Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Angazo la Kongamano la Kiulimwengu

 “Je, Ni Katiba Gani Tunayoitaka?”
lililofanywa chini ya usimamizi wa Muungano wa Kimataifa wa Mawakili wa Kiislamu Wanaoshiriki katika Kongamano la Katiba Wanaotaka "Katiba ya Kiislamu kwa Dola ya Kiislamu" 

Kwa kuzingatia mabishano yanayoendelea kati ya vyama mbalimbali vya kisiasa nchini, kuhusu umbile la mfumo wa kisiasa nchini Tunisia na katiba inayoudhibiti, hasa baada ya matokeo ya Julai 25, Muungano wa Kimataifa wa Mawakili wa Kiislamu uliandaa kongamano la kimataifa nchini Tunisia chini ya kichwa: Je, ni katiba gani tunayoitaka?

Ambapo kongamano hilo lilionyesha ruwaza ya asili inayotokana na imani ya watu wa Tunisia na kueleza kitambulisho chao wa kistaarabu. Kundi la wasomi na viongozi wa maoni kutoka kwa mawakili, wataalam na wasomi kutoka nchi tofauti walishiriki, mnamo Jumamosi Machi 19, 2022 katika Hoteli ya Al-Mashtal Inn jijini Tunis. Kongamano hilo lilipokelewa vyema huku ukumbi wa kongamano hilo ukiwa umejaa hadhira kutoka kwa Watunisia waliofuatilia moja kwa moja shughuli za kongamano hilo katika miji zaidi ya moja ya Tunisia, na kupeperushwa moja kwa moja na Chaneli ya Runinga ya Al-Waqiyah na katika Ukurasa wa Facebook wa Muungano wa Kimataifa wa Mawakili wa Kiislamu na tovuti nyenginezo.

Huu hapa mukhtasari wa program ya kongamano hilo.

Wazungumzaji walijumuisha:

Wakili Fathi bin Mustapha Khamiri

Mwakilishi wa Muungano wa Kimataifa wa Mawakili wa Kiislamu tawi la Tunis, ambaye ni wakili nchini Tunisia, aliwakaribisha wanakongamano na wahudhuriaji, kisha akaelezea kongamano hilo katika muundo wake wa kisiasa ambapo alishutumu kuingizwa kwa watu wa Tunisia katika hali mbaya ya pande mbili inayotokana na mchakato wa sheria wa serikali. Utunzi wa kibinadamu wa katiba, na kuwanasa katika mvutano rasmi kati ya mifumo miwili: ima kurudi kwa mfumo wa bunge na katiba ya 2014 kama inavyotakiwa na wafuasi wa bunge, au kurudi kwa mfumo wa kabla ya mapinduzi, yaani kwenye mfumo wa urais na katiba sawa na katiba ya 1959 kama Rais Qais Saeed anavyotaka kuweka uhalali wake. Katiba zinahitaji kuchunguza sababu za msingi na msingi wa kifikra ambao kwao falsafa ya katiba imejengwa juu yake na udhibiti unaopelekea kupitishwa kwa ibara zake na kuchukua maoni ya wanazuoni na wataalamu wa Sharia kwa namna inayodhihirisha kitambulisho cha Kiislamu cha wananchi wa Tunisia, wakitangaza kuanza kwa kazi ya kongamano hilo.

Wakili Shiraz Al-Harabi

Bi. Shiraz Al-Harabi, alizungumza katika hotuba yake yenye kichwa: “Fahamu ya Katiba, Katiba ya Kimila, Katiba Iliyoandikwa.” Ilikuwa ni utangulizi ambao kwao masharti muhimu zaidi ambayo kazi ya mjumuiko huo ilizunguka, iliijua katiba kutoka kuwa ni hati au kitabu kinachojumuisha idadi ya vifungu na kanuni za msingi zinazofafanua muundo wa dola na mfumo wake wa utawala na sheria na kuonyesha mipaka na mamlaka ya kila madaraka na uhusiano wake na watu binafsi, pamoja na haki na wajibu wa pande zote mbili. Katika kutumia neno katiba au sheria kama maneno ya kigeni na kisha kutofautisha katiba ya Kiislamu na katiba nyinginezo. Mazungumzo yake yalionyesha kwamba katiba ya Kiislamu ina sheria za kikatiba za Kiislamu ambazo chimbuko lake ni Qur’an na Sunnah na sio kitu chengine. Ama kuhusu katiba zisizokuwa za Kiislamu, zina vifungu vilivyotungwa na mwanadamu vilivyopitishwa na bunge la katiba ambalo chimbuko lake ni mila na desturi, maamuzi ya mahakama, au maagizo ya washawishi wa ndani au wa kigeni.

Mhadhiri Muhammad Sjaiful kutoka Indonesia:

Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria, Jakarta, Indonesia, ambaye hotuba yake ilikuwa na kichwa "Umuhimu wa Utaratibu wa Kikatiba katika Kudhibiti Maisha ya Kisiasa", kupitia video kwa lugha ya Kiingereza yenye tafsiri ya hapo kwa hapo ambapo alisema licha ya kuwa katiba za nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Misri, Saudi Arabia Syria na Tunisia zinaweka masharti kuwa Uislamu ni dini ya dola au Qur'an ndiyo chimbuko la sheria, lakini kiuhalisia kifungu hiki ni sherehe ya kisiasa tu kwa watawala waanzilishi wa nchi hizo. Kisha akauliza: Je, kuwepo kwa katiba kama hiyo kunahakikisha kwamba watawala hawatawadhulumu watu wao? Hili ndilo nitakalojaribu kuwasilisha kupitia mchango huu, pamoja na kuwasilisha katiba mbadala ambayo inaweza kuhakikisha kuwa watawala wanawekewa vikwazo ili wasitende uimla kwa wananchi wao.

Wakili Qais ElBaradei:

Kisha Qais El-Baradei, wakili mjini Sfax, alitoa hotuba yenye kichwa “Je, katiba ya Aprili 26, 1861 ilikuwa katiba halisi?” Alieleza kuwa katiba ya Aprili 26, 1861 haikidhi matakwa ya fahamu ya kisheria ya katiba kwa sababu imetolewa na mamlaka isiyofurahia masharti ya uhuru na ubwana na hivyo inaweza kuzingatiwa kuwa ni upanuzi wa Ahadi ya Usalama iliyotolewa tangu Septemba 10, 1857, wakati bey huyo alipolazimishwa na nchi za kikoloni, haswa Ufaransa na Italia, kutoa katiba kwa lengo la kuiondoa Tunisia kutoka kwa mamlaka kuu jijini Istanbul na kujiandaa kuamiliana nayo kama dola huru isiyofungamana na Khilafah Uthmani, na katiba hiyo ilikuwa utangulizi wa kupitisha Mkataba wa kuanzisha koloni la Ufaransa mnamo Mei 12, 1881, kwa kudai kuamiliana na Tunisia kama dola huru inayoweza kuhitimisha mikataba ya kimataifa  yenye madhara kwa maslahi ya dola kuu.

Sheikh wa Msikiti Mkuu, Sheikh Hussein Al-Obaidi:

Kisha Sheikh wa Msikiti Mkubwa kabisa, Msikiti wa Al-Zaytoonah, Sheikh Hussein Al-Obaidi, akatoa hotuba ya kuvutia yenye kichwa “Mitazamo ya Wanazuoni wa Al-Zaytoonah kutokana na Katiba ya 1959,” ambapo Sheikh Al-Obaidi alianza hotuba yake kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya Uislamu na muongozo wa Qur'an, na kwa kueleza lengo la kuumbwa watu kuwa makhalifa wa Mwenyezi Mungu duniani, amri na sio ikramu ya kumuabudu Yeye (swt). Sheikh Hussein Al-Obaidi aliwasifu wanachuoni wema wa Ummah wenye ikhlasi walioshikamana na hazina ya kisheria ya Ummah, akiwemo mwanachuoni Sheikh Taqi Al-Din Al-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu.

Zaidi ya hayo, Sheikh Al-Obaidi alizungumzia ujanja wa Ufaransa na sababu za kuanzishwa kwa sheria za Magharibi na kutenganisha dini na dola. Alieleza kuwa, hali halisi ya maisha ya Tunisia hivi leo ni utegemezi kamili wa nchi za Magharibi na Ulaya kifedha na kiuchumi, jambo lile lile lililoiwezesha Ufaransa kuitawala Tunisia kwa jina la ulinzi baada ya nchi hiyo kuzama kwenye madeni. na lengo lake lilikuwa Msingi ni kutenganisha dini na nchi za Tunisia na kusitisha kuhukumiwa na mahakama za Sharia.

Ustadh Khabib Karbaka:

Hotuba ya Khabib Karbaka ilikuwa na mada, “Katiba ya Januari 2014 katika Mizani” ambapo alilaani ushiriki wa tabaka la kisiasa nchini Tunisia katika kuvuka mipaka na kupinga Uislamu kutengwa na mfumo wa utawala na sheria katika katiba na sheria nyinginezo, kana kwamba mapinduzi yalikuwa dhidi ya Uislamu na hukmu zake, wakati kila mtu anatambua kwamba kutokuwepo kwa Uislamu katika hali halisi ya Maisha ni maafa makubwa yaliyoleta uharibifu na uovu. Alikemea uingiliaji wa mkoloni katika kuandika rasimu na kusimamia katiba moja kwa moja au kupitia zile zinazoitwa asasi za kiraia zenye fedha zinazoshukiwa kuwa za Magharibi.

Naibu Sheikh Saeed Al-Jaziri

Hotuba ya mwakilishi na mmiliki wa kituo cha Redio cha Qur'an Tukufu, Sheikh Saeed Al-Jaziri, kwa kichwa "Waraka wa Al-Madina: Waraka wa Kwanza ya Kikatiba katika Uislamu," ambapo alizungumza juu ya Katiba ya Al-Madina iliyofafanua mahusiano, haki na majukumu, ikapanga uhusiano wa Waislamu na wengine, na akabainisha marejeo ya haya yote kwenye Kitabu na Sunnah, na jinsi Mtume (saw) alivyoweza kuwaweka washirikina na Mayahudi katika Katiba hiyo ambapo aliwadhamini Mayahudi haki zao za kufuata dini yao, na kwamba kila walichohitilafiana na Waislamu, kiliregeshwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Sheikh Al-Jaziri akaeleza jinsi katiba ya Mtume (saw) ilivyoweza kujenga taifa. Vile vile alifafanua uhalisia wa katiba chanya kwamba zinalindwa na dola za kikoloni ili nchi hizo ziweze kulinda maslahi yao, na katika muktadha huu aligusia uporaji wa mali na jinsi wawakilishi hao hawakuweza kuingia kusini mwa Tunisia, ambayo bado iko chini ya ukoloni.

Wakili Jandal Salah kutoka Palestina:

Wakili, Bw. Jandal Salah, alizungumza chini ya kichwa "Kufuta katiba zilizotungwa na mwanadamu zinazotumika katika nchi za Kiislamu," ambapo alisisitiza kwamba Waislamu ni mabwana wa sheria za wanadamu. Fikra ya katiba, ingawa wanahistoria wanajaribu kurejelea sheria za Wagiriki, Wagiriki, Hammurabi na wengineo; lakini yote yaliyotajwa na mengine si chochote zaidi ya kanuni za adhabu zisizo na ustaarabu na miondoko ya Kikaisari ambayo hayafikii kiwango cha hadhi ya kisheria katika taratibu na mada zake. Kisha akaweka bayana kwamba, wajibu wa taifa kabla ya kutafakari juu ya uandishi wa katiba yake, ni kubainisha ni kundi gani linalofaa kutekeleza jukumu hili, na kuwatenga kutokana nalo wale wote walioshindwa, waliodanganyika, na wenye ajenda, kama vile Talut alivyofanya alipowatenga waoga na wanafiki kabla ya kukabiliana na Goliath.

Wakili Osama Al Barhoumi:

Kisha wakili, Ustadh Osama Al-Barhoumi, akazungumza chini ya hotuba yenye kichwa: “Uzushi wa Kupindua Katiba katika Nchi za Kiarabu,” ambapo alieleza kuwa katiba zilizotungwa na binadamu zinazounda mifumo ya kisiasa katika nchi za Kiarabu ni katiba zinazotokana na masharti ya muundo na maudhui kutoka katika kitambulisho cha Umma wa Kiislamu, ambao uliwezesha mchakato wa kupindua katiba hizi. Kwa sababu haifurahii uungwaji mkono wa watu wengi, pamoja na kuegemezwa kwenye itifaki, maridhiano na maelewano kati ya pande zote za ndani kwa upande mmoja na mabwana zao kutoka dola kuu kutoka ng'ambo kwa upande mwingine.

Alifafanua kuwa, falsafa ya katiba katika mfumo wa Kiislamu inatokana na imani ya Kiislamu. Kwa hiyo, mtawala na mtawaliwa wako chini ya hukmu za kisheria, na hakuna uvunjaji wa sheria kwa mtawala au uasi wa taifa. Mamlaka katika Uislamu hayamilikiwi kikanuni isipokuwa kwa yule ambaye Ummah umemchagua kwa hiari yake, na una haki ya kumshauri, kumhisabu, na kumuuzulu.

Wakili Fakir Haj kutoka Sudan

Wakili, Bw. Faqir Haj kutoka Khartoum, alitoa hotuba kwa anwani “Vizingiti kwa Katiba ya Kiislamu” ambapo aliorodhesha vizingiti kumi vinavyozuia utabikishaji wa Katiba ya Kiislamu, vikubwa zaidi kati ya hivyo ni:

Kuenea kwa wazo kwamba ubwana ni kwa watu miongoni mwa wasomi na wanasiasa katika nchi za Kiislamu, na matokeo yake ni kwamba msingi wa katiba ni utashi wa watu na hauhusiani na dini, iliyochukuliwa kutoka katika itikadi ya kutenganisha dini na maisha. Waislamu wanapaswa kujua kwamba msingi wa katiba yao ni wahyi huu mtukufu; Kitabu na Sunnah.

....Ijapokuwa demokrasia, iliyowavutia Waislamu wengi si njia tu ya kuchagua mtawala, na wala si kiolezo kinachoweza kujazwa na hukmu za Uislamu. Bali, ni mfumo wa serikali unaokinzana msingi wake na jinsi unavyotunga sheria na mfumo wa Khilafah. Msingi wa demokrasia ni itikadi ya usekula; yaani, kutenganisha dini na maisha, ikiwemo dola, na ni njia ya kutunga sheria.

Ustadh Mohamed Ali Bouazizi

Profesa wa sheria Muhammad Ali Al-Bouazizi pia alikuwa na mchango kwa anwani "Sifa ya Sharia ya Kiislamu ni kuwa chimbuko pekee la katiba", ambapo alizungumza kuhusu kustahiki kwa Sharia ya Kiislamu na uwezo wake wa kuwa chimbuko pekee la vifungu vya Katiba, pasi na mengine, kwa kuzingatia mapana ya Uislamu na uwezo wake wa kushughulikia mambo yote ya mwanadamu na mahitaji ya maisha katika nyanja zote, iwe kijamii, kiuchumi au kisiasa.

Wakili Hadi Khader

Wakili  kutoka jiji la Sfax, Bw. Hadi Khader, pia alitoa hotuba yenye kichwa “Mfumo wa Kutabanni: Mbinu ya Kivitendo katika Mada ya Sheria,” ambapo alieleza kwamba utaratibu wa kutabanni ni njia ya kivitendo ya kubadilisha maoni ya kisheria na kifiqhi na fiqhi kwa kutegemeza nguvu ya dalili kutoka ngazi ya kinadharia hadi ngazi ya vitendo, ili rai hizo na fiqhi zigeuzwe na kuwa maandiko halali ya kisheria.

Na akaashiria uwanja ambao kutabanni kwa serikali hufanyika: kila kitu kinachohusiana na mambo ya utawala na mamlaka kinajumuishwa katika kazi ya asili ya kuchunga mambo na lazima ifanyike kwa mujibu wa kanuni moja maalum, ambayo inahitajika na umoja wa serikali. Na akaashiria kwamba ijma ya Maswahaba ilifanyika kwamba kutabanni kuhusiana na dola ni kwa khalifa, na akaregelea kanuni za kisharia katika hilo kama kanuni ya “Sultan ana haki ya kutokea katika wilaya kadri ya matatizo mengi yanavyotokea,” na “Amri ya Imam huondoa mzozo,” na kanuni “Amri ya Imam inatekelezeka, kwa nje na kwa ndani.”

Wakili Hanan Khamiri

Wakili huyo, akitoa maoni yake nchini Tunisia, Bi Hanan Khamiri, Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, alitoa hotuba kuhusu "Miangaza kutoka kwa Rasimu ya Katiba Iliyo Tayari Kutabikishwa", rasimu ya katiba iliyochukuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake Mtukufu, ambapo alionyesha jinsi katiba chanya iliyo lazimishwa juu ya Tunisia kwa upande wa dola za kigeni, jinsi gani zinapiga vita kitambulisho cha watu wa Tunisia. Alitaja mifano ya wazi katika hili, pale aliposema: Lakini walitutengenezea katiba za wanadamu zinazotumikia maslahi ya waandishi wao na walinzi wao wa kikoloni, ili watufunge kwa tuhuma za kukufuru tunaposoma Aya za Mwenyezi Mungu.

Kisha akaangazia kanuni muhimu zaidi za utawala katika Uislamu: Ubwana ni kwa Sharia na mamlaka ni kwa Ummah, na akaonyesha kwamba hali ya Tunisia inaweza tu kuimarishwa kwa katiba ya Kiislamu ya dola ya Kiislamu yenye kufikia mamlaka na uongozi. Alijibu swali kuu la kongamano: Je, ni katiba gani tunayoitaka?

Ustadh Khabib Karbaka

Hotuba ya mwisho ilitolewa na Ustadh Khabib Karbaka, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, ambapo aliwasilisha sehemu ya pili ya “Miangaza kutoka katika Rasimu ya Katiba iliyo Tayari Kutabikishwa”, Rasimu ya Katiba iliyochukuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake Mtukufu, iliyoegemezwa juu ya imani thabiti ya Uislamu yenye dalili za kukatikiwa na yakini (na sio mawazo ya kukidhi hili au lile la watu), imani ambayo ukweli wake umethibitishwa kwa dalili zinazoafikiana na ghariza ya mwanadamu, yenye kukinaisha akili na kuujaza moyo utulivu wa kweli. Dhamana ya kwanza ya kushikamana na katiba na sheria zilizotabanniwa kama hukmu za kisheria kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo kushikamana kamili na sheria hutokana na kushikamana kiakili, si kwa chuma na moto.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Video Kamili ya Amali ya Kongamano

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu