- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Mkutano na Waandishi wa Habari “Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba inayotatua mizozo, inayoleta pamoja Makundi na Kuwaudhi Maadui”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan iliandaa mkutano na waandishi wa habari katika Taasisi ya Taiba ya Vyombo vya Habari, wenye mada: “Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba inayotatua mizozo, inayoleta pamoja Makundi na Kuwaudhi Maadui” uliohudhuriwa na makadirio ya idadi ya waandishi wa habari, wanasiasa, wanaharakati, watafiti na walio na hamu na mambo ya umma. Ukumbi wa mkutano ulijaa, na kijitabu cha rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kikagawanywa kwa wote waliohudhuria ukumbini.
Jumapili, 03 Jumada al-Awwal 1444 H - 27 Novemba 2022 M
- Ripoti ya Habari ya Mkutano na Waandishi wa Habari -
Wilayah Sudan: Hizb ut Tahrir Yafanya Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Taasisi ya Taiba ya Vyombo vya Habari, wenye Kichwa:
(Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba inayotatua mizozo, inayoyaleta Makundi pamoja, na Kuwaudhi Maadui)
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari katika taasisi ya Taiba ya Vyombo vya Habari, mnamo siku ya Jumapili tarehe 03 Jumada al-Awwal 1444 H, sawia na 11/27/2022 M saa saba mchana kwa anwani “uwasilishaji wa rasimu ya katiba inayotatu mizozo, inayoyaleta makundi pamoja, na kuwaudhi maadui”. Wanaharakati, watafiti, na wale wenye hamu na mambo ya umma walihudhuria, na kujaza ukumbi wa mkutano, na kijitabu cha rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kikagawanya kwa wote waliohudhuria ukumbini. Wazungumzaji katika mkutano huo ni:
1. Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) - Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
2. Ustadh Hatem Jaafar - Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Mwendeshaji mkutano alikuwa Muhammad Jami (Abu Ayman) - Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan.
Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) aliwasilisha mistari mipana kuhusu rasimu ya katiba iliyowasilishwa na hizb kwa ajili ya kutatua matatizo ya nchi, na miongoni mwa yaliyotajwa katika waraka wake: Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan tunawasilisha kwa kila anayejali maslahi ya nchi na wananchi rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah yenye ibara 191, ambayo ina hukmu jumla, mfumo wa serikali, mfumo wa uchumi, mfumo wa kijamii, sera ya elimu, na sera ya kigeni, na miongoni mwa yale yaliyokuja katika waraka huo: kwa sifa yetu kama Waislamu, msingi wa rasimu ya katiba, ambayo ndiyo kanuni msingi ya dola, lazima ujikite juu ya aqida ya umma; aqida tukufu ya Uislamu.
Hukmu za katiba hii zimevuliwa kwa ijtihad sahihi kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake (saw), na yale zilizoyaongoza katika ijma ya Maswahaba, na qiyas ya kisheria.
Rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah inatatua mizozo inayoendelea kwa hukmu za Wahyi Tukufu, ambapo:
a) Mamlaka ni kwa ajili ya umma, kwani ndio anaomchagua mtu miongoni mwao ambaye anakamilisha masharti ya mkataba wa Khilafah, na kumpa kiapo cha utiifu kwake kama Khalifa kwa Waislamu.
b) Waislamu wana haki ya kusimamisha vyama vya kisiasa ili kuwahisabu watawala, au kufikia madaraka kupitia umma kwa sharti viwe msingi wake ni aqida ya Kiislamu.
c) Jeshi katika Uislamu lina jukumu la kupigana jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kulinda yai la Uislamu na mipaka ya Waislamu, na halina uhusiano wowote na utawala kwa kuzingatia kuwa ni jeshi lenye silaha.
Rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah inazileta pande zote pamoja na hukmu zifuatazo:
a) Haitaruhusu ushawishi wowote wa kafiri mkoloni katika nchi yetu, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amekataza hilo na akasema: ﴿وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً﴾ “Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisaa:141]
b) Sera ya mambo ya nje katika dola ya Kiislamu imejikita katika kubeba ulinganizi wa Kiislamu, na huamiliana na dola zengine kwa mujibu wake, na kwa hiyo dola za kikoloni kivitendo kama Amerika, Uingereza na Ufaransa, na dola zinazo na ulafi katika nchi zetu kama vile Urusi zinazingatiwa kuwa dola za vita kihukmu, kwa hivyo tahadhari zote zinachukuliwa kuzihusu, na hairuhusiwi kuanzisha nao uhusiano wowote wa kidiplomasia. Pia hairuhusiwi kwa mtu binafsi, chama, kambi, au kikundi chochote kuwa na uhusiano na nchi yoyote ya kigeni hata kidogo, na uhusiano na nchi ni wa serikali pekee.
Tano: Kuregeshwa kwa maisha kamili ya Kiislamu, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo rasimu yake ya katiba inaweka mwamko wa kweli kwa msingi wa Uislamu, inawaudhi maadui, kwa sababu inachukua hatua na uongozi wa kiulimwengu kutoka kwao.
Kwa kumalizia: Tunawasilisha rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah kwa umma zima, kwa viongozi na waheshimiwa wa umma, wanasiasa na wanafikra, waisome, watabanni fikra zake, na waitabikishe na waitekeleze kivitendo, mpaka Mwenyezi Mungu atubariki kwa rehema na baraka zake. Na kwa askari walio na ikhlasi kwa aqida na umma wao, Hizb ut Tahrir inawaomba waikabidhi mamlaka ili kuiweka katiba hii na mfumo mzima wa sheria na mifumo ambayo hizb imeitabanni kutoka katika Uislamu.
Kalima ya pili ilitolewa na Ustadh Hatem Jaafar, ambaye alitoa ufafanuzi wa kisheria wa ibara za katiba, jinsi zinavyozingatia wahyi wa Mwenyezi Mungu, na uwezo wake wa kutatua shida za maisha. Pia akawahakikishia wahudhuriaji miongoni mwa wanahabari na wengineo kuwa maneno haya haiogelei kwa mtindo uliofadhiliwa na dola za kikoloni, kwani ni maneno ya kipekee na nje ya mfumo wa sanduku la kibepari, hivyo tunachowasilisha kwenu hakiingii ndani ya mfumo wa suluhu, makubaliano, na mapendeleo ambapo masuala ya utawala na siasa yananunuliwa na kuuzwa, kama hali halisi ilivyo leo. Kama zilivyo simama katiba za awali tangu 1923 M, tarehe ya kuingia kwa Kitchener nchini Sudan, na akasema zote zinatokana na katiba ya kikoloni.
Ustadh Hatem alieleza kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, na maandiko yake ya sheria ni mapana kushughulikia masuala na matukio mapya hadi Siku ya Kiyama, kwa hivyo maandiko hayo yanatoa hukmu za Sharia katika usemi wake, ufahamu wake, au mantiki yake, yaani sababu (illa) ya kisheria. Na akasema: Rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah inaweka dola ambayo msingi wake ni aqida tukufu ya Uislamu, na ujenzi wa dola unasimama juu ya mfumo wa hukmu za kisheria zilizotabanniwa na khalifa, na ili asiwadhikishe Waislamu njia pana, khalifa hatabanni katika ibada isipokuwa katika zaka na jihad ili kuunganisha neno la Waislamu. Wala hatabanni fikra yoyote inayo fungamana na aqida. Na akaeleza kuwa Khilafah haiwajumuishi wasiokuwa Waislamu katika kuutekeleza Uislamu katika masuala ya imani, ibada, chakula, mavazi, ndoa, talaka, na mirathi. Na akaashiria kuwa katiba chini ya Khilafah asili yake imeegemezwa juu ya kutokuwa na hatia ya uwajibikaji wa kiraia. Isipokuwa kwa hukmu ya mahakama. Alisisitiza kuwa mfumo wa utawala katika Uislamu ni Khilafah, ambao ni mfumo wa umoja na sio mfumo wa shirikisho. Ustadh huyo alishambulia shirikisho, kujitawala, na haki ya kujiamulia kwa ukali sana, na kusema kwamba ilikusudiwa kuisambaratisha nchi, kama ilivyotokea katika kujitenga kwa Sudan ya Kusini, na akaonyesha kwamba misingi ya mfumo wa utawala ni minne: Ubwana ni wa sheria na sio wa watu, na mamlaka ni ya umma, ikimaanisha kuwa umma ndio unaomchagua khalifa na kumteua kupitia mkataba wa utiifu. Dola ya Khilafah ina chombo cha idara chenye vyombo 13 vinavyohusika na kushughulikia mambo, kwani hakuna nafasi ya mgawo, kama inavyotokea katika ugawanyaji wizara miongoni mwa mamluki wa siasa na wabebaji silaha. Ama idara ya mahakama iliyo chini ya Khilafah ni tafauti na hali halisi, kuna mahakimu watatu: kadhi anayeamua mizozo na miamala, kadhi wa Hisba na kadhi madhaalim anayeondoa dhulma ya dola dhidi ya raia... Hakuna kinga, kwani kila mtu yuko chini ya mahakama, hata Khalifa wa Waislamu.
Katika kipindi cha maingiliano, wahudhuriaji walikuwa wapambanuzi, pamoja na ushiriki na mwingiliano. Waandishi kadhaa wa habari waliwasilisha maswali na michangio, akiwemo Ustadh Imad El-Din Musa kutoka Chama cha Wanahabari wa Kitaalamu, na maustadh: Sufyan Noreen Al-Intibaha, Gazeti la Hani Othman Al-Watan, Gazeti la Al-Rashid Ahmed Akhbar Al-Youm, na Ahmed Abkar, mwakilishi wa idhaa ya Al-Waqiyah.. na Nahla Muslim kutoka gazeti la Al-Ahram Al-Youm, na Tharwat Al-Hadi, mwanaharakati wa kisiasa... Mwanahabari na mwandishi mkongwe, Muhammad Mabrouk, alikuwepo na mshiriki mashuhuri, kama ilivyo tabia yake ya heshima, na pia idhaa ya Blue Nile, ambayo ilichapisha mahojiano ya video na Abu Khalil, na vile vile chaneli ya Al-Hilal.
Kwa kumalizia, mwendesha mkutano aliishukuru hadhira kwa kusikiliza na kushiriki, na kuwaomba wanahabari kuchangia kwa usambazaji.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah ya Sudan
Kupakua Nakala ya PDF Bonyeza Hapa
- Video za Mkutano wa Waandishi wa Habari -
Kalima ya Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Kalima ya Ustash Hatem Jaafar (Abu Awab)
Mjumbe wa Baraza la Wilayah la Hizb ut Tahrir Sudan
[Kipindi cha Maswali na Majibu]
- Angazo la Vyombo vya Habari -
- Angazo la Video la Baadhi ya Vituo vya Sudan kwa Mkutano wa Waandishi wa Habari –
Jumapili, 03 Jumada al-Awwal 1444 H sawia na 27 Novemba 2022 M
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan