Jumamosi, 09 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nidhamu ya Elimu ya Msingi Katika Khilafah ya Uthman

Kampeni mbaya dhidi ya Waislamu na Uislamu zimekuwepo tangu kuteremshwa kwa Aya ya kwanza ya Quran. Yaliyokuwa madai ya kawaida zaidi ni yale yaliyotolewa na wale wanaotamani kuushambulia mtazamo wa Uislamu juu ya maisha ni kwamba mafunzo ya Uislamu yanapigia debe ujinga, ufuataji wa kipofu, kujenga watu wasiojali wenzi wao na wasio heshimu maendeleo ya kiteknolojia na kijamii hususan masuala yanayohusiana na wasichana na kuwawezesha kupitia elimu.

Lakini lau tutatathmini kwa makini ushahidi wa kihistoria kwa uadilifu tutaona kwamba Nidhamu ya Kisiasa ya Kiislamu imeipa elimu na kusoma kipaombelea cha juu kwa wanaume na wanawake.

Uislamu unapigia debe ufahamu safi kwamba kutafuta elimu ni kitendo cha ibada ambacho kitanyanyua daraja ya mtu hapa duniani na kesho akhera.

 (أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاء اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ)

“Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitarajia rehema za Mola wake Mlezi? Sema: Ati watakuwa sawa wale wanaojua na wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.” [Azzumar: 9]

Ni ruwaza hii ya mafanikio ndio iliyo wasukuma watawala wa Kiislamu ili kushajiisha masomo kwa wengi ili kuweza kuifahamu Quran na Sunnah. Dola ya Kiislamu ya kwanza ndani ya Madina iliasisi tamaduni ya kusomesha ummah tangu mwanzoni ulipojengwa Msikiti wa Mtume ambao ulitumika kama sehemu ya kuwafunza wadogo na wakubwa pamoja na kuwa ndio kituo msingi cha mujtama kwa jamii ya Waislamu.

Jukumu la Uislamu la kusomesha lilipelekea kuanzishwa kwa Chuo cha Kiislamu cha kwanza duniani kiitwacho Al Qarawiyyin katika mji wa Fez, Morocco.

Harakati za uvumbuzi katika elimu zilizifanya ardhi za Waislamu kuwa ndio kiongozi wa dunia katika nyanja za maarifa na usomi, kwa kiasi kikubwa mpaka watu muhimu kutoka nje ya ardhi za Waislamu walitaka kusomesha raia wao ndani ya Dola ya Khilafah katika zama tofauti tofauti za historia. Khilafah ya hivi majuzi ni ile ya Uthman ndani ya Uturuki, ilikuwa na mpagilio wa elimu ambao ulikuwa unashindana na wa taasisi nyingi zilizopo leo. Kwa mujibu wa Bwana Paul Ricaut (Muingereza Mwanadiplomasia, mwanahistoria na mjuzi kuhusu Ufalme wa Uthman), “Nidhamu ya elimu na kuadhibu ya Waturuki ni moja katika nguvu zao muhimu za siasa na ambazo zinamakinisha ufalme. Katika nidhamu hii si utajiri wala hongo wala si utabaka wa juu au ukaribu hauangaliwi, isipokuwa kinachotizamwa ni wema, umakinifu, uwajibikaji na tabia njema. Sultan mwenyewe amesimama kwa msingi wa sifa hizi.”

Tukizingatia kuwa miaka 600 ya Khilafah ya Uthman ilijumuisha kilomita mraba milioni 14 za ardhi ambazo zilijumuisha Waturuki wa Cypriot, Wagiriki, Wabulgeria, Wapomak, Wasabia, Wakrosia, Wamontenegro, Wabosnia, Waablania, Wahangari, Wapole, Warumi, Waarmenia, Wajojia, Wasyria, Wachaldi, Waarabu, Waromania, Wafursi, Wakurdi, Wakopti, Waithiopia na Wabarbar, matamshi ya Ricaut yanadhihirisha kiukweli namna nidhamu ya elimu ya Khilafah ilikuwa ni yenye kujumuisha ambapo fursa ya mtu kusoma na kujiboresha haikukatazwa mtu, tatizo ambalo mpangilio wa kisiasa uliopo leo umeshindwa kulitatua kwa ukamilifu. Pamoja na mchanganyiko huo mkubwa wa jamii na tamaduni  chini ya mamlaka moja pia tunao namna nidhamu ya elimu ya Kiislamu ilikuwa ni kiunganishi kikubwa kwa kuwa utaifa hauna thamani katika mfumo wa Kiislamu, aya kutoka katika Quran ilifundisha hivyo:

(يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ)

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mataifa na makabila ili mjuane (SIO KWAMBA MCHUKIANE).” [Hujuraat: 13]

(وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ)

“Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.” [Ar-Rum: 22]

Huku akili changa zikitambulishwa fikra aina hizo, utambulisho ulijengwa kuanzia katika umri mdogo kuweza kuwa na uvumilivu na ubinadamu kwa watu wote kwa kuwa wameunganishwa kama raia wa Khilafah. Kwa hivyo ushindani na chuki za kidini zilikuwa kwa kiwango cha chini ambayo ilipelekea mujtama kuwa salama na usiokuwa na madhara.

Tathmini ya elimu ya Msingi pekee itadhihirisha namna kiukweli Uongozi wa Khilafah ya Uthman ulikuwa uko kipaombele katika kuhakikisha kunapatikana nafasi ya kivitendo ya elimu yenye kusifiwa kwa watoto wachanga ambao wako katika usimamizi wao. Katika Khilafah ya Uthman shule ilianza umri wa miaka 3 katika zile zijulikanazo kama Shule (Mektepleri) za Msingi (Sibyan)

Katika makala yake iliyochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Watu na Sayansi ya Kijamii mnamo 2013, Professa Dkt Selami Sonmez wa Chuo cha Ataturk kutoka Uturuki aliorodhesha malengo ya elimu ya Msingi katika Khilafah ya Uthman kama ifuatavyo: 

1. Kufundisha watoto wa Waturuki na Waislamu kusoma Quran kwa ufasaha na kuandika kwa Kiarabu vizuri

2. Kufundisha mambo ya msingi ya Uislamu

3. Kufundisha aina za ibada katika Uislamu

4. Kufundisha misingi ya maadili katika Uislamu na tamaduni.

5. Kuwasilisha na kufundisha maadili ya kweli ya Kiislamu.

6. Kutambua uwezo wa watoto

7. Kuandaa wanafunzi kwa Madrasa


Shule ima zilidhaminiwa moja kwa moja na serikali yenyewe au zilijengwa na kufadhiliwa na watu matajiri au makundi ya kijamii yakishirikiana kuelimisha vijana. Ilikuwa si jambo la ajabu kuona shule hizo zikifungamanishwa na msikiti wenyewe.

Ergin Osman katika kitabu chake cha 1977 cha, Historia ya Elimu ya Uturuki, aliandika kuwa ilikuwa ni umuhimu mkubwa kuelimisha kila nyanja ya jamii kwa serikali ya Uthman kiasi kwamba Fatih Sultan Mehmet alianzisha fikra ya kuweka kiwango maalum cha shule ambazo ziliruhudu watoto kutoka katika familia masikini au mayatima kuweza kuhudhuria ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote asiyejiweza anakosa haki ya kupata elimu. Akaweka kanuni rasmi za elimu ya shule ya Msingi:

a. Elimu katika Shule za Msingi zilikuwa bure.

b. Matumizi ya kila siku ya 2 akche yalipeanwa.

c. Nguo, fez, shati, suruali, mikanda, viatu na kofia ziligawanywa kwa watoto wote.

d. Chakula kilipeanwa.

e. Safari iliandaliwa kila mwaka.

Ilikuwa sio jambo la ajabu kwa familia tajiri kudhamini watoto masikini hivyo basi kupelekea uwiano wa mujtama katika Dola ya Kiislamu.

Pia akataja kuwa siku ya kwanza kwa mtoto shuleni ilikuwa ni jambo kubwa la kijamii na kithaqafa kiasi kwamba wazazi, matajiri na masikini wangeli andaa sherehe maalum na maonyesho ya mtaani ili kusherehekea tukio hilo adhimu. Tamko rasmi la tukio hilo lilijulikana kama " Maonyesho ya Amen ya Watoto." Ahmed Rasim katika kazi yake ya 1927 ya Falaka. Istanbul imeelezea kwa undani sherehe hiyo kama iliyo jumuisha kuwalisha ndugu na marafiki na mtoto kutuzwa zawadi na kuvalishwa nguo mpya nzuri na dua kutolewa kwa mafanikio yao.

Mpangilio kabambe wa sherehe hiyo ya siku ya kwanza kwa mtoto shuleni ilikuwa na dori muhimu katika mujtama ifuatavyo:

a. Kushajiisha wazazi ili wawapeleke watoto wao shuleni

b. Kushajiisha mababa wa watoto walioko karibu na shule ili wawapeleke watoto wao shule

c. Kushajiisha mtoto kuanza shule

d. Kushajiisha kina dada na kaka walio na umri mkubwa pamoja na watoto majirani kuanza shule

e. Kupeana hadhi kwa familia ya mtoto

Osman Ergin ana nukuliwa katika utafiti wake wa 1977 uliofichua kwamba umuhimu wa shule kwa mujtama hauwezi kupatikana “ndani ya taifa lolote katika historia yake ya elimu!"

Dkt Selami Sonmez (2013) ameandika kwamba mbinu za mafunzo zilikuwa nyepesi ili kuweza kuruhusu watoto kusoma kwa kadri ya uwezo wao na watoto waliokuwa na uwezo zaidi waliruhusiwa kusonga mbele mara moja na wasiokuwa na uwezo walitengewa muda zaidi ili kuweza kufaulu. Madarasa makubwa yalisaidiwa na wanafunzi mahiri ambao walichaguliwa kama 'wasomeshaji wasaidizi' kwa wanafunzi wengine, hali ambayo imeigwa sasa na nidhamu ya shule za magharibi.

Kwa mujibu wa ushahidi wa kihistoria na kijamii ambao upo tunaweza kuhitimisha kwamba mpango wa elimu ya Msingi wa Khilafah ya Uthman unafichua wazi kwa ukamilifu uongo wa eti nidhamu ya kisiasa ya Kiislamu haina heshima kwa elimu, maendeleo na uelimishaji wa wasichana. Kinyume chake ni kwamba vikwazo vilivyoko katika kuweza kupata elimu kwa raia wanaoishi katika nchi zilizo kuwa kidemokrasia kutokana na utajiri, jinsia, kabila na utabaka vinajulikana na mataifa yote ya kimagharibi yanakumbana na janga hilo linaloendelea ambalo ni kuweza kuweka usawa wa kiukweli kwa raia wake.

Katika mwaka huo huo wa 2013 katika makala iliyotajwa hapo awali, Dkt Selami Sonmez alinukuu kwamba sifa nzuri za Nidhamu ya Elimu ya Khilafah ya Uthman zilikuwa:

 “... hata kwa dunia ya leo, sifa na dori ya Shule ya Msingi… ni jambo la ziada, na zipo nchi nyingi ambazo hazijafikia kiwango hicho." (Nidhamu ya Elimu ya Msingi ndani ya Ufalme wa Uthman, Professa MsaidizI Dkt Selami Sonmez Chuo cha Ataturk 2013)

Tukijihami na elimu hii sasa tunaweza kutathmini khofu yetu ya kurudi tena kwa nidhamu ya Kiutawala wa Siasa ya Kiislamu na badala yake tubebe ruwaza njema, iliyojaa matumaini na kushajiisha watu wote kutokana na uwezo wake mkubwa wa kunyanyua wanadamu kwa kurudi tena Khilafah, Dola ya Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 14 Februari 2020 07:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu