- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Amali za Kilimwengu za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa kwa Khilafah 1446 H – 2025 M
Khilafah Rashidah kwa Njia ya Utume
Yenye Kuokoa Ulimwengu na Wanadamu
Katika mwezi wa Rajab Mtukufu mwaka huu 1446 H - 2025 M, tunakumbuka kumbukumbu mbaya ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Waarabu na Waturuki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Wakati huo huo mauaji ya kikatili na mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile nyakuzi na la kutisha la Kiyahudi yanaendelea dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa zaidi ya Waislamu elfu 170, wanaume na wanawake, hadi sasa, ambao wengi wao ni wanawake, watoto na wazee. Kwa upande mwingine, mapinduzi yaliyobarikiwa ya Ash-Sham yamefikia kitovu cha Makao ya Uislamu (ash-Sham) na kumng’oa dhalimu wa Damascus, lakini bado yanapitia mchakato mgumu na hatari katika jaribio la kutoroka kutoka kwenye mshiko wa mfumo wa dunia pamoja na nchi zake zote na vyama vyenye uadui kwa Uislamu na Waislamu!
Kutokana na hili, Hizb ut Tahrir inaandaa amali mbalimbali za umma katika nchi zote ambazo inaendesha shughuli zake za kuwahamasisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ni Khilafah peke yake ndiyo itakayotoa izza duniani na wokovu kesho Akhera, na ndiyo pekee yenye uwezo wa kukomboa ardhi na wanadamu kutoka kwa makafiri wahalifu na kutoka kwenye vitimbi vya Kafiri Magharibi dhidi yetu!
Na sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu akipenda, kupitia ukurasa huu tutaangazia kwa kina amali hizi, tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Ijumaa, 10 Rajab Tukufu 1446 H sawia na 10 Januari 2025 M
Ujumbe kutoka kwa Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
kuhusu Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
Ujumbe kutoka Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
kuhusu Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah | |
#أقيموا_الخلافة |
#EstablishKhilafah | |
YenidenHilafet# |
#خلافت_كو_قائم_كرو |
Al-Waqiyah TV
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Kama vile Yalivyo anza na “Ni ya Mwenyezi Mungu,” lazima Yamalizike na “Ni ya Mwenyezi Mungu”! Imetolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki Kwa ushirikiano na Al-Waqiyah TV Ijumaa, 25 Jumada Al-Akhir 1446 H sawia na 27 Disemba 2024
|
Wilayah |
K Rajab 1446 H - Januari 2025 M |