Ijumaa, 30 Shawwal 1447 | 2026/04/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Kwa Kukosekana Khilafah Wanawake Waheshimiwa wa Ash-Sham Wanakabiliwa na Kudhulumiwa Hata na Wale Wanaodai Kuwa Walinzi Wao!!!

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia ufadhili wa watu (UNFPA) limesema kuwa wanawake katika kambi za wakimbizi nchini Syria wamekuwa wakidhulumiwa kimapenzi na wanaume wanaotoa misaada kwa niaba ya UM na mashirika ya kimisaada ya kimataifa. Ripoti hiyo, “Sauti kutoka Syria 2018”, ili eleza kwa kina namna wanawake wakimbizi wa Syria wanavyo lazimishwa kutoa ngono kama badali kwa chakula kutoka UM, na kwamba dhulma hii imeenea maeneo yote kusini mwa Syria.

Watoto wa Mashariki Mwa Ghouta Wanaangamizwa! Ni Nani Atakaye Hifadhi Damu Zao?!!

Mnamo 22 Februari, shirika la Kiingereza la kuchunguza haki za kibinadamu za watu wa Syria lilisema kuwa zaidi ya watu 400 waliuwawa, ikiwemo watoto 150 katika shambulizi baya la mabomu lililopita la siku 5 Mashariki mwa Ghouta lililofanywa na majeshi katili ya Syria na Urusi, ambayo yanalenga kiholela nyumba za raia, maduka, mashule, mahospitali na masoko, yakiwaacha watoto wakiwa wamezikika katika vifusi vya majumba. Watoto wamelazimika kutafuta hifadhi katika mapango, mashimo au mivungu ya nyumba zao huku 'wakisubiri zamu yao kufa'.

UN – Wanaotarajiwa Kuwa Walinzi Ndio Wauwaji!!

Gazeti la Uingereza la The Times, lilichapisha ripoti kwa kichwa "Wafanyikazi wa UM 'wanahusika na ubakaji 60000 kwa muda wa muongo mmoja'". Ripoti hii inajiri wakati ambapo kumetukia uenezaji mkubwa wa habari na gazeti hilo kuhusu kufichuka kwa kashfa hii iliyo yashtua mashirika ya "misaada"; ambapo lilichapisha katika ukurasa wake wa mbele ripoti inayofichua kuwa shirika la Oxfam lilikuwa limemteua Roland Van Hauwermeiren kama mkurugenzi wa tawi lake la Haiti, ambaye hatimaye alikuwa katikati ya kashfa ya kuhusika na makahaba wakati wa shughuli za uokozi za shirika hilo kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Haiti, miaka miwili baada ya kutimuliwa kutoka kwa shirika jengine la misaada la Kiingereza kwa madai ya kuwatumia makahaba vile vile!

Makongamano ya Kimataifa, Mipango ya Amani, Pasi na Kukomesha Wala Kupunguza Mashambulizi ya Mabomu ya Urusi!

Matukio ya umwagikaji damu yanayojiri Mashariki mwa Ghouta na Idlib; Mtandao wa Kutetea Haki za Kibinadamu wa Syria umesema kwamba raia wapatao 370 wameuwawa Mashariki mwa Ghouta tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ukitaja kuwa miongoni mwa wafu ni watoto 63 na wanawake 72. Katika eneo la Idlib, hususan mji wa Sarakib, ambao ndio uliolengwa kwa dhoruba hii tangu mnamo 25 Disemba, Warusi na serikali ya kihalifu ya Syria zimemwaga chuki zake dhidi yake, ikitangazwa na baraza lake la mji kuwa eneo lililo kabiliwa na janga, ambapo idadi ya vifo mwezi Januari ilikuwa ni watu wapatao 30 na zaidi ya raia 60 kujeruhiwa. Hii ni ikiongezewa na kulengwa kwa mashule na mahospitali, ambazo idadi yake kubwa haziendeshi tena shughuli zake.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu