapalestina 103 na kuwajeruhi 223 kila siku. Ilhali, Ummah na majeshi yake bado hawajatekeleza wajibu wa Shariah wa Jihad dhidi ya jeshi linaloshambulia. Mwenyezi Mungu ﷻ ametanguliza faradhi ya Shariah kuliko iliyopendekezwa (nafilah). Imepokewa kutoka kwa Khalifa Rashid wa Kwanza, Abu Bakr al-Siddiq (ra) kwamba amesema, أن اللهَ لا يقبلُ النافلةَ حتى تؤدَّى الفريضةُ “Mwenyezi Mungu ﷻ haikubali nafilah mpaka itimizwe faradhi.” Hebu kila Muislamu na awasiliane na jamaa zake na marafiki zake katika vikosi vya jeshi na awaamuru kusimamisha Khilafah Rashida, ambayo inaukusanya Umma na majeshi yake dhidi ya maadui.

4. Wanajeshi wa Msalaba wa Marekani Wanaonyesha Uadui wao kwa Uislamu Hadharani, Ilhali Uongozi wa Kijeshi wa Pakistan Unaendelea na Kazi Yake kama Kibaraka wa Ukoloni wa Kijeshi

 

Mnamo tarehe 26 Machi 2025, Waziri wa Ulinzi wa Marekani aliwakasirisha Waislamu kote ulimwenguni baada ya kufichua tattoo ambayo haikuonekana hapo awali kwenye mkono wake wa kulia inayosomeka "كافر" (kafiri). Amerika ya Trump haifichi maumbile yake ya vita. Hata hivyo, uongozi wa kijeshi wa Pakistan unaendelea na kazi yake kama kibaraka wa ukoloni wa kijeshi. Unazuia shambulizi lolote kwa Jeshi la India huko Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Unazuia uhamasishaji wa kijeshi kuinusuru Gaza. Haufanyi chochote kumaliza vita na Waislamu nchini Afghanistan na Baluchistan. Enyi Maafisa wa Pakistan! Mtakubali hadi lini usaliti wa uongozi wenu wa kijeshi? Ukombozi wa Ummah unaanza na ukombozi (tahrir) wa majeshi yake kutoka kwa ukoloni wa kijeshi. Wang'oeni watawala hawa. Toeni Nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida. Songeni kwa ajili ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa.

5. Pongezi kwa Idd ul-Fitr. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Ayatakabali Matendo yenu Mema

 

Kila Mwaka na ukutane na Ummah wa Muhammad ﷺ kama Ummah bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu. Kila mwaka na uuone Ummah wa Muhammad ﷺ ukiamrisha yale ambayo ni maruf na kukataza yaliyo munkar. Kila mwaka na uwaone Waislamu washindi. Kila mwaka na uuone Ummah wa Muhammad (saw) ukimridhisha Mola wake Mlezi na kutekeleza Shariah Yake. Mwenyezi Mungu (swt) na atujaalie sisi na nyinyi Idd, huku chombo cha haki dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida, imeasimamishwa, na nchi za kikafiri na wapambe wa madhalimu, wawe wanyonge na madhalili kwake. Amiin, Ewe Mola ﷻ Mlezi wa wanadamu wote.

 

6. Ukombozi (Tahrir) wa Al-Masjid Al-Aqsa Huanza na Ukombozi wa Majeshi ya Waislamu

 

Siku ya Idd ul-Fitr, umbile la Kiyahudi lilianzisha mashambulizi ya anga huko Gaza. Makumi ya Waislamu waliuawa kishahidi, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Ukombozi wa Gaza unaanza na ukombozi wenu kutokana na vibaraka wa ukoloni. Msikubali kumuasi Mwenyezi Mungu ﷻ. Msikubali khiyana dhidi ya Ummah wa Muhammad ﷺ. Zirusheni rushwa za viwanja, pensheni na marupurupu kwenye nyuso za watawala duni, ambao wameuza Akhera yao kwa Dunia. Mkamateni mtawala au kamanda yeyote wa kijeshi anayekuzuieni. Mteueni Khalifa Rashid kama kiongozi wenu kwa ajili ya vita vikali. Ongozeni mafuriko ya Ummah na majeshi yake kwenye ushindi dhidi ya watesi wake. Fungueni milango ya Al-Masjid Al-Aqsa iliyokombolewa kwa mikono yenu, na mumsujudie Mola wenu Mlezi ﷻ ndani yake!

7. إِلَّا تَنفِرُوا۟ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًۭا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ﴿

Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine” [Surah at-Tawba 39]

 

Mnamo tarehe 31 Machi 2025, jeshi la Kiyahudi lilitoa maagizo makubwa ya kuwahamisha watu wa Rafah na maeneo ya karibu. Enyi majeshi ya Waislamu! Adui yenu ametangaza kuongezeka kwa vita, na bado hamujajiunga na vita, baada ya miezi kumi na nane! Songeni, jemadari wa Firauni dhalimu wa Misri, sasa yuko Motoni, pamoja na jeshi lake. Kuwatii madhalimu hautakuwa udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Yaondoleeni majeshi mizigo ya Mafirauni wa leo. Mteueni Khalifa Rashid na musonge kuinusuru Gaza. Au mnasubiri kuungana na Haman na jeshi lake? Au mnangoja kubadilishwa na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu ﷻ pekee?

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu