Jumatano, 18 Shawwal 1446 | 2025/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Kampeni ya “Majeshi na Yaelekee Al-Aqsa”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa zaidi ya wanaume na wanawake 170,000 wa Kiislamu hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Pakistan inaandaa msururu wa amali kwa kichwa:

 “Majeshi na Yaelekee Al-Aqsa”

Ili kuyataka majeshi ya Waislamu yatimize wajibu wao wa kidini na kusonga mara moja kuwanusuru Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kuusafisha Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na Palestina yote inayokaliwa kwa mabavu kuanzia mto wake hadi bahari yake kutokana na najisi ya Mayahudi wauaji na halifu.

Ijumaa, 13 Shawwal 1446 H, sawia na 11 Aprili 2025 M

- Sehemu ya Amali za Wilayah ya Pakistan za Kuinusuru Gaza -

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Enyi Majeshi! Chagueni kati ya Watawala hawa ambao ni Watiifu kwa Trump, na Khalifa Rashid ambaye ataikomboa Gaza na Palestina nzima kupitia Nguvu za Kijeshi!

17 Shaaban 1446 H - 16 Februari 2025 M

Kwa Washiriki wa Kongamano lenye Kichwa:
"Kashmir na Palestina inayokaliwa kwa mabavu - Suluhisho ni Nini?"

6 Shaaban 1446 H - 5 Februari 2025 M

Baada ya Kutazama Tu Mauaji ya Kinyama kwa Siku 467, Watawala wa Pakistan Sasa Wanasherehekea Usitishaji Vita

18 Rajab 1446 H - 18 Januari 2025 M

Gaza ni Kadhia ya Umma na Majeshi yake, Sio Vibaraka wa Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani (US CENTCOM)

19 Jumada I 1446 H - 21 Novemba 2024 M

Vikosi vyetu vya Jeshi vimejaa Maafisa Wenye Ikhlasi, Mashujaa na Wenye uwezo.
Kutananeni na Kila Mmoja Wao Ili Kuwashajiisha Kuondoa Kila Kikwazo Kinachosimama Katika Njia ya Uhamasishaji Wao Katika Kuinusuru Gaza!

11 Jumada I 1446 H - 13 Novemba 2024 M

Imepita Mwaka Mmoja Tangu Mauaji ya Halaiki mjini Gaza Yaanze! Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Lazima Usimamisha Tena Khilafah Rashida na Kuikomboa Palestina

5 Rabi' II 1446 H - 8 Oktoba 2024 M

Umbile la Kiyahudi Lawaua Waislamu nchini Lebanon na Palestina Kwa Sababu ya Mwaka Mzima wa Kutochukua Hatua kwa Watawala wa Waislamu na Makamanda wao wa Jeshi

29 Rabi' I 1446 H - 2 Oktoba 2024 M

Marekani Yazipatia India na Umbile la Kiyahudi Silaha za Kisasa, Huku Ikiweka Vikwazo kwa Mpango wa Makombora ya Ballistiki wa Pakistan

11 Rabi' I 1446 H - 14 Septemba 2024 M

Watawala wa Pakistan wanatekeleza Ukamataji ili Kuzuia Hizb ut Tahrir Kutaka Kuhamasishwa kwa Jeshi la Pakistan Kuinusuru Gaza. Badala ya Kushambulia umbile la Kiyahudi, Watawala Wanawashambulia Waislamu

9 Dhu al-Hijjah 1445 H - 15 Juni 2024 M

Baada ya Shambulizi la Kinyama la Mabomu la Kambi za Wakimbizi mjini Rafah, Ni Dhahiri kwamba Ummah na Majeshi Yake Lazima Wawang'oe Watawala na Kusimamisha Tena Khilafah Rashida

21 Dhu al-Qa'adah 1445 H - 29 Mei 2024 M

Enyi Waislamu wa Pakistan! Waislamu Jasiri wa Gaza Wanasimama Kidete Mbele ya Umbile la Kiyahudi, Hivyo Musikate Tamaa. Washajiisheni Ndugu Zenu na Watoto Wenu katika Vikosi vya Jeshi la Pakistan Kutangaza Jihad kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina

15 Shawwal 1445 H - 24 Aprili 2024 M

Enyi Waislamu wa Pakistan na Jeshi Lao! Hakikisheni Waislamu wa Gaza Wanasherehekea Idd kama Tunavyosherehekea Sisi kwa Kutuma Askari Wenu Utashi na Uwezo

28 Ramadhan 1445 H - 7 Aprili 2024 M

Ni juu ya Majeshi ya Waislamu Kuwang'oa Watawala, Kusimamisha tena Khilafah Rashida na Kwenda Kuinusuru Gaza

21 Ramadhan 1445 H - 31 Machi 2024 M

Njaa ya Kulazimishwa ya Mamia ya Maelfu ya Waislamu huko Rafah, Gaza, ni Kwa sababu ya Utepetevu wa Maafisa wa Kijeshi na Askari, Wanaosubiri Amri Ambazo Kamwe Hazitatoka

23 Sha'aban 1445 H - 4 Machi 2024 M

- Video za Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan za Kuinusuru Gaza Hashim -

[إِلَّا تَنفِرُوا۟ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًۭا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ]

"Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." [At-Tawba: 39]

Mnamo tarehe 31 Machi 2025, jeshi la Kiyahudi lilitoa maagizo makubwa ya kuwahamisha watu wa Rafah na maeneo ya karibu. Enyi majeshi ya Waislamu! Adui yenu ametangaza kukoleza vita, na bado hamujajiunga na vita, baada ya miezi kumi na nne! Haaman, jemadari wa Firauni dhalimu wa Misri, sasa yuko Motoni, pamoja na jeshi lake. Kuwatii madhalimu si udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Wapunguzieni majeshi mizigo ya Mafirauni wa leo. Mteueni Khalifa Rashid na musonge kuinusuru Gaza. Au munasubiri kuungana na Haaman na jeshi lake? Au mnangoja kubadilishwa na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu pekee?

#Time4Khilafah

Imetolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumapili, 04 Shawwal 1446 H sawia na 02 Aprili 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Enyi Majeshi wa Waislamu! Je, Majabari katika zama za Ujahiliya ni Madhaifu katika Uislamu?!

Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Gaza na umbile la Kiyahudi, umbile hilo lilipanua mashambulizi yake ya ardhini huko Gaza mnamo 20 Machi 2025. Wakati huo huo, viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Waislamu wanashughulika kumfurahisha Farauni wa Washington, Trump, na majeshi yetu yanatumiwa katika vita vya uasi. Tunaweza kuuliza majeshi ya Waislamu: Je, si ndugu zenu Waislamu ndio walioifanya Marekani ionje kushindwa nchini Iraq na Afghanistan? Ni kipi kinakuzuieni kuwaondoa hawa viongozi wasaliti na kusonga kuwanusuru Waislamu? Tunakwambieni maneno yale yale aliyoyasema Khalifa Abu Bakr Al-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, pale alipokataa kuwa mpole katika kupigana na waasi pamoja na hali ngumu: “Je, Majabari katika zama za Ujahiliya ni madhaifu katika Uislamu?! Timizeni ahadi yenu na mahitaji ya imani yenu, na muende kuinusuru Gaza.

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumapili, 23 Ramadhan 1446 H sawia na 23 Machi 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Enyi Jeshi la Pakistan! Songeni kwa ajili ya Kuinusuru Gaza, kwa Kumtii Mwenyezi Mungu!

Televisheni ya serikali ya Pakistan ilisema mnamo 19 Machi 2025: “Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel.” Hivi ndivyo watawala wa Pakistan walivyolaani hujuma ya Mayahudi na jinai zake zinazoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza! Bila kusonga askari au kuinua silaha! Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Je, mnawafuata watawala wanaofuata sera za dola za kikoloni na kuuweka utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) nyuma ya migongo yao? Wanajifanya kana kwamba hawaegemei upande wowote huku ndugu zetu huko Palestina wakiuawa na kuangamizwa! Watawala hawa wanalinda maslahi ya dola  za kiadui huku mauaji yakifanywa dhidi ya watu wa Palestina. Utiifu wenu kwao hautakuepusheni na fedheha ya dunia na adhabu ya Akhera, na mutajuta wakati majuto hayatafaa kitu.

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Ijumaa, 21 Ramadhan 1446 H sawia na 21 Machi 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Mjini Gaza, Mashahidi 400 ndani ya Masaa 5!

Maneno yanashindwa kuelezea uhalifu huu wa kutisha katika mwezi huu mtukufu. Mayahudi wa Netanyahu na Marekani ya Trump wanawaonea watu wasio na hatia huku wakiwa wamelala, wakitumia ndege 100, zikiwemo ndege za kivita za Marekani, kulenga mahema yaliyojaa raia, kwa kisingizio kwamba wapiganaji wachache wa upinzani wapo. Waliwafuatiulia huku kukiwa na udanganyifu waliouita "usitisha mapigano"!

Ikiwa huu sio uhalifu, ni nini?! Lakini uhalifu ulio mkubwa kuliko huu ni uhalifu wa usaliti wa watawala wa Waislamu na majeshi yao! Kwa wana uwezo wa kukamata mikono ya wahalifu hawa na kuikata, lakini wamekataa.

Huu ni usaliti wa aina gani, ni ubaya wa aina gani huu, na ni aina gani ya adhabu imeandaliwa kwa ajili yao katika Moto wa Saqar? Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): "مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلاَّ خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلاَّ نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ" “Hakuna mtu atakayemtelekeza Muislamu katika hali ambayo utakatifu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika hali ambayo angependa nusra yake, na hakuna mtu atakayemnusuru Muislamu katika hali ambayo heshima yake inavunjwa na utakatifu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru katika hali ambayo angependa nusra yake.”

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumanne, 18 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 18 Machi 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Enyi, Jeshi la Pakistan! Mzamisheni Trump Firauni wa Marekani katika Bahari ya Gaza kwa Kusimamisha Khilafah!

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumanne, 11 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 11 Machi 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Ramadhan ya Mwaka Huu, ni Wakati wa Ukombozi (Tahrir) kutoka kwa Ukoloni wa Kijeshi!

Shirika la habari la Reuters liliripoti mnamo Februari 21, 2025 kwamba “Marekani imetoa dolari milioni 397 kusaidia mpango wa kijeshi katika chini ya Pakistan yenye silaha za nyuklia, huku msaidizi mmoja wa bunge akisisitiza kwamba matumizi ya F-16 ya Marekani katika operesheni za kukabiliana na ugaidi yatafuatiliwa isipokuwa dhidi ya India.” Huu ndio uhalisia wa ukoloni wa kijeshi: kuyafanya majeshi ya Waislamu kupigana wao kwa wao, huku wakiyazuia kupigana jihad dhidi ya India, umbile la Kizayuni, na majeshi ya Msalaba! Enyi  Maafisa wa Jeshi la Pakistani Je, munaweza kufikiria kwamba dola ya Kiislamu ya Madina ingeweza kutegemea silaha za Warumi au Wafursi?! Acheni kujidhalilisha! Huisheni ari ya Vita vya Badr ndani ya Ramadhan, ondoeni tawala vibaraka, na toeni Nusra yenu kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ambayo itaukomboa Ummah kutokana na utumwa.

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumatano, 05 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 05 Machi 2025 M

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Huku Mwezi wa Ramadhan, Mwezi wa Ushindi, Unapokaribia, Umma na Majeshi yake lazima Yakabiliane na Mfumo wa Kilimwengu wa Kidhalimu wa Marekani!

Kati ya tarehe 7 na 11 Februari 2025, wanajeshi kadhaa wa majini wa Kiislamu watashiriki katika zoezi la (Aman 25) jijini Karachi, Pakistan, ambayo lengo lake ni "kuamiliana kwa pamoja katika kushughulikia vitisho vya baharini." Je! ni tishio gani kubwa la baharini kwa usalama wa Waislamu kuliko Jeshi la Wanamaji la Marekani? Jeshi la Wanamaji la Marekani linashambulia Waislamu na kulisaidia umbile la Kiyahudi katika mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza. Pamoja na hayo, Jeshi la Wanamaji la Marekani limetenganishwa na ulimwengu wa Kiislamu na bahari, kwa hivyo linategemea watawala wa Waislamu, kwani watawala vibaraka wa Waislamu wanawapa Jeshi la Wanamaji la Marekani kambi za kijeshi na njia za baharini, ambayo pasi kwayo, Amerika haingeweza kushambulia Waislamu. Ramadhan ni mwezi ambao ndani yake Umma wa Kiislamu ulishinda maadui wengi wenye nguvu. Hebu Waislamu na waregeshe hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ katika mwezi wa Ramadhan, na warudishe ushindi dhidi ya maadui, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Jumatatu, 11 Sha'aban 1446 H sawia na 10 Februari 2025 M

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

 Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

 Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Twitter: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu