Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Gazeti la Al-Rayah.

Ugonjwa wa virusi vya Korona na Muungano wa Ulaya

 Je, Virusi hivi Vitauvunja? Au Je, Wataendelea Kukithiri Kulia?

Kipi Kitawatokea Waislamu na Kipi Wafanye?

 Na: Bw. As’ad Mansour

(Imetafsiriwa)

Ugonjwa huu hakika umeathiri Ulaya kama ulivyo athiri wengine, kutatanisha nchi zake kwa sababu ya uharaka wa kusambaa kwake na kukosa kwao uwezo wa kuukabili, wa kihisi unyonge mbele ya virusi hivyo. Hiyo ndio sababu, hata kama wao ni masekula, wametafuta msaada katika dini, na wameruhusu Waislamu kunadi miito ya swala kupitia vipaza sauti katika anga za miji mikuu, lakini janga litakapo malizika, je unyanyasaji wa kidini utakoma? Haswa kwa vile hawakubuni sheria kwa manufaa ya Waislamu, badala maamuzi haya ni ya mda mfupi tu. Hivyo basi, sera zao kwa Waislamu hazito kabiliwa na mabadiliko makubwa. Hata haki rahisi ya Waislamu, kama vile vazi la mwanamke la kisheria, sheria ya kuchinja na kunadiwa kwa swala bado yanazuiliwa. Lakini kupungua kwa uadui wao kumeshuhudiwa kwa kiasi fulani.

Pindi wazalendo wakaidi ndani ya Ujerumani walipoona Waislamu wakiingiliana na kupeana msaada kwa watu wakati wa janga, walisema, “Waislamu wanajifaidisha kupitia janga la Korona.” Lakini sauti za watu hao zilikuwa chini, kwani hawakuweza kutenda, kupeana maoni na suluhu, au kufanya lolote kwa watu wao, hivyo wakatupa chuki na wivu wao kwa Waislamu, na hili ndio lengo pekee la kazi yao, kwa vile wamefilisika kifikra na kisiasa. Hivyo basi, hawakuweza chukua jukumu ama kupeana suluhu, na umaarufu wao ukashuka, hivyo matarajio yao ya kuenuka yakawa dhaifu, na hili limetambulika Ulaya yote, kana kwamba wamejificha nyuma ya utaratibu unaoendelea wa serikali kwa mapungufu yao, sawa na kungojea nafasi katika kufeli kwa serikali na kwa matatizo kutokea ili waweze kuenuka. Umaarufu wa chama tawala umeongezeka, haswa Ujerumani; Kufikia sasa, kimeweza kudhibiti janga kwa kupeana huduma za kiafya na misaada ya kifedha kwa watu walio athirika, na kuzuia ukiritimba wa bidhaa na bei zake za juu. Watu pekee wanao wasaidia na wanao fanya kazi nyingi, haswa wahudumu wa afya ikiwemo madaktari na wauguzi ni vijana wa Kiislamu.

Virusi vya Korona vimekuwa jaribio kwa Muungano wa Ulaya, kuonesha kiwango cha ushirikiano na ujasiri wao. Mnamo 26/3/2020, Raisi wa Ufaransa Macron alisema, “Kilicho hatarini ni uhai wa mradi wa Ulaya… Hatari tunayo kabiliwa nayo ni kifo cha Schengen.”

 “Katika mtazamo wangu, Muungano wa Ulaya unakabiliwa na mtihani mkubwa zaidi tangu kubuniwa kwake, tunakabili changamoto kubwa ya kiafya ambayo imeathiri nchi zote hata kama kitofauti, kitu muhimu ni kwamba muungano uibuke imara kutoka kwa janga la kiuchumi lililo sababishwa na virusi hivi, “Chansela wa Ujerumani Merkel alisema mnamo April 7, 2020.

Viongozi hao wawili wa Muungano wa Ulaya wameonya dhidi ya kuanguka, na kama muungano umefeli kushughulikia janga hili, kwamba umeshidwa kubuni mipango ya pamoja inayomfunga kwa kila mmoja ili kufaulisha ushirikiano na umoja. Bali, wamefungiana mipaka wao kwa wao, na imani juu ya makubaliano ya Schengen ikatetemeshwa; Makubaliano Mipaka Wazi na Uhuru wa kutembea na biashara. Wakatuhumiana kwa kutoshirikiana, kila nchi ikaanza kijifikiria kibinafsi na kuzuia wengine kufikia vifaa vya kiafya. Ubinafsi ukatokea katika hali yake halisi yakutisha, hakika ni asili yao kama warasilimali, na hakuna makubaliano watakayo weza kuondosha asili hiyo, hivyo Wataliani wakanadi kujiondoa katika muundano. Hivyo, kukosekana kwa utulivu katika muungano ilikuwa kawaida, kwa sababu ni muungano tete.

Muungano huenda usianguke sasa kutokana na kuhitaji kwao msaada, lakini hilo lilipanda mbegu mpya wa kutoamiana ambayo sasa ndicho kiini cha kuporomoka, huku ukiwa ungali unateseka kutokana na mshtuko wa kujiondoa kwa Uingereza (Brexit). Ni vigumu kwake kuwa muungano kwa maana yake halisi baada ya janga la virusi vya korona, hivyo wasiwasi wao umekuwa ni kulinda kile walicho faulu, kama vile makubaliano ya Schengen. Umeshidwa kufanya maendeleo muhimu katika umoja wa maamuzi ya kisiasa katika sera za pamoja za ndani na nje, mfano, Poland, Hungary, Slovakia na Jamhuri ya Czech walikataa uamuzi wa Muungano wa kugawa wakimbizi baina yao wa mnamo 2015-2016, na bado zinashidwa kubuni jeshi la Ulaya.

Huu ni mda wa afueni kwa muungano, kama hautaharakisha kuziokoa nchi zake zilizo athirika vibaya, hatima yake itakuwa shimoni. Hii ndio sababu Waziri Mkuu ya Uhispania Pedro Sanchez alionya mnamo April 5, 2020, akisema: “hali zilizopo ni za kipekee na zinahitaji misimamo thabiti, ima tuenuke juu ya changamoto hii ama tutafeli kama Muungano…Tumefika hatua muhimu ambayo hata nchi na serikali zinazo unga mkono Muungano, kama ilivyo hali nchini Uhispania, zinahitaji agano halisi la kujitolea kwa Muungano kwao... Changamoto tunayo ikabili ni ya ki pekee na isiyo kuwa ya kawaida, inahitaji umoja, wa kiasi kikubwa na hatua kabambe ili kuhifadhi uchumi wetu na hali yetu ya kijamii na kulinda raia wetu.

Haya yote yamenasibishwa na viongozi wa Muungano, Ufaransa na Ujerumani. Tukifahamu kwamba Ufaransa imeharibiwa vibaya, Waziri wake wa Fedha Bruno Lemerre alisema mnamo Aprili 6, 2020: “Ufaransa inao uwezekano wa kushuhudiwa mporomoko mbaya wa kiuchumi tangu Vita vya Pili vya Dunia, mbaya zaidi ya kiwango cha mshuko cha asilimia 2.2 cha 2009 baada ya janga la kiuchumi duniani la 2008… Na kitashuka kwa asilimia 1 mwaka huu.” Hata hivyo, Ufaransa inataka kuthibitisha uongozi wake katika Muungano, hivyo Raisi wake ameelezea kujitolea kwa Ufaransa kupeana msaada kwa Italy, ambayo imekashifu serikali za Ulaya, ikiongozwa na Ufaransa na Ujerumani, kwa kutoshughulikia utoaji wa barakoa na vifaa vyengine vya kimatibabu. Alisema: “Hatutoshinda janga hili bila ya Umoja imara wa Ulaya katika viwango vya kiafya na kifedha,” na akatoa wito wa kuzinduliwa kwa mkopo wa pamoja kati ya Muungano mzima wa Ulaya ili kukabiliana na virusi vya Korona, huku Ujerumani inapinga ukusanyaji wowote wa deni, na inataka kitu kingine kuidhibiti Ulaya.

Ulaya iliharibika katika Vita vya Pili vya Dunia, hivyo Amerika ikazindua mpango Marshall ili kupeleka pesa na kampuni zake hadi Ulaya, lakini ililipa gharama kubwa sana kwa hilo, nayo ni, kwamba Ulaya ikaanguka chini ya mamlaka ya Amerika, ambayo mpaka sasa haijajikwamua. Lakini Amerika haiwezi kuisaidia Ulaya kwa sasa, kwani itang’ang’a kujinusuru yenyewe baada ya janga lililo sababishwa na maambukizi litakapo kwisha, na hakuna dhamana ya mafanikio. Hapo nyuma ilizindua kauli mbiu “Amerika Kwanza” na ikatangaza vita vya kibiashara juu ya Ulaya na wengineo ili kujinusuru kutokana na athari za janga la kiuchumi la 2008.

Kuna uwezekano kwa Ujerumani kuathirika kidogo kiuchumi na kupoteza maisha, ina mizani kubwa ya kifedha na uwezo mkubwa wa kiviwanda, hivyo ni kama itapeleka pesa na kampuni zake kwa nchi nyingine za Ulaya zaidi ya inavyo fanya sasa. Itakuwa ni fursa kwa Ujerumani kumiliki Ulaya na kukuwa kwake kama nguvu ya kiulimwengu, kitu ambacho imekitafuta kwa miaka mingi, lakini hili linanasibishwa na ufahamu wa wanasiasa, ujasiri wao na hatua mwafaka.

Hata hivyo, Urasilimali unakaribia kuanguka na nchi zake kusambaratika. Ujerumani haitasaidia hata ikipaa, na haiaminiki kwa Ulaya na wengine kwa sababu ya giza la historia ya Nazi. Kile kilicho baki pekee ni itikadi sahihi ya Kiislamu; kunayo fursa kwa Ummah wa Kiislamu kuinuka, lakini kuna changamoto kubwa ambayo lazima iondolewe, ambayo ni serikali na watawala, kwani wanachokitaka pekee ni kunasibishwa na dola kuu za kikoloni. Ikiwa moja itaanguka, wataifuata nyengine! Ama kwa sasa, tunategemea kwa ikhlasi, ufahamu wa vyama vya kisiasa vya Kiislamu ambavyo vimemakinisha fikra za Kiislamu na kubuni katiba yake, kikiainisha nidhamu zake, taratibu za kiidara utawala na uongozi and njia za utabikishaji, na kuandaa wanaume walio na sifa za kuwa watu wa dola. Jukumu liko juu ya kila Muislamu katika Ummah huu ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewapa amana ya jukumu la kuwaokoa wanadamu, kwa kufanya kazi na wafanyikazi watiifu ili kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ambayo kihakika itafanya kazi hii kwa niaba yao na pamoja nao.

Chanzo: Gazeti la Al-Rayah Toleo 284, Imechapisha Mnamo 29/04/2020

#Covid19    #Korona     كورونا#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu