Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 24/11/2022

Muendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika maeneo na mikoa tofauti tofauti ya nchi ili kujenga rai jumla yenye ufahamu juu ya hukmu za Uislamu na suluhu zake zinazohusiana na mifumo tofauti tofauti ya maisha, ambazo zinashughulikia mapigano na migogoro ya kikabila inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini...

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya mihadhara mitatu katika mji wa Gadharef. Moja ya mihadhara hiyo ulikuwa na kichwa, "Mkizozana katika jambo lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume (saw)." Mzungumzaji alionyesha jinsi kusimamisha Dola ya Khilafah kwa Njia ya Utume kutasuluhisha matatizo pamoja na kushughulikia mambo ya watu katika Uislamu, ili wawe na furaha duniani na Akhera.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Khartoum mnamo Oktoba 26, 2022, ambapo machapisho ya hizb yaliwasilishwa.

“Ugomvi wa kikabila (fitna) ni moto chini ya jivu, nani atauzima?” chini ya mada hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika vyuo vikuu waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain / Chuo cha Biashara, mnamo 29 Oktoba 2022. Ust. Al-Fateh Abdullah alizungumza kuhusu hali halisi ya mapigano ya kikabila yaliyoanzishwa upya nchini humo na hivi majuzi katika jimbo la Blue Nile. Na akadokeza kuwa moja ya sababu za mzozo huu ni mfumo wa Hawakir, ulioundwa na ukoloni ili kuusaidia kusimamia nchi na baadaye kuwa cheche ya ukabila.

Katikati ya maingiliano machangamfu, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa kalima katika vyuo vikuu mnamo Jumatatu, Oktoba 31, 2022, katika wilaya ya Musab bin Omair huko Kalakila, kusini mashariki mwa Khartoum. Kalima ya kwanza iliwasilishwa na Ust. Ibrahim Musharraf baada ya swala ya Maghrib kwa kichwa: “Demokrasia ni fikra inayogongana na Uislamu”, ambapo alieleza kuwa Uislamu ni njia iliyounganishwa ya maisha, na ubwana lazima uwe kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na utawala ni wake yeye kama Waislamu. Ama hotuba ya pili, iliwasilishwa na Ust. Al-Fateh Abdullah, baada ya swala ya Isha, chini ya mada: “Mapigano Mapya ya Kikabila... Sababu na Tiba”, ambapo alielezea uharamu wa kupigana kwa misingi ya ukabila, akinukuu maandiko ya Kiislamu.

“Uingiliaji kati wa Magharibi ni ukiukaji wa ubwana wa nchi na usalimishaji kutoka kwa watawala wa nchi” chini ya anwani hili, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika wilaya ya kaskazini ya Omdurman walitoa hotuba ya kisiasa katika soko maarufu la Omdurman, ambapo Ust. Al-Radi Muhammad alizungumza, ambapo alielezea uhalisia wa uingiliaji kati wa wajumbe wa nchi za Magharibi, iwe ni mabalozi au wajumbe, ni uingiliaji unaohusiana na uchungaji mambo ya nchi, iwe yanahusiana na uchumi, jeshi, mzozo wa kikabila, au masuala ya kisiasa kama vile Makubaliano ya Juba.

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan pia ilifanya mkao wake wa kawaida huko Al-Obeid mnamo Jumamosi, Novemba 12, 2022, chini ya kichwa: “Mapigano ya Kikabila ni Moto Chini ya Majivu, Nani wa Kuuzima?” Ust. Muhyiddin Hassan alizungumzia sababu zilizopelekea mapigano ya kikabila. Ni msuguano kati ya wakulima na wachungaji ili kupata ardhi au malisho yenye rutuba, mfumo wa Hawakir aliouleta mkoloni, maslahi katika ardhi ya dhahabu na mafuta, na uhasama wa kisiasa ambapo kabil hunyonywa ili kufikia malengo duni ya kisiasa.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain - Kitivo cha Biashara; mnamo tarehe 12 Novemba 2022 yenye kichwa: “Khilafah ndio dhamana ya mabadiliko na kung'oa ushawishi wa Kikafiri.” Mzungumzaji wa kwanza, Mhandisi Awab Yasser, alianza hotuba yake kwa kueleza uhalisia mchungu ambao watu wanaishi ndani yake nchini Sudan, na hatari halisi ambayo nchi inapitia inayo onya juu ya mgawanyiko na kuvunika kwa nchi hii. Mzungumzaji huyo alisisitiza kuwa, suluhu ya kisiasa inayoendelea hivi sasa kwa misingi ya katiba (inayodaiwa) ya Jumuiya ya Wanasheria si lolote bali ni vita dhidi ya misingi na maadili ya taifa hili la Kiislamu, na akaweka wazi kuwa mabadiliko ya kweli yamejengwa juu ya msingi wa Uislamu. Na hiyo ni kwa kupitia kutoa kiapo cha utiifu kwa mtu anayewatawala kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake (saw), khalifa wa Waislamu.

“Utabikishaji wa Umoja wa Umma wa Kiislamu”, chini ya kichwa hiki Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya mnamo Novemba 16, 2022, ambapo Ustadh Babiker Al Mahdi alielezea fiqhi ya umoja wa Umma na kukosekana kwake katika maisha ya Umma wa Kiislamu; kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kwamba fiqhi hii imeamrishwa na Uislamu. Adui alijua kuwa siri ya nguvu ya Ummah wa Kiislamu ni katika umoja wake, kwa hivyo alipanga njama na kuhadaa kwa makusudi, na kisha akaja na fikra ya utaifa kati ya Waturuki na Waarabu, ikifuatiwa na fikra ya uzalendo, ukabila na ueneo.

“Uingiliaji kati wa Magharibi katika nchi za Kiislamu... Sudan kama Mfano”, chini ya anwani hii Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika mji wa Gadharef mnamo Novemba 17, 2022, ambapo Bw. Muhammad Al-Hassan Ahmed, mjumbe wa Baraza la Wilayah, alizungumzia hali ya dharura ambayo Umma wa Kiislamu unapitia katika utawala wa Kikafiri wa Magharibi kwa maelezo madogo kabisa ya maisha yake kupitia watawala vibaraka ambao wameuza dini yao kwa ofa kutoka kwa ulimwengu, walikubali udhalilifu na kuwa chini ya amri, hivyo walilifunga minyoror taifa linalotamani ushindi na uongozi. Ambapo aligusia uingiliaji kati wa Magharibi kupitia kanuni na sheria ili kulazimisha mtazamo wao wa maisha kwa taifa ambalo Mwenyezi Mungu aliliwekea mtindo wa kipekee wa maisha ambao ni bora zaidi kuwahi kutokea.

“Khilafah Rashida ni ahadi na bishara njema ambayo viongozi wa Magharibi wanaiogopa,” chini ya mada hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu walifanya mhadhara katika Msikiti wa Dakhiliya Al-Wasat katika Chuo Kikuu cha Khartoum mnamo tarehe 20 Novemba 2022. Uongozi mkuu wa Waislamu wa kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu ni wajibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ahadi kutoka Kwake.

Mwishoni mwa muhadhara huo, mzungumzaji aliwaeleza wanafunzi ulazima wa kufanya kazi pamoja na wanaofanya kazi ili kusimamisha Khilafah Rashida, kwani ni faradhi na ahadi. Maingiliano ya wanafunzi yalikuwa ni mazuri sana, kwani walishiriki kwa maswali, michangio, na kutaka ufafanuzi ambapo mhadhiri Sheikh alijibu kwa njia ya kuvutia iliyovutia hadhira.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu