Jumanne, 16 Rabi' al-thani 1442 | 2020/12/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Maandamano mbele ya Baraza la Mawaziri, Kukataa Kutenganishwa Dini na Dola

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa kisimamo cha kukataa kipengee cha kutenganisha dini na dola (sekula), katika makubaliano yaliyotamatishwa baina ya Waziri Mkuu Abdullah Hamdok na Abdel Aziz Al-Hilu, mbele ya Baraza la Mawaziri, mnamo Jumatano 21 Muharram 1442 H sawia na 09/09/2020 saa nane adhuhuri. Ambapo Mashababu wa Hizb, wafuasi na wengineo walishiriki katika kisimamo hiki, na wakanyanyua mabango na vipeperushi vya wastani kwa urefu wa mamia ya mita mbele ya majengo ya baraza la mawaziri.

Idadi kadhaa ya hotuba ziliwasilishwa katika kisimamo hiki, ikiwemo:

1. Hotuba ya msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil).

2. Hotuba ya msaidizi wa msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Muhammad Jama (Abu Ayman).

3. Hotuba ya Dkt. Saad Ahmed Saad – kutoka kwa wanachuoni wa Sudan.

4. Hotuba ya Profesa Hassan Abdel Hamid – Naibu wa Mwangalizi Mkuu wa Ikhwan al-Muslimin.

Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alitoa hotuba mbele ya Baraza la Mawaziri kuhusu uhalisia wa makubaliano ya khiyana yaliyotamatishwa kati ya Hamdok na Al-Hilu, ili kutabikisha ajenda ya njama za wakoloni, kwa kuishambulia itikadi ya watu wa nchi hii kupita mipaka, na kusisitiza kwamba tutaendelea kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume maadamu bado tungali hai.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

- Video za Kisimamo -

Kisimamo cha Kupinga cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Mbele ya Baraza la Mawaziri Kukataa Usekula

Kalima ya Ustadh Ibrahim Uthman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Kalima ya Ustadh Ahmad Abakr

- Maingiliano ya Wageni -

Ustadh Hassan Abdul Hamid

Dkt. Saad Ahmad Saad

Kalima ya Ustadh Muhammad Jameh (Abu Ayman)

Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

- Maingiliano -

Rafaat Awadh - Khalid Abdullah - Al-Fatih Abdullah - Ali Abbas

Mahojiano ya Msemaji Rasmi na Msaidizi Wake

Kalima ya Ustadh Fadhlullah Ali

Kalima ya Ustadh Abdul Qadir Abdul Rahman

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 17 Septemba 2020 11:00

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu