- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:
Maoni ya Habari 09/04/2025 M
Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.
Kwa ajili ya mabadiliko ya kweli... kataa Demokrasia... simamisha Khilafah Rashida.
Ewe Mola turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume... Allahumma Amina.
#BringBackKhilafah
Jumatano, 11 Shawwal 1446 H sawia na 09 Aprili 2025 M
1. «مَا تَرَكَ قَوْمٌ الْجِهَادَ إلاّ ذُلّوا»
“watu wataacha Jihad isipokuwa watadhalilishwa.” [Hadith Imepokewa na Imaam Ahmad]
Mnamo tarehe 1 Aprili 2025, Dola ya Kibaniani iliinua sauti na kilio juu ya ufyatuaji wa risasi kwenye Mstari wa Udhibiti (LoC) na Jeshi la Pakistan. Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Hii ndio hali ya kusikitisha ya Dola ya Kibaniani baada ya makabiliano kidogo ya risasi. Je, itakuwaje wakati Khalifa Rashid atakuongozeni kwa ukombozi wa Kashmir, kama utangulizi wa kutekwa kwa Hind? Hakika kuna heshima katika Jihad na kukata tamaa katika kuiacha. Wapiganaji wa Gaza, Syria na Afghanistan wamethibitisha ukweli huu katika zama zetu. Mtupeni kando kamanda yeyote anayekuzuieni. Mteueni Khalifa Rashid na mushiriki katika Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu ﷻ, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu ﷻ na Umma wa Kiislamu wa bilioni mbili unaowangoja mashujaa wake.
2. Enyi Majeshi ya Waislamu, Utiifu wenu ni kwa Mwenyezi Mungu ﷻ Sio Vibaraka wa Ukoloni
Mnamo tarehe 2 Aprili 2025, Waziri wa Ulinzi wa umbile la Kiyahudi alitangaza upanuzi mkubwa wa shambulizi la ardhini huko Gaza. Ni kipi kilichobakia kubebwa na Waislamu wa Gaza, na kushuhudiwa na Umma wengine wote? Njaa, kukatika kwa umeme, kunyimwa maji, kulazimishwa kuhama makaazi yao, vifaru, makombora, droni, ubakaji na mauaji ya halaiki. Enyi maafisa wa Waislamu! Utiifu wenu kwa makamanda wenu waoga hautakuokoeni. Amesema Mwenyezi Mungu, وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا * رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا “Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa!” [Surah Al-Ahzaab 33:67-68]. Wang'oeni wasaliti na musonge!
3. Ushuru wa Trump Unathibitisha Haja ya Haraka ya Uchumi Mmoja wa Waislamu Chini ya Khilafah Rashidah
Gazeti la ‘Wall Street Journal’ lilitangaza mnamo tarehe 2 Aprili 2025, “Ushuru wa Trump Unalenga Kushusha Pazia kwenye Enzi ya Utandawazi,” alipotangaza ushuru wa 29% kwa Pakistan. Pakistan sasa itateseka kwa sababu ya sera ya kikoloni ya uchumi unaoendeshwa na mauzo ya nje. Kukwepa kwetu pekee ni kupitia kuunganishwa kwa uchumi wa Ulimwengu wa Kiislamu chini ya Khilafah Rashida. Sisi ni Umma wa bilioni mbili. Pato la Pamoja la Taifa (GDP) ni dolari trilioni 8.7. Usawa wetu wa Pamoja wa Nguvu ya Ununuzi (PPP) ni $26.4 trilioni. Tuna akiba kubwa zaidi ya nishati na madini ulimwenguni. Tuna idadi kubwa ya watu, vijana na wenye nguvu. Sehemu inayokosekana ya mlingano huo ni uongozi wa kisiasa wa Khalifa Rashid. Swali pekee lililobakia ni je, tuko tayari kuhangaika na kujitahidi kusimamisha Dini ya Haki kama dola?
4. Kupambana na Maadui wa Nje Huhakikisha Usalama wa Ndani
Mnamo tarehe 4 Aprili 2025, kitengo cha vyombo vya habari cha jeshi la Pakistan kilitangaza, “Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuharibu amani ya Balochistan” Hata hivyo, uasi wa silaha huko Baluchistan tangu 2003 unaendelea, na hakuna mwisho. Bila kupigana na maadui wa nje, haiwezekani kuhakikisha usalama wa ndani. Kushindwa kwa washirikina katika Vita vya Badr kuliwazima wanafiki ndani ya Dola ya Kiislamu ya Madina. Kushindwa kwa umbile la Kiyahudi huko Khaybar kuliimarisha ukanda wa hatari wa kaskazini hadi ash-Sham. Baada ya kulazimisha kuondoka kwa Warumi kutoka Tabuk kupitia mkusanyiko mkubwa wa jeshi la Waislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alibomoa kwa urahisi makao makuu ya wanafiki, Masjid al-Dhirar huko Thu Awan. InshaaAllah hivi karibuni, Khilafah Rashida itapigana na Dola ya Kibaniani, umbile la Kiyahudi na Marekani.
5. Ulinganizi Lazima Uwaelekeze Watu kwenye Kambi za Jeshi na Wito wa Kuondolewa kwa Watawala
Mnamo tarehe 3 Aprili 2025, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) “ilishutumu vikali uvamizi unaoendelea na unaoongezeka wa Israel.” OIC inajisifu kama “Sauti ya Pamoja ya Ulimwengu wa Kiislamu.” Waislamu wa Gaza hawahitaji maneno. Wanahotaji vitendo vya majeshi ya Waislamu. Zaidi ya hayo, watawala wa Waislamu hutenda tu ili kuimarisha umbile la Kiyahudi. Ibn Salman anatoa mafuta na kuweka daraja la ardhini. Abdullah anaweka daraja la anga. Erdogan anatuma meli za biashara. Jenerali Sisi anatekeleza mzingiro wa kikatili wa Gaza. Jenerali Asim Munir anazuia jeshi la saba kwa ukubwa duniani. Ni wakati wa chemichemi ya Ummah na majeshi yake. Simameni enyi Umma wa Muhammad ﷺ na wana wa Khalid bin Walid (ra)! Waondoeni watawala, simamisheni Khilafah Rashida na mukomboe Al-Masjid Al-Aqsa.
6. Majeshi yanapaswa Kuitikia Ummah kwa Kuwaondoa Watawala na Kukusanyana katika Kuinusuru Gaza
Mnamo tarehe 6 Aprili 2025, Kunakili Ukandamizaji Dhidi ya Waislamu (DOAM) iliripoti, “Maandamano makubwa nchini Algeria yakitaka majeshi yao kuhamasishwa kuwakomboa watu wa Gaza, wakiimba الشعب يريد جهاد لغزة "Watu wanataka jihad kwa ajili ya Gaza.” Kama ilivyotarajiwa vyombo vya habari vya serikali vilikuwa kimya kama makaburi. Hata hivyo, wanaharakati wa mitandao ya kijamii walisambaza video za maandamano makubwa ya kutaka kuhamasishwa kwa majeshi nchini Tunisia, Algeria, Morocco, Jordan, Syria, Uturuki, Mauritania na Pakistan. Enyi majeshi ya Waislamu! Umma wa Kiislamu haujafa na hautakufa. Umetangaza kuunga mkono kikamilifu uhamasishaji wenu. Kizuizi pekee kwa matakwa ya Umma ni watawala wa Waislamu. Waondoeni na musonge ili mutembee katika nyayo za Salahudin na mupate ukombozi (tahrir) wa Al-Masjid Al-Aqsa.
7. Maandamano ni Lazima yawe katika Kambi za Kijeshi yakidai Kuhamasishwa kwa Majeshi katika Kuinusuru Gaza
Tarehe 7 Aprili 2025, Khawaja Saad Rafique, mwanachama wa chama tawala nchini Pakistan alisema, “Hatujaweza kuwa sauti kamilifu ya watu wanaodhulumiwa wa Gaza dhidi ya magaidi wa Kizayuni.” Wakati ambapo Umma umelipuka, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Waislamu uko chini ya shinikizo kubwa. Kwa hakika, Gaza haihitaji sauti madhubuti, hata wasiokuwa Waislamu wanapaza sauti zao. Wajibu wa Shariah kwa Waislamu ni zaidi ya hayo. Ni Jihad kwa majeshi yao. Hivyo, badala ya maandamano mbele ya balozi za makafiri, maandamano lazima yawe mbele ya makao makuu ya jeshi na vituo vya kijeshi. Waislamu wa kwanza wenye ujasiri wa kutosha kufanya hivyo watauongoza Ummah kwenye ukombozi (tahrir) kutoka kwa ukoloni.