- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mustakabali wa Vita vya Kisasa na Dori Iliyokosekana ya Khilafah
Na: Dkt. Abdul Rahman Irfan – Wilayah Afghanistan
Gazeti al Al-Rayah – Toleo 557 - 23/07/2025 M
(Imetafsiriwa)
Vita vinavyoendelea katika sehemu mbalimbali za dunia—hasa vita kati ya Urusi na Ukraine na mzozo kati ya Iran na umbile la Kiyahudi—vinaonyesha wazi kwamba ulimwengu umeingia katika awamu mpya na tofauti ya vita vya kijeshi na kijasusi. Mtazamo wa kale wa vita, uliopitwa na wakati, unaojengwa juu ya vikosi vikubwa vya askari wachanga, vifaru, na mizinga, unabadilika kwa kasi na kuporomoka. Leo, dola kama vile Marekani, China na Urusi zinatenga bajeti kubwa kwa viwanda vya juu vya kijeshi na zinafafanua upya mbinu mpya za kivita. Vita kwenye mstari wa mbele wa kisasa havikomei tena kwa risasi na bunduki – ni vita vya operesheni za kimahesabu (algorithms), akili ya bandia, droni, mtandao na mawimbi ya satelaiti.
Nchini Ukraine, droni rahisi za kibiashara zimefanikiwa kuangamiza vifaru na ndege za Urusi. Mjini Gaza, umbile la Kiyahudi limefanya mauaji makubwa kwa kutumia maelfu ya droni zinazoendeshwa na AI, na katika siku ya kwanza ya vita, liliwaua makamanda kadhaa wakuu wa jeshi la Iran. China imepanua jeshi lake la mtandao, na Marekani inawekeza katika kizazi kijacho cha silaha za leza na vita vya kielektroniki.
Ushindani huu unaokua unabeba ujumbe wazi na mzito kwa vita vya siku zijazo: Nchi zinazoongoza katika teknolojia ya kijeshi na tasnia ya ulinzi zitakuwa nguvu kubwa. Vita vya mustakabali vitakuwa na utegemezi mdogo kwa wanajeshi wa kibinadamu na kutegemea zaidi mashini zinazofanya kazi bila kuchoka, bila uoga, na bila hitaji la kupumzika. Katika muongo ujao, roboti zenye umbo la binadamu (humanoid) zitaingia hatua kwa hatua kwenye safu za utendakazi wa majeshi wa hali ya juu. Mifumo ya otamatiki itachukua nafasi ya marubani wa kibinadamu, droni zitafanya upelelezi na misheni ya kushambulia, na mamlaka ya kufanya maamuzi yatahamishiwa kwenye operesheni ngumu za kimahesabu. Katika vita hivi vijavyo, ubora hautaamuliwa tena na ushujaa wa kimwili, bali akili, teknolojia, na uwezo wa kutumia kwa ufanisi mbinu na zana za hali ya juu.
Swali la msingi ni: sisi Waislamu tunasimama wapi katika mlingano huu? Uhalisia mchungu ni kwamba leo hii, Khilafah ya Kiislamu – ambayo wakati mmoja ilikuwa mstari wa mbele katika uwezo wa kijeshi na ubunifu wa medani ya kivita – haipo tena. Tunakosa dola ambayo sio tu inaulinda Ummah bali pia inamiliki uwezo wa kuhami na mpango wa kijeshi.
Historia yetu imejaa mifano angavu ya ubora wa kijeshi. Wakati wa zama za Khilafah, Waislamu walipata ushindi mkubwa sana katika vita kama vile Vita vya Khandaq, Mu'tah, Yarmouk, Nahavand, kutekwa kwa Sham na Konstantinopoli—licha ya kukabiliwa na maadui ambao walikuwa wakubwa zaidi kwa idadi na vifaa—kupitia mkakati sahihi, uvumbuzi wa uwanja wa vita, na imani isiyoyumba. Inasikitisha kwamba leo, kwa kukosekana kwa Khilafah, Ummah huu huu umekuwa mhanga wa milipuko ya mabomu na vita vya wakala ndani ya ardhi zake wenyewe.
Kama Khilafah haipo leo, je, sisi kama Ummah tunapaswa kubaki tu tumelala na watazamaji tu? Sivyo kabisa. Ni faradhi juu yetu kujitahidi kwa nguvu na uwezo wetu wote kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya utume. Juhudi hii si wajibu tu wa kidini; Ni haja ya dharura kufidia vikwazo vya kifikra, kisiasa na kijeshi vya Ummah ambavyo tunateseka kutokana navyo.
Kwa mtazamo wa Kiislamu, fahamu ya i‘dad (matayarisho)—kama ilivyoamrishwa katika Qur’an:
[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِن قُوَّةٍ]
“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo” [Al-Anfal: 60] sio hatua ya kitaalamu inayoanza baada ya kusimamisha Khilafah; bali, ni faradhi ya kihistoria inayoendelea kwa Ummah. Maandalizi katika ngazi zote—kutoka kwa mtu binafsi hadi kwa pamoja—ni wajibu wa kidini, na kupuuza kunachukuliwa kuwa ni kuasi amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Ingawa utambuzi kamili na uliopangwa wa i’dad unawezekana tu chini ya uongozi wa Khilafah, hii haimaanishi kwamba Ummah hauwajibiki kabla ya kusimamishwa kwake.
Ni muhimu kwa Waislamu kuanza kuweka msingi wa nguvu za kijeshi kwa kukuuza mwamko wa kisiasa na kijeshi ndani ya Ummah, kuanzisha mitandao ya kisayansi, na kuunda timu za utafiti zinazolenga viwanda vya kijeshi. Hatuwezi kungojea tu kuunda serikali na kuanza kujiandaa. Kinyume chake, wakati Khilafah inaposimamishwa, lazima tayari kuwe na mafunzo na kutayarishwa timu za kiufundi, uhandisi, kijeshi, na uongozi mahali pake, ili Khilafah iweze kubadilika kwa haraka kutoka kwenye hali changa na kuwa nguvu ya kijeshi ya kimataifa. Hiki ndicho hasa ambacho dola za kimataifa zimefanya, na haifai kwa Umma wa Kiislamu kubaki nyuma.
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba Ummah ambao haujajiandaa utazuia dola yake, lakini Ummah ulioandaliwa utainyanyua hadi kwenye utukufu na izza. Sisi, kama Ummah, tuna jukumu la kubeba bendera ya Uislamu na kuongoza wanadamu—na uongozi huu hauwezi kufikiwa bila dola yenye nguvu na vifaa kamili, hasa katika uwezo wa kijeshi, kiteknolojia, na kiviwanda. Umma wa Mtume Muhammad (saw) haukusudiwi kuwa mtazamaji tu wa maonyesho ya nguvu za wengine; badala yake, ni lazima wenyewe uwe ndio mwandaaji wa mageuzi makubwa zaidi ya kijeshi na kiteknolojia ya karne hii. Na njia hii inaanza leo, kwa kazi ya kifikra na kisiasa kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.